1. Mkubwa Hachezi Na Akicheza basi Wanaingia Wawili.
2. Mwenye Mpira Hatolewi Hata Akicheza Vibaya.
3. Inaruhusiwa Kubadili Kipa Kama Penati Imetokea Na Baada Ya Penati Anaruhusiwa Kurudi Wa Mwanzo.
4. Yule Mtaalam Wa Soka Hakosi Namba Hata Siku Moja.
5. Dogo Mnene Lazima Awe Golikipa.
6. Mwenye Mpira Ataamua Nani Acheze na nani Asicheze.
7. Penati Itatokea Tu Pale Mchezaji Akiumia Sana Na Kutoka Damu.
8. Mechi Itaisha Kama Kila Mchezaji Atakuwa Amechoka.
9. Hakuna Free Kick, refa Wala Offside.
10. Ukichaguliwa Mwishoni Ujue Uwezo Wako Mdogo Kuliko Wote Uwanjani.
11. Mtaalam Wa Timu Akipewa Kazi Kwao Na Wazazi Wake Lazima Mumsaidie Ndio Mwende Kucheza.
12. Ukiumia Kidonda Kinawekwa Mchanga.
13. Kipa Anaruhusiwa Kudaka Popote.
14. Wale Ambao Wamekosa Namba Kazi Yao Ni Kufuata Mipira Ikitoka.
15. Mwenye Mpira Akikasirika Mechi Ndo Inakuwa Imeisha.
16. Hakuna Jezi, Timu mmoja Itavua Mashati Na Nyingine Itabaki Imevaa.
17. Wote Lazima Mcheze (Peku) Bila Viatu.
#Utoto wa zamani raha, siku hizi watoto wanacheza mpira kwenye simu, dunia imeisha.