Sheikh Farid: Tunashukuru tumeachiwa ni mwanzo mwema wa Rais Mwinyi na Samia

Anawashukuru watu?
Kwani haki haijaamua?
Mbona mnatuweka mtanziko?
Kwani wameachiwa na mahakama au na hawa marais wetu wawili?
Kuachiwa kumeambatana na conditions hivyo mengine hautakiwi kuyashangaa.
 
MUNGU mbariki mama samia,
Mungu mbariki raisi Mwinyi,
Mungu mbariki DPP,
MUNGU MSHUGHULIKIE JIWE.

Mungu ibariki Tanzania
Kwa kunbukumbu zangu sidhani kama jiwe ndiye aliyewaweka ndani!!! Hawakuwekwa ndani kipindi cha J. K kweli? Nakumbuka yale machafuko ni ya muda mrefu kidogo!!!
 
Mhubiri dini ya Mtume wenu sasa! na siyo kuhamasisha vitendo vya uvunjifu wa amani kwa kisingizio cha kutaka kuvunjwa kwa Muungano!

Wamekuwa gerezani kwa miaka 9 shutuma za ugaidi zimeshindwa kuthibitishwa
 
Wavunje hata kesho! Sina cha kupoteza. Ila sitawaunga mkono kamwe hao Masheikh kuhubiri chuki na mwisho wa siku baadhi ya Watanzania wenzetu kumwagiwa tindikali, kwa kisingizio cha kutaka kujitenga na Tanganyika!

Wamekuwa gerezani kwa miaka 9 shutuma za ugaidi zimeshindwa kuthibitishwa wewe kwa nini hukupeleka ushahidi Mahakamani?
 
Hawa magaidi wameachiwa kwa sababu ya dini yao .... Lazima kosa hili liwagharimu watu na serikali..yaani mkawaalika na wamarekani kuwasaidia leo hii mnasema hawana hatia ...
Hawa ni magaidi na magaidi huwa wanawekwa kizuizini milele

Wamekuwa gerezani kwa miaka 9 shutuma za ugaidi zimeshindwa kuthibitishwa.Peleka Ushahidi wako Mahakamani sio hapo
 
Babu seya alikamatwa wakati wa Mkapa?
 
Waambie warudie upuuzi wao waone

Utafanya nini wewe! Wako kwenye himaya yao hukoo, sehemu ambayo 98% ya waislamu.. na wanapotaka muungano uvunjwe wewe mmatumbi wa tandale huko inawauma nini!! Mnawapa nini haswaa cha maana kutoka bara. Acha waendelee kudai haki yao.


Imewachoma sana kuachiwa huru, mlitaka waendelee kuteswa sio! Mungu amepokea dua za waja wake na amejibu alhamdulilah. Wewe endelea na chuki zako mwanaume mzima huoni hata aibu, huenda hata dada zako/mke wako anakushangaa ulivyo. Badilika mzee, acha chuki za kijinga, fanya kazi, lisha el familia.
 
Waambie waongee tena ujinga waone nini kitawapata, and kumbuka mara ya kwanza walibebwa mzobe mzobe kutoka huko huko kwenye hiyo 98%. Wapande majukwaani tena waongee shit, washukuru Mother ana huruma, jiwe angelala nao mbele
 
Kwa kunbukumbu zangu sidhani kama jiwe ndiye aliyewaweka ndani!!! Hawakuwekwa ndani kipindi cha J. K kweli? Nakumbuka yale machafuko ni ya muda mrefu kidogo!!!

Pamoja na yote, why magu awatoe kina babu seya ambao wanadaiwa wamewalawiti watoto na kuwaacha masheikh!! Na ndio kesi bab kubwa iyo ukilinganisha na masheikh ambao kesi yao haina ukweli wowote, miaka 9 haisikilizwi na Rais kalikalia kimyaa, kama sio uonevu ni nini!!! Kikwete mpaka amestaafu, magu nae ndani ya 5yrs kimyaaaa.


Mungu ampe afya njema mama yetu SSH
Mungu ampe afya njema Hussein Mwinyi
Na wengine wote wariofanya haki hiyo Mungu awape afya njema.
 
Vp ikiwa Mama kawatoa hao masheikh kwa sababu ni wazanzibari wenzake kwa maana hiyo ndio sababu ya kwanza halafu zengine zinafuata?
 
Bi Mkubwa, mimi sina tatizo kwa mtu/watu kudai haki yake/zao. Hata mimi ni mpenda haki. Mimi ninapinga matumizi ya kutumia mahubiri ya dini kuhamasisha uvunjifu wa amani, mauaji, kumwagia watu wasio na hatia tindikali! nk.

Kama tatizo ni Muungano, si mjitenge tu? Kuna sababu gani ya kuwwmwagia Mapadre wetu tindikali! Au kuchoma nyumba za ibada? Kwa nini hamtuigi sisi Wakristu? Siku zote tunaishi kindugu!

By the way, mimi ni Mkristo, ninayesali kwenye Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume.
 
Acha roho mbaya.
 
Mhubiri dini ya Mtume wenu sasa! na siyo kuhamasisha vitendo vya uvunjifu wa amani kwa kisingizio cha kutaka kuvunjwa kwa Muungano!
unaushahidi wewe na jamaa zako ? hilo kuhamasisha mnalifahamu nyinyi tu mnaoleta dada zenu mbele ya mikutano wakikata viuno ndio mnaojenga muungano.
 
Acha roho mbaya.
Sina roho mbaya! Ila ni vyema mkaendelea kuishi kindugu na Watanganyika wenzetu waliopo huko Zanzibar kama tunavyoishi na nyinyi huku Bara.

Nimefarijika kuona hao Masheikh kwa sasa wanaongelea zaidi amani kuliko jambo lingine lolote lile!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…