Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

Magoli yalikua ya mawe so sometimes nikiwa beki nikiona hali tete na wanakuja washambuliaji wa timu pinzani,naenda nabeba yale mawe yote mawili yanayokaa kama alama ya goli....,kinachofuata hapo ni mkono tu utatembezwa.
 
18.Jezi ni kwamba upande mmoja wamevaa mwingine wamevua(mashati)
19. uwanja ni popote na kwa vipimo vyovyote (tushawahi kucheza mechi golikpa na golikipa hawonani-uwanja umekata kona
Ebna we ni nouma.Hiyo 19 ni babkubwa!Umenikumbuxha mbaal xna yan
 
Mkienda kucheza mechi mtaa mwingine ndala au malapa lazima uivae mikononi cz kikiwaka nduki unasepa zako hakunaga time ya kutafuta ndala uliweka wapi
Daa,utaniua mkuu.Tunaandaa ni fimbo kabisa,tunazificha.Kikinuka tu,tunazama porini.
 
1. Hakuna idadi ya wachezi kwenye mechi moja yoyote aliyepo anapata namba hata kama hajui kucheza
2. Mchezaji harusiwi kucheza na viatu
3. Mwenye mpira ndo anapanga kikosi chake na hata kama hajui kiucheza namba uhakika
4. Magor huwa mara nyingi ni mawe na kama ni ya miti bas hakuna mlingoti wa juu gori linafungwa kulingana na urefu wa kipa
5. Mpira hauna refa na kama kuna refa uwasikiliza wababe wa timu wanasemaje
6. Mechi haina half time mchezaji hakichoka ruksa kutoka na kuingia tena
7. Mwenye mpira akiondoka na mechi huishia hapo. Hata kama ndo mechi inaanza
8. Gori la kwanza ndo linaamua nani wa kuvua nguo nakubaki na ngua
9. Penati ikitokea . Mchezaji yoyote anaweza kuwa gorikipa hata kama yuko nje

10.
11.

Unaweza kuongezea mambo kadha ambayo yanapatika kwenye mpira wa makaratasi enzi hizo na kama hujacheza mpira huu umemis mambo mengi

Karibu sana tukumbushane kibumbu ili lilo watoa wachezaji maarufu dunia kama ronaldo kante mane n.k
 
Siti ya mbere hapa..

Giza likiingia ndiyo mpira umeisha.

Dogo mnene anakuwaga golikipa.

Mwenye mpira ndiye huamua nani acheze.
 
1. Mkubwa Hachezi Na Akicheza basi Wanaingia Wawili.

2. Mwenye Mpira Hatolewi Hata Akicheza Vibaya.

3. Inaruhusiwa Kubadili Kipa Kama Penati Imetokea Na Baada Ya Penati Anaruhusiwa Kurudi Wa Mwanzo.

4. Yule Mtaalam Wa Soka Hakosi Namba Hata Siku Moja.

5. Dogo Mnene Lazima Awe Golikipa.

6. Mwenye Mpira Ataamua Nani Acheze na nani Asicheze.

7. Penati Itatokea Tu Pale Mchezaji Akiumia Sana Na Kutoka Damu.

8. Mechi Itaisha Kama Kila Mchezaji Atakuwa Amechoka.

9. Hakuna Free Kick, refa Wala Offside.

10. Ukichaguliwa Mwishoni Ujue Uwezo Wako Mdogo Kuliko Wote Uwanjani.

11. Mtaalam Wa Timu Akipewa Kazi Kwao Na Wazazi Wake Lazima Mumsaidie Ndio Mwende Kucheza.

12. Ukiumia Kidonda Kinawekwa Mchanga.

13. Kipa Anaruhusiwa Kudaka Popote.

14. Wale Ambao Wamekosa Namba Kazi Yao Ni Kufuata Mipira Ikitoka.

15. Mwenye Mpira Akikasirika Mechi Ndo Inakuwa Imeisha.

16. Hakuna Jezi, Timu mmoja Itavua Mashati Na Nyingine Itabaki Imevaa.

17. Wote Lazima Mcheze (Peku) Bila Viatu.

#Utoto wa zamani raha, siku hizi watoto wanacheza mpira kwenye simu, dunia imeisha.
 
Sisi senior citizens tulitumia manailon ya kufuma
Yes , wewe ni wa kipindi Mkapa anauza nyumba za serikali kwa bei chee, masaki na Oysterbay, nyumba nyingi waliuziana milioni 4, bei ya pikipiki.
 
Back
Top Bottom