Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Daah wengine hatujapitia izi mambo kabisa.Sheria 15 za mpira za kipindi cha utotoni;
1. Mkubwa hachezi na akicheza mnaingia wawili.
2.Mwenye mpira hatolewi hata akicheza vibaya.
3.Inaruhusiwa kubadili kipa kama penati imetokea na baada ya penati. anaruhusiwa kurudi wa mwanzo.
4.Yule mtaalam wa soka hakosi namba hata siku moja.
5. Dogo mnene lazima awe golikipa.
6.Mwenye mpira ataamua nani asicheze.
7.Penati itatokea tu pale mchezaji akiumia sana na kutoka damu.
8.Mechi itaisha kama kila mchezaji atakuwa amechoka.
9. Hakuna free kick, refa wala offside.
10. Ukichaguliwa mwishoni ujue uwezo wako mdogo kuliko wote uwanjani.
11.Mtaalam wa timu akipewa kazi na wazazi wake lazima mumsaidie ndo mwende kucheza.
12.Ukiumia kidonda kinawekwa mchanga.
13.Kipa anaruhusiwa kudaka popote.
14. Wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufata mipira ikitoka.
15. Mwenye mpira akikasirika mechi ndo inakuwa imeisha.
Daaah wasasa mnajua mambo ya panyaroad tu [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Daah wengine hatujapitia izi mambo kabisa.