Mpira wa utotoni raha sana.
Yaani mtu huchoki, hiyo hata kula huoni umuhimu wake.
Hasa siku ya Jumamosi, nakumbuka Muda wa kula ukifika nikisikia naitwa "HARUFU, we HARUFU Chakula tayari" hiyo lazima niende sehemu nikajifiche, Maana tulikuwa na Dada wa Kazi mmoja, Muda wa Chakula ukifika lazima aite kwa makelele kabla ya kufika eneo husika.
Nakumbuka mambo ya kubambikiana, kupiga madochi ukipiga kijiwe, au lami ujue mpaka vidole vinatoka vidonda.
Mara ngumi zinaanza mpirani, ukinitukana ujue lazima tuzichape. Kupigana mpirani ni jambo la kawaida sana.
Magoli madogo, Gombania Goli, Kuchonga Kona, N.K.
Jamani