Sheikh Ponda: Kabla ya kuomba mvua, tuondoe Dhuluma

Sheikh Ponda: Kabla ya kuomba mvua, tuondoe Dhuluma

WALIOKO NDANI NIKUTOKANA NA MABAYA YAO HIVI UNASEMA MBOWE ATOKE NJE WAKATI KUNA WATU KAUA KINA WANGWE KINA SAANANE KWAAJILI TYU YA UCHU WA KUWA MWENYEKITI HALAFU UNAKUJA KUHARISHA HAPA KUWA WAACHIWE WATU MAGEREZANI SI UJINGA HUO KAA KIMYA KAMA HUWEZI KUONGEA YA MAANA

Zingatia matumizi ya herufi stahiki panapo paswa. Kwa mwendo huu hayupo wa kusoma ulichoandika ..
 
Sheikh Ponda ni Mtanzania wa kwanza kuwahi kutokea kukwepa SMG na Risasi zake.

Shekhe Ponda na Tundu Lissu walikuwa wafe kwa maagizo kutokea juu

Kafa yeye alhamdulilaa.
 
Huyu Sheikh ponda huwa ana misimamo yake isiyo yumbishwa kwa upepo wa misimu... Sijajua tatizo au ugumu unakuwa wapi kwa viongozi wengine wa dini kuwa kama huyu mzee.!!!
 
Nilipokuwa mdogo sekondari skuli niliamini na kuaminishwa kuwa sheikh Ponda ni mtu mbaya.. asiyefaa katika jamii, muuaji, gaid n.k

Nashukuru nimekuwa mtu sasa naamini kinyume chake.
Naomba Mungu anisamehe kwa fikra zile utotoni.

Hii ndiyo tofauti ya utoto na utu-uzima. Kuna watu wanaongezeka miaka tu na mvi mengine yote zikiwemo akili zinazidi kupungua kila sk.
 
Huyo sheikh namkubal kinoma kwanza hana unafiki kama wale wengine wa makada wa chama cha kijani..
 
Sheikh Ponda, mwanazuoni maarufu nchini asiyeupa nafasi unafiki amefunguka bayana:

View attachment 2021205

Kwenu viongozi wengine wa madhehebu zingine:

"Ninyi dhuluma hizi kwa wengine haziwafikirishi kabisa?"
Shekhe Ponda, Mungu akubariki. Nina hakika unaliishi neno la Mungu.

Kifalsafa, uislam wa kweli, hauna tofauti na ukristi wa kweli.

"Mathayo 5:23-24

“Basi, ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na ndugu yako, ndipo urudi utoe sadaka yako.

Mungu wetu, walioenda kuomba mvua, huku wakiwa wamewarundika watu wasio na hatia kwenye mahabusu, huku wakijitwalia madaraka bila ya matakwa ya watu, huku wakitawanya pesa za watu kwa manunuzi ya anasa, maskini wakiendelea kuteseka kwa kukosa huduma iwapasayao, basi ibada hiyo ya kuomba mvua, twaomba ukiibatilishe ikawe laana juu ya vichwa vyao, na wana wao, na wana wa wana wao. Bwana ukiendelee kuwasimamia, kuwatetea na kuwalinda wale wote wanaoonewa.
 
Basi kipindi cha jiwe haki ilitamalaki sana!

Maana hatukuona ukame kama huu
 
Back
Top Bottom