Sherehe ya Mwaka Mpya ni ya Kikristo, Waislamu tumeivamia tu bila kujua

Nabii Issa Ni nani...?nipe mawili matatu kumhusu.
 
Unavuka kwenda wapi na kalendar haikuhusu,hizi kalendar ni vitu vya kubuni,wachina wana calendar yao inaanza mwezi wa pili,waarabu wanayao ila zimeouuzwa na ulimwengu
Na wewe katengeneze kalenda yako
 
Tukubali tu dunia inatawaliwa na mfumo kristo,kila mtu hata sheikh ukimuuliza tupo karne ya ngapi atakupa jibu kulingana na kalenda ya Papa Gregory

Mtume wetu mtukufu Muhammad (saw) alipata kusema; "Jambo lolote jema ni hazina iliyopotea ya Muisilamu basi tuionapo tuichukue".

Hapo jambo jema maana yake ni jambo lenye manufaa kwa Muisilamu mwenyewe na kwa watu wengine hivyo kwakuwa Gregorian Calendar inayo manufaa kwa Waisilamu na dunia nzima basi hiyo ni hazina Muisilamu iliyopotea na hakuna kosa kuitumia.
 
Kwanza mtoa mada ni mpumbavu Sana,,,,unajua Kwa nini?

Kwasababu

Umeandika post kana kwamba wewe ni muislamu, kwani ungeandika kama Mgalatia lingekuwa na tatizo gani?

Pili ifahamike kwamba Uislamu sio kwamba hautambui hii kalenda ya kizungu laa hasha inaitambua kwasababu masuala mbali mbali ya kijamii yanaenda kwa kufuata kalenda hiyo.

Ila

Haifai kwetu Sisi kushangilia mwaka mpya huo ingawa tunautambua kuwa upo,naona hapa tumeelewana.

Mwaka mpya WA kiislamu upo na Una miezi Yake mitukufu katika ibada zetu mbali mbali ambayo maarufu miongoni mwenu ni mwezi wa Radhamani huu mnaujua Sana.

Kwahiyo ifahamike kuwa tunautambua mwaka mpya WA kizungu lakini hatupaswi kuushangilia.

Kwanza katika akili ya kawaida Tu,angetakiwa mtu atafakari juu ya miaka yake hapa duniani inapungua kadri mwaka mpya unapo ingia,je amefanya mema mangapi? Ametanguliza nini mbele ya Allah ikiwa Leo au kesho anakufa?

Huo ni mfano tu nimeutoa.

Next time mtoa mada usiridie upumbavu WA kujifanya muislamu kumbe Mgalatia!
 
Calenda ya kiislamu ina siku ngapi katika mwaka? Miaka aliyoishi mtume duniani 63 ilihesabiwa kwa kalenda ya kiislamu ama gregorian?
 
We ndio moumbavu,hivi unajua waislamu wengi wanaushangilia huu mwaka wa kizungu,kuutambua haina shida .shida ni kuushangilia,wanaoushangilia akiwemo rais mstaafu mmoja muislam safi wanaelewa maana yake au ni kujitoa akili.soma uelewe
 
Kuutumia sawa kuushangilia je???
 
Kuutumia sawa kuushangilia je???

Jiulize; Unapoushangilia unapata manufaa gani??!!--- Mtukufu Mtume Muhammad (saw) kazungumzia juu ya manufaa ya kitu ndio maana akaita "hazina ya muumini iliyopotea", hazina ni kitu chenye manufaa.
 
Vizuri
 
Jiulize; Unapoushangilia unapata manufaa gani??!!--- Mtukufu Mtume Muhammad (saw) kazungumzia juu ya manufaa ya kitu ndio maana akaita "hazina ya muumini iliyopotea", hazina ni kitu chenye manufaa.
Wakristo wanashangilia kwa sababu ina uhusiano na dini yao,ilianzishwa na Papa Gregory na ina uhusiano na umri wa Yesu,
Cha ajabu inashangiliwa na kila mtu,mktisto,muislam na mpagani
 
Wakristo wanashangilia kwa sababu ina uhusiano na dini yao,ilianzishwa na Papa Gregory na ina uhusiano na umri wa Yesu,
Cha ajabu inashangiliwa na kila mtu,mktisto,muislam na mpagani

Ni hivi; wewe kama unaona kuna faida kuishangilia basi shangilia ili ufaidike, jambo la msingi hapo ni kupata faida ya kushangilia.

Mfano mimi inapoingia mwaka mpya huku watu wakipiga honi, kelele, fataki nk, mimi hushika udhu na kuswali rakaa 2 za sunna/nafal kumshukuru Allah kwa kuuona mwaka mpya isitoshe pia kutoa shukurani kwa manufaa niliyopata katika mwaka uliopita.
 
We ndio moumbavu,hivi unajua waislamu wengi wanaushangilia huu mwaka wa kizungu,kuutambua haina shida .shida ni kuushangilia,wanaoushangilia akiwemo rais mstaafu mmoja muislam safi wanaelewa maana yake au ni kujitoa akili.soma uelewe
Kwanini umeandika huku unajifanya muislamu kama sio upumbavu ni nini?
 
Kiuhalisia hakuna mwafrika anayehusika na dini yoyote kati ya hizi mbili, wahusika wenyewe ni watu weupe (wazungu na waarabu)
Kama wewe ni mweusi na una midomo mipana na unajiita Muislamu au Mkristo basi tambua hauna akili sababu wewe ni follower tu wa hizo dini na sio mlengwa wala muhusika.

Sema Waafrika weusi wote wanafuata Calendar ya Mzungu, huu ndio uhalisia.
 
Kwanini umeandika huku unajifanya muislamu kama sio upumbavu ni nini?
Kwani nikijifanyq muislam au nikiwa muislam au mpagani shida nini??angalia content uache kushabikia sherehe zisizokuhusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…