Shemeji yangu amekataa! Abadani, Mwanangu hapimwi DNA ikibidi ndoa ivunjike tu

Shemeji yangu amekataa! Abadani, Mwanangu hapimwi DNA ikibidi ndoa ivunjike tu

Mkuu uhangaike na mtoto si wako? Biblia inakataa kubebe geneology isiyoyako.

Ndio maana wazee wanajiua mwishoni baada ya kujua mtoto aliye mhangaikia hakuwa wake na Mama alificha.

Ukumbuke Kiroho iko hivi. Mtoto kama si wako ukamlea kwa kudanganywa ni wako. Hata kama unampenda kivipi siku atakayogundua Baba yake wa Damu sio wewe na ni mwingine atakushangaza na wala usilaum ni Nature.
Kwani wewe huwezi kulea mtoto asiye wako?
 
FB_IMG_16646613623086734.jpg

Kuna haja ya kutembelea maeneo ya kazi na anapopenda kushinda mkeo kuona watoto wanafanana na Nani ?
 
Asee mbna kaz ipo.
Aje huku ndungu Kuna Mtaalam wa DNA za kienyeji, hapo haihitajiki hata mtoto kuwepo.

Na usikute mtoto wa mtoa mada rafiki. Ko kaka yako ajiandae na Majibu yotee🤣😲
Na huku Kwa Fundi wetu utaambiwa Hadi baba halisi wa mtoto.
Nyie waganga wachonganishi tu hamna lolote. Mtaanza kunisingizia na mimi. Mimi mwenyewe mweusi nazaa vipi mweupe?
 

Wanahume atuja andaliwa kubeba fedheha siku zote akilini mwetu kuna kitu kimekaa na kinatuambia ni lazima tushinde kila kitu

Angalia mwanaume anapo mtongoz mwanamke akimkataa unaona nguvu anayo tumia ni kubwa ili akubaliwe hatuna uwezo wa kukubali ukweli

Kitu kinapelekea watu kujinyonga mwanaume akichapiwa anaumia sana kuliko mwanamke akiibiwa mwanaume na shoga yake
 
Wakuu tumefika mwisho. Tumekuwa watabe kushauri kwenye mahusiano ya wengine huku mtandaoni lakini huku field Mke wa Brother(rafiki yangu wa longtime) ametushinda.

Ni hivi Mwaka Jana Mke wa Huyu Best Yangu alijifungua mtoto wa kiume. Tulifurahi kupata mtoto wapili na sisi kama ndugu na jamaa wa karibu sana ukizingatia yeye jamaa alinisaidi sana kusoma enzi hizo kipesa na kimawazo basi tulimfanyia Tafrija ndogo ya kupata mtoto.

Siku chache baadae furaha ya jamaa iliingia shubiri kila alipokuwa akifatilia ukuaji wa mtoto.

Yaani mtoto amekuwa na sura na mwonekano tofauti na Baba na Mama yake.

Yaani Mshikaji ni Mweusi na Mke wake maji ya kunde lakini Mtoto ni Mweupe.

Kwa sayansi ndogo tuliyo nayo kama baba mweusi na Mama maji ya kunde sio rahisi kupata mtoto mweupe. Pengine angepata rangi ya kunde kama Mama yake au Mweusi kabisa kama Baba yake.

lakini Baba ni msomi hawezi kufanya maamuzu based on just feelings. Ameamua kushauriana na mkewe kuwa wakampime DNSA maana jamaa roho inakataa kumpenda mwanaye kati kati ya mashaka.

Mke amekataa kata kata kuwa Mwanaye hapimwi DNA ikibidi hata ndoa ivunjike.

Ana dai kama hamwamini mke wake basi bora waaachane.

Mimi na Braza tume baki mdomo wazi juu ya msimamo wa Mwanamama huyu.

Tulitegemea angekubali ili kumwondolea hofu mumewe na upendo uzidi kutamalaki. Hali imekuwa tofauti.
Hapo kapigwa changalamoto machoni.
One man down,mpe pole sana brother.

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Na inaleta dharau miaka yoote utakayoishi na mke aliyezaa nje ndani ya nyumba yako anakuona boya tu.
Isaya 58:7
[7]Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?
Is it not to deal thy bread to the hungry, and that thou bring the poor that are cast out to thy house? when thou seest the naked, that thou cover him; and that thou hide not thyself from thine own flesh?

Biblia Iko wazi, hupaswi kuiacha damu yako, ni dhambi kubwa kulea mtoto asiye wako anayetokana na uzinzi.
 
Back
Top Bottom