Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

Kuna wakati tukiita goose kupigiana pasi ana kwa ana, anayepiga mnazi alishangiliwa Sana, hakukuwa na Muda wa kuanza hakukuwa na sharia,
 
Na ukipigwa tobo wakati wa kusafa basi utasafa mara mbili
 
Nakumbuka wakati wa kuchagua team mnajipanga mstari mmoja mrefuu halafu yule mbabe ndio anasimamia zoezi la waliojipanga,mmoja anarudi nyuma na anayefuatia anapiga hatua mbele,ilikua mmoja anasogea mbele anayefuata anarudi nyuma mpaka zinapatikana team mbili,team ya waliorudi nyuma na waliopiga hatua mbele!!
 
Halafu eti ilikua tunajifunga bandeji mguuni hata kama hatujaumia! Tulijiaminisha kua kujifunga bandeji eti ndio unakua mchezaji wa maana!! Old gold days.
 
Na play stations pia zimechangia kuharibu ladha ya soka la utotoni
Mkuu siku hizi hakuna hata zile ngumi za utotoni! Hata vijana wa siku hizi wanaishia kutukanana kwenye Instagram tu,hakuna tena ngumi za watoto kupigana mitaani kama zamani,kila mtu yuko bize na kubeti!!
 
Mkuu siku hizi hakuna hata zile ngumi za utotoni! Hata vijana wa siku hizi wanaishia kutukanana kwenye Instagram tu,hakuna tena ngumi za watoto kupigana mitaani kama zamani,kila mtu yuko bize na kubeti!!
Kweli kabisa mkuu..., hebu fikiria hata zile creativity za kutengeneza magari ya box au waya siku hizi hakuna kabisaaa.., michezo kama baba na mama au komborela kizazi cha sasa kinakosa vitu adimu. Kuuza sura tu na kuombana namba huko facebook na whatsapp hadi kero
 
Kuna hawa wa siku izi kila siku unakita wametandika kitambaa chini kila anayepita anaombwa pesa utasiki, Kaka mkubwa tuchangie wanao leo Tuna mechi bana, ukiwapa badae wanaenda kubet yaani ni kero sana watoto wa siku hizi hakuna kitu
 
Kweli kabisa yani kwa wasichana siku hizi hata rede,makida na mdako ni nadra sana kukuta wakicheza..utandawazi pia umetuathiri tunajenga nyumba ndani tiles nje vitofali vile chini hatubakizi ata kasehemu ka mchanga na udongo mtoto ata achimbe shimo la mdako na vishimo vya bao au achore kipande aruke aruke mtoto siku hizi akishika tu udongo mzazi anafoka minyoo akienda kucheza rede anaambiwa chokoraa...nitoe wito kwa wazazi watoto ni michezo ukiruka stage za mchezo utotoni matokeo yake ukikua sasa unaanza kuruka ruka kama mtoto
 
Tobo bao/Dobo dunda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…