Sheikh apinga Urais kwa mwanamke

Sheikh apinga Urais kwa mwanamke

Wapi Biblia ilikataza bwashe?

Mwanzo 3:16.....tamaa yako itakuwa KWA mumeo nae atakutawala" Uongizi alipewa mwanaume bwashee.Pia ongeza 1korintho 11:3 "kichwa cha kila mwanamume ni Kristo na kichwa mwanamke ni mwanamume na kichwa cha Kristo ni Mungu" pia 1korintho 11:6 ......mwanamke ni utukufu wa Mwanamume.Zaidi soma kutoka 18:17-27 kama utakuwa hujaelewa nitafte KWA maelezo zaidi
 
Shehe ubwabwa huyo!
Umemaliza mjadala,huyo Sheikh Ubwabwa.Yupo Mwanamke anaitwa Balkiss,alikuwa mtawala,na Qur'an imetaja kisa chake.Na Qur'an haikupinga utawala wake.

Zipo Chapter,ndani ya Qur'an ,imeitwa kwa jina Maryam,na ni Mwanamke huyu.

Yupo Bi Asia,ametajwa ndani ya Qur'an.

Yupo Bi Aisha,mpaka leo waislamu ,dunia nzima,anawaongoza,kwa kufuata hadithi(miongozo),aliyopokea kutoka kwa Mtume Muhammad(S.A.W.).Mpaka miongozo ya mume na mke,kuanzia chumbani mpaka nje ya chumba.

Wapo kina Bi Khadija,na wemgine kina Sumaiya,walipigana vita.Mama wa Nabii Musa,ametajwa,Mtoto wa kike wa huyu Mama wa Nabii Musa,ametajwa Kwenye Qur'an.
 
Shehe ubwabwa huyo!
images (70).jpeg

Kama huyu mwanalumumba mwenzenu?
 
Tusiwe na mhemuko au jazba tusikilize nasaha, tuwe watulivu kupata darsa toka kwa maulana sheikh Hemed Jalala


Katika siku hizi za Bibi Fatma tunamulika nafasi ya mwanamke kwa mtazamo wa kiislamu na kuangalia riwaya na hadithi zilizochomekwa katika Uislamu ili kumdhoofisha mwanamke, Mwanamke na mwanaume Je wameumbwaje ? Je kuwa mwanamke ni udhaifu?

 
Katika uislamu,hakuna ambaye ataingia Peponi(Paradise),ila kupitia kwa Mwanamke(mama),ikiwa hukumtendea mema mama yako mzazi(Mwanamke)hata uwe Sheikh,au ufanye ibada gani,pepo huipati.

Pepo katika uislamu,iko chini ya nyayo za mama(Mwanamke).Kwa hiyo uislamu umemtukuza Mwanamke(mama),ufunguo wa pepo

Mwanamke katika uislamu,kapewa nafasi kubwa sana,ya uongozi,huyo Sheikh ubwabwa,anataka uongozi gani tena.
Hata katika kulea,katika uislamu,atakaye walea vizuri watoto wake wa kike,mpaka akawafanya harusi zao,basi pepo,imebakia kwake kutenda mema mengine,na kufanyiwa wema wazazi wake(hasa mama)ambaye ni mwanamke.Mama katika uislamu,amepewa daraja zaidi,kumtendea mema kuliko baba.

Sheikh,ubwabwa huyu,hajui huo ndio uongozi,ataka uongozi tena.Huwezi kupata funguo ya pepo,mpaka umfanyiwe wema mama yako(ambaye ni mwanamke).

Ikiwa huyo anayejiita Sheikh,kama hakumfanyia wema mama yake(Mwanamke),ufunguo wa pepo,hataupata,hata afanye ibada vipi.Hapo Mwanamke ,katika uislamu,hajakuwa kiongozi wako?Kwa maana huwezi kuingia Peponi ,mpaka umfanyie wema mama(Mwanamke).
 
Bila kumfanyiya wema Mama(Mwanamke),katika uislamu,huingii Peponi,hata uwe Sheikh,ufanye ibada zote,uzijuazo na usizozijuwa.

Uongozi wa kupata Pepo,katika uislamu uko mikononi mwa Mwanamke(mama).

Hata Maswahaba,walikuwako wanaume na walikuwako wanawake.

Bi Aish,mpaka leo,tunatumia miongozo yake(Hadithi alizopekea kutoka kwa Mtume),zaidi ya 2000.Sasa katika uislamu,kunatakiwa uongozi gani tena.
 
Wengi watamuandama sheikh kwa aliyoyahubiri ila si maneno yake bali ni maneno ya Mtume Muhammad (sala na amani ziwe juu yake) .Na mtume wa Mungu hazungumzi kwa matamanio ya nafsi yake bali ni ufunuo kutoka kwa aliye juu zaidi, ALLAH subhana wa ta3ala.

Dola kubwa nyingi kama persian empire zilianguka pale ambapo masuala yao ya utawala waliowaachia wanawake.

Marekani licha ya upuuzi wao wote hawataki kuruhusu mwanamke awe rais wa nchi yao maana wanajua hizi historia.Hillary clinton alishinda kabisa urais ila alifanyiwa zengwe wakampatia urais Donald Trump.
 
Narrated Abu Bakra: During the battle of Al-Jamal, Allah benefited me with a Word (I heard from the Prophet). When the Prophet heard the news that the people of the Persia had made the daughter of Khosraw their Queen (ruler), he said, "Never will succeed such a nation as makes a woman their ruler."

[Sahih Bukhar]

Katika utawala huu wa mama tutashuhudia mengi tu ,tuombe Mungu atuwezeshe kufika 2030 tukiwa na afya njema. Mtume aliyoyaongea ni ufunuo kutoka kwa ALLAH. Sio matamanio ya nafsi yake.
 
Mtume hajakataza wanawake kuongoza.Leo waislamu tunafuata hadithi(miongozo ya uislamu),kupitia Bi Aisha,na hata huyo Sheikh,kuna mambo ya mume na Mke,anayafundisha na kutafuta kupitia Bi Aisha.Bi Aisha ni Mwanamke sio mwanamme.
Usimzulie uingo Mtume Muhammad (pbuh).Unaposema hakulisema hilo jambo maana yake unamzushia kuwa hakufikisha kile alichofunuliwa na ALLAH.

Ni nani dhalim kuliko yule anayemzushia uongo ALLAH na Mtume wake??

Narrated Abu Bakra: During the battle of Al-Jamal, Allah benefited me with a Word (I heard from the Prophet). When the Prophet heard the news that the people of the Persia had made the daughter of Khosraw their Queen (ruler), he said, "Never will succeed such a nation as makes a woman their ruler."

[Sahih Bukhari]

Chanzo cha kusambaratika kwa dola ya persia (Fursi) ni pale walipomteua binti wa aliyekuwa mfalme wao kuwa ndio malkia (mtawala) wa dola yao. Matokeo yake persian empire ilisambaratika yote na haiwezi kurejea mpk ulimwengu huu unaisha.
 
Katika uislamu,hakuna ambaye ataingia Peponi(Paradise),ila kupitia kwa Mwanamke(mama),ikiwa hukumtendea mema mama yako mzazi(Mwanamke)hata uwe Sheikh,au ufanye ibada gani,pepo huipati.Pepo katika uislamu,iko chini ya nyayo za mama(Mwanamke).Kwa hiyo uislamu umemtukuza Mwanamke(mama),ufunguo wa pepo
Mwanamke katika uislamu,kapewa nafasi kubwa sana,ya uongozi,huyo Sheikh ubwabwa,anataka uongozi gani tena.
Hata katika kulea,katika uislamu,atakaye walea vizuri watoto wake wa kike,mpaka akawafanya harusi zao,basi pepo,imebakia kwake kutenda mema mengine,na kufanyiwa wema wazazi wake(hasa mama)ambaye ni mwanamke.Mama katika uislamu,amepewa daraja zaidi,kumtendea mema kuliko baba.
Sheikh,ubwabwa huyu,hajui huo ndio uongozi,ataka uongozi tena.Huwezi kupata funguo ya pepo,mpaka umfanyiwe wema mama yako(ambaye ni mwanamke).
Ikiwa huyo anayejiita Sheikh,kama hakumfanyia wema mama yake(Mwanamke),ufunguo wa pepo,hataupata,hata afanye ibada vipi.Hapo Mwanamke ,katika uislamu,hajakuwa kiongozi wako?Kwa maana huwezi kuingia Peponi ,mpaka umfanyie wema mama(Mwanamke).
Hakuna hadithi sahihi inayosema kuwa Pepo ya mtu ipo chini ya nyayo za mama ake. Ikiwa una ushahidi wa hadithi sahihi naomba uiweke hapa watu waishuhudie.

Usipindishe kauli za mtume Muhammad (peace be upon him) ili kutetes tumbo lako.

Mtume Muhammad (pbuh) alishasema kuwa hakuna taifa litakaloendelea pindi watakapomfanya mwanamke kuwa mtawala wao.
 
naunga mkono hoja, ni kweli kuna baadhi ya Masheikh ni Masheikh ubwabwa.
Sheikh wa ukweli ni huyu

P

Haya mambo kiongozi wangu yanataka elimu ili uyajue. Inaonekana Uislamu huuji. Hawa wananukuu aya ambayo Wanawake walienda kuunga mkono Uongozi wa Mtume siyo wao wawe viongozi. Sababu mitume na manabii wote huwa ni wafikisha habari na muda huo huo huwa ni viongozi wa juu kwa watu au hata huwa Wafalme kama ilivyo kwa nabii Suleyman.

Huwezi kumjua Sheikh wa kweli kama huna elimu ya dini au ukaambiwa na wajuzi wa Dini. Mtume mwenyewe ndiyo alisema ya kuwa hawatofaulu wale ambao jambo lao waliegemeza kwa Mwanamke, hii ni baada ya yeye kuletewa za watu walio kuwa wanaabudu Jua, watu hawa walikuwa wanaongozwa na Mwanamke.

Mwanamke yeye ni kiongozi kwenye nyumba yake, tena muda ambao sisi wanaumue tukiwa hatupo, kwa maana tunamuachia nyumba yeye kama msimamizi.

Kuhusu Wanaume wengine kutokuwa viongozi bora huo ni katika udhaifu wa mtu mmoja mmoja, ila suala la Uongozi linarudi kwetu sisi, ndiyo maana hapajawahi kuwa na Mtume au nabii wa kike kutoka kwa Mola muumba (hapa siwaongelei hawa wahuni na manabii wa uongo wanao jiita kwa majina hayo hasa wanawake).

Hata kama Mwanamke ataongoza vizuri suala la kutengamaa au kifaulu kwa jamii hiyo halipo, yaani mwisho wa hiyo jamii ni kufeli.

Wakatoa mfano Malkia Balqis , huyu alikuwa ni Malkia baada ya nabii Suleyman kupata hizp habari nini alikisema na mwisho ilikuwaje ? Mwisho alikuja kuwa mke wake (kama mapokezi yalivyokuja). Maana yake hakuwa kiongozi kwa watu wale.

Kwahiyo suala la Mwanamke kuwa kiongozi au kuwaongoza watu si jambo lao.

Shukrani.
 
Huyu Sheikh ni male chauvinist, analeta mambo ya male chauvinism ya kuwabagua Wanawake.

Hapa aitwe Sheikh Mkuu, kulifafanua hili na ikibidi huyu Sheikh avuliwe usheikh.

Mafundisho ya kweli ya Uislamu kuhusu mwanamke wa Kiislamu na uongozi ni haya


P
Mbona kama unatetea sana mkuu. Kwani hakuna ukweli hapo?! Wewe nyumbani kwako mkeo ndio 100% final decision maker??
 
Back
Top Bottom