Tujivunie zaidi uhuru wetu? Sawa, lakini tuambizane ukweli pia. Hakuna mtu anayeupigania uhuru huu. Tukiongelea uhuru wetu, tunaongele TANZANIA. Kwa hali ilivyo sasa, tuna watu wanaopigania zaidi maslahi ya vyama vyao kuliko wanavyoipigania TANZANIA. Wamekuwa wakiitumia Tanzania kama "Scapegoat" ili kufanikisha adhima hiyo. Utawasikia wakisema wanawapigania wanyonge, lakini kiukweli wanakipigania chama chao. Wanyonge wanaosema wanawapigania kila siku, wamebaki katika hali almost zile zile kwa miaka yote 56. Tunapoadhimisha miaka 56, ni lazima tutafakari upya kuhusu Tanzania. Ni nani hasa yuko tayari kukipoteza chama chake siasa kwa ajili ya Tanzania???