Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

kapolo

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2012
Posts
303
Reaction score
103
Duuuuuuuh
SHERIA 13 ZA BOLI WAKATI TUKIWA WATOTO.
1. dogo mnene lazima awe Golikipa
2. Mwenye mpira ataamua nani acheze na nani asicheze.
3. Penati itatokea tu pale mchezaji akiumia sana na kutoka damu.
4. Mechi itaisha kama kila mchezaji atakua amechoka.
5. Hakuna free kick, kitu kama icho hakipo kwenye mechi zetu.
6. Hakuna Refa, mchezaji anaweza kuzunguka na mpira ata nyuma ya goli.
7. Kama haushiriki kwenye kutengeneza mpira unaweza usipate namba uwanjani.
8. Ukichaguliwa mwishoni ujue uwezo wako ni mdogo kuliko watu wote uwanjani.
9. Wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufata mpira ukitoka, au kutungua mpira endapo utanasa kwenye mti uku wakisubiria mchezaji aitwe kwao na wao wapate nafasi.
10. Mwenye mpira akikasirika, mechi ndo itakua imefika mwisho.
11. Inaruhusiwa kubadili golikipa kama penati ikitokea na baada ya penati golikipa anaweza kuendelea yule wa mwanzo.
12. yule mtaalam wa soka huwa hakosi namba ata siku moja.
13. Mwenye mpira huwa hatolewi ata akicheza vibaya.
14.Timu moja lazima wawe vifua wazi.
 
15. Unaruhusiwa kucheza na viatu vyovyote, hata kiatu kimoja ruksa.
16. Hamna idadi kamili ya wachezaji, ukichelewa unachotakiwa kufanya ni kutafuta mtu na kujigawanya mmoja kila timu.
17. Hakuna muda maalumu, mpira unachezwa hata masaa manne mpaka mtosheke
 
Mmenikumbusha mbali sana. Nimebaki kucheka hasa hapo kwa kubadili golikipa wakati wa penalti kisha golikipa wa awali anaendelea. Kucheza hadi mchoke,hata masaa 8. Kweli utotoni kulikua na burudani.
 
Duuuuuuuh
SHERIA 13 ZA BOLI
WAKATI TUKIWA WATOTO.
1. dogo mnene lazima awe
Golikipa
2. Mwenye mpira ataamua nani
acheze na nani asicheze.
3. Penati itatokea tu pale
mchezaji akiumia sana na kutoka
damu.
4. Mechi itaisha kama kila
mchezaji atakua amechoka.
5. Hakuna free kick, kitu kama icho
hakipo kwenye mechi zetu.
6. Hakuna Refa, mchezaji anaweza
kuzunguka na mpira ata nyuma ya
goli.
7. Kama haushiriki kwenye
kutengeneza mpira unaweza
usipate namba uwanjani.
8. Ukichaguliwa mwishoni ujue
uwezo wako ni mdogo kuliko watu
wote uwanjani.
9. Wale ambao wamekosa namba
kazi yao ni kufata mpira ukitoka,
au kutungua mpira endapo
utanasa kwenye mti uku
wakisubiria mchezaji aitwe kwao
na wao wapate nafasi.
10. Mwenye mpira akikasirika,
mechi ndo itakua imefika mwisho.
11. Inaruhusiwa kubadili golikipa
kama penati ikitokea na baada ya
penati golikipa anaweza
kuendelea yule wa mwanzo.
12. yule mtaalam wa soka huwa
hakosi namba ata siku moja.
13. Mwenye mpira huwa hatolewi
ata akicheza vibaya.
14.Timu moja lazima wawe vifua wazi.


Sasa mbona namba 7 na 13 zinapingana?!
7 asiyeshiriki kutengeneza Mpira hatocheza!
13:mwenye Mpira huwa hatolewi ata akicheza vibaya!
SWALI vipi kuwe na mwenye Mpira na wewe umeshasema Mpira umetengenezwa na wote?! Tena asiyeshiriki kutengeneza hachezi,sasa mwenye Mpira ni nani tena hapo?!
 
Sheria zetu 13 za mpira za utotoni.....
1.Mwenye mpira lazima acheze hata kama
hajui mpira...
2. Dogo mnene lazma awe
golikipa...
3.Mwenye mpira ataamua nan
acheze na nan asicheze..
4.Penat itatokea
pale 2 mchezaj ataumia sana na kutoka
dam...
5.Mechi itaisha kama kila mchezaj
atakuwa amechoka hoi...
6. Akuna free kick
wala kona katika mechi.
7.Hakuna lefa,
mchezaj anaweza kuzunguka na mpira hata
nyuma ya goli..
8.Kama haujashiliki
kutengeneza mpira unaweza usipate namba
uwanjani...
9.Ukichaguliwa mwishoni ujue
uwezo wako ni mdogo kuliko wote...
10.Wale
ambao wamekosa namba kazi yao ni kufata
mpira ukitoka,au kutungua mpira endapo
utakwama kwenye mti au kusubiri mchezaji
aitwe kwao....
11.Mwenye mpira akikasilika
mechi imeisha...
12.Inaruhusiwa kubadili
golikipa, kama penat ikitokea baada ya
apo,ataendelea kudaka yule yule..
13.Yule
mtaalam wa soka huwa hakosi namba ata
siku moja..

Tukumbushane nyingine.....
 
Hii kali hii,

Nimeipenda hiyo ya kubadili kipa wakati wa penati
 
14:Hakuna ruhusa kucheza na viatu(enzi hizo raba za DH).Kila mtu lazima acheze peku
 
Ahahahaha hizi mbili ni kweli ..nimekumbuka mbali sana

11.Mwenye mpira akikasirika
mechi imeisha...

12.Inaruhusiwa kubadili
golikipa, kama penalt ikitokea, baada ya
apo ataendelea kudaka yule yule..
 
11. Ukipigia vidole wanasema unapiga doso au dochi kwa hiyo toka nje.
12. Akiitwa mchezaji wa kuaminika nyumbani kwao anamweka mtu kucheza badala yake, hii iliitwa kushikia namba, ila mwenyewe akirudi unatoka.
13. Kulikua na kipindi cha gombania goli huku mkisubiri wachezaji wawe wengi ndipo mjigawe ktk timu mbili
 
Ukiwa Umegombana na mwenye mpira bas utakaa benchi mpaka ukome hata kama star vipi

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Pia,magoli ya utata daily!wengine wanahesabia goli wengine wanapings afu refa hakuna

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Hakuna kuchezea viatu (mpira wa makaratasi ; )
 
Back
Top Bottom