Sherehe ya Mwaka Mpya ni ya Kikristo, Waislamu tumeivamia tu bila kujua

Sherehe ya Mwaka Mpya ni ya Kikristo, Waislamu tumeivamia tu bila kujua

Ukigoma kuyaoga,utakunywa tu. Ukigoma kuyanywa utafulia tu. Ukigoma kuyafulia utakula samaki wake tu. Ukigoma kula samaki utayavuka tu kutoka mahala moja kwenda kwingine lazima uvuke iwe daraja au kwa ndege. Ukigoma wewe mama ndugu,rafiki atakupikia chakula ule tu
Kalenda ya Gregory inahusiana nini na ukiristo!?..ni Kama wewe uanzishe kalenda ukipimia mwaka wa elnino au mwaka wa Vita vya kagera
 
Soma maelezo niliyo kupa yako wazi sana. Kwenu nyinyi kusherehekea mwaka mpya ni ibada au siyo ibada ? Kama ni ibada wapi ibada hii mmeipata ? Je Yesu alisherehekea kupinduka kwa mwaka ?

Kusherehekea ni dhambi sababu hakuna waio tutangulia wailifanya jambo hili si mitume wala si manabii. Mola wetu ameweka usiku na mchana ili watu wapate kuhesabu na kujua hesabu na idadi ya miaka na si kusherehekea.

Kwahiyo suala la sisi Waislamu kutumia mwaka usio wa Kiislamu upo nje ya uwezo wetu sababu tumekuta tayari jambo hilo lipo ila kwa nchi ambazo zinajitawala zenyewe yaani za Kiislamu unazingatiwa mwaka wa kiislamu. Kwahiyo hili linaingia katika mlango huo wala haliathiri dini maadamu tunajua mwaka wetu wa Kiislamu ukoje, siku inadalika saa ngapi haidhuru.
UMESEMA:
Kusherehekea ni dhambi sababu hakuna waio tutangulia wailifanya jambo hili si mitume wala si manabii.

SWALI:
Hao Waliowatangulia mitume na manabii ,Walitumia Kalenda ya Kanisa kama ninyi mnavyotumia kalenda ya kanisa?
 
Namshukuru Allah kwa mafanikio aliyonipa mwaka uliopita na sio namshuru Allah kwa kubadilika mwaka.-- soma vizuri pont yangu. Hata pia huwa namshukuru kwa mafanikio mwaka mpya wa kiisilamu unapoingia.
Unamshukuru Alah kwa Mwaka uliopita upi?

Huu wa Kanisa ulioanzishwa na Wakristo chini ya Papa Gregory au upi?
 
Tunalitumia sababu lipo nje ya uwezo wetu kutokana na mfumo wa nchi jinsi ilivyo. Unaelekea ninacho kiongelea ?

Ndiyo maana katika kuliacha tunafanya yale ambayo yapo ndani ya uwezo na Hilo linaingia katika mlango wa dharura, na dharura hukadiriwa kwa makadirio yake.
Lipo nje ya uwezo wenu kivipi?

Alah ameshindwa kuwasaidia kujinasua kutoka kwenye huo mtego wa kalenda ya kanisa?
 
Kalenda ni Kama elimu,Haina dini,haijalishi nani kagundua,hata Gregory hakusukumwa na ukiristo kutengeneza hiyo kalenda, Qur'an 17:12,10:6,29:14,2:260 inatambua kwamba tunatumia jua na mwezi kupima nyakati
Acha uongo.
Gregory ambaye alikuwa papa wa kanisa katoliki alisukumwa na Ukristo ndio maana alianza kuhesabia mwaka kuanzia kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

Huu ni mwaka 2023 AC (After Christ)
 
Uislamu umekamilika sana, unauliza maswali mepesi sana. Huko kwenye madaladala ni katika mlango wa dharura na mlango katika dini upo.

Lakini suala la kiibada si jambo la dharura, Yesu alifanya vipi ibada au mafundisho ya kufanya ibada zenu mmeyapata wapi ?

Lakini nashangaa wewe huoni ubaya wa kuchanganyika jinsia mbili tofauti akili zako ndogo sana kijana au hufikirii. Jamii imeharibika na kuwa hivi katika sababu kubwa ni kuruhusu michanganyiko hiyo.
Daladala ni dharura?
Nyie jamaa ni comedy sana.

Migahawani huwa mnakaa jinsia tofauti?
Sokoni mnakaa jinsia tofauti?
Vyuoni/shuleni huwa mnakaa jinsia tofauti?
Kwenye ndege huwa mnakaa jinsia tofauti?
Wanaoenda Zanzibar huwa wanakaa jinsia tofauti?
Uwanja wa taifa huwa mnakaa jinsia tofauti?



Hebu punguza ujuaji kidogo.
 
Hii kalenda tunayotumia,Gregorian Calendar ilikuja baada ya Julian Calendar, zote zina uhusiano na Issa ndio maana utakuta maneno kama AD au BC yote yanamrefer Nabii Issa.

Sasa sisi Waislam imekuwaje hatulijui hili au kufuata mkumbo? au ndio dunia inaongozwa na mfumo Kristo?
Kalenda nayo ni kitu cha kupiga vita????

Watoto wako shule zikifunguliwa utawaambia waandike 2023 au efu moja mia nne na kitu???
 
Hii kalenda tunayotumia,Gregorian Calendar ilikuja baada ya Julian Calendar, zote zina uhusiano na Issa ndio maana utakuta maneno kama AD au BC yote yanamrefer Nabii Issa.

Sasa sisi Waislam imekuwaje hatulijui hili au kufuata mkumbo? au ndio dunia inaongozwa na mfumo Kristo?
Mwaka mpya ni sherehe ya KIPUMBAVU kama zilivyo nyingine za kipumbavu
 
Back
Top Bottom