Sheria mpya ya TISS tusijifanye vipofu wakati kumbe tunatawaliwa ama tunaenda kutawaliwa kijeshi

Sheria mpya ya TISS tusijifanye vipofu wakati kumbe tunatawaliwa ama tunaenda kutawaliwa kijeshi

Kuna haja ya kuangalia usalama wa taifa kama raia wenye nchi yao wanayoilinda na kuipenda badala ya jeshi au kikundi fulani Cha kulinda maslahi au usalama wa viongozi.
Usalama wa taifa ulenge maslahi mapana ya raia na taifa kwa ujumla dhidi ya hatari za kiusalama kutoka nje.
Haiwezekani na haikubaliki popote pale, usalama wa taifa uhusishwe na utekaji, kuua au wizi wa kura kwa sababu tu ya kulinda madaraka ya mtu mmoja au kikundi fulani.
Kinga ya kisheria dhidi ya jinai inaweza kuunganisha nukta kuelekea kwenye tuhuma hizo.
Kuna njia nyingi za kuepuka jinai kama wangetumia intelijensia, labda waliotengeneza muswada hawana hiyo.
 
Mwanzo walikuwa wanateka, wanatesa na wanaua kama wasiojulikana, kinachobadilika sasa ni kuyafanya hayo kwa mujibu wa sheria.
P
Mkuu labda leseni ya kuua itaongeza ufanisi kwenye utendaji kazi😁

James_Bond_Licence_Atari.jpg
 
Mkuu labda leseni ya kuua itaongeza ufanisi kwenye utendaji kazi😁

View attachment 2643493
I got a License to kill so I steer the Gat
Roc-A-Fella, Ruff Ryders, niqqas scared of that
Got a new motto this year, "Don't Fv<k With My Ones"
Knock on your door, three in the morning
"It's just us and the guns!"

Jigga oh My Nikka - 1999
 
Hao jamaa wa TISS wataanza kuua watu hasa wapinzani wa watawala na hawatochukuliwa hatua yoyote ile kwa sababu sasa wana Kinga.

Na wanaCCM watakuwa wajinga wakidhani kuwa hii itaenda kuwagusa wapinzani tu, atatokea mtawala kichaa ataanza kuwashughulikia kupitia watu wa usalama wa Taifa na hawatakuwa na yeyote wa kumhold accountable
 
Magu alikuwa Kweli Dictator uchwara,

Huyu anaandaliwa kuwa zaidi ya hapo!!!!
 
Hapa dawa ni kutafuta tu mtu mwenye majini yake makali ili iwe fundisho kwa kolokolo yeyote akizingua
 
Hao jamaa hata sheria isipobadilishwa haithiri chochote Ben amepotezwa na wao wao(Zitto alithibitisha baada ya kufanya upelelezi) hakuna aliyekamatwa wala kushitakiwa.

Zakaria aliwapiga risasi hao majamaa walivyotaka kumteka lakini hawakushitakiwa kwa UTEKAJI kwahiyo mimi sioni hata faida ya kwenda kuwalipa wabunge wakae kujadili amendments ni kupoteza muda na fedha za posho haisaidii kitu maana kwa sheria hii wanaua /wanateka/wanajeruhi lakini hawaguswi.
Tofauti kubwa sana iwapo sheria itawalinda kushtakiwa.
 
Tofauti kubwa sana iwapo sheria itawalinda kushtakiwa.

Kwani kwasasa haiwalindi? Mbona wamempoteza Ben watcheight? Mbona wamemtandika Lissu risasi? Kuna aliyeshitakiwa? Kwani hii sheria ndiyo itawaruhusu kuua hadharani huku watu wakiwaona na kutembea bila wasiwasi kama wafanyavyo polisi wakiwa field? Si wataendelea kufanya kwa kificho hicyo hivyo? Sasa mantiki ya kuwa na sheria ya kuwalinda ni nini? Kwani kuna aliyewahi kushitakiwa? Kama yupo unaweza kuweka hiyo case hapa?
 
View attachment 2643253

Nimeweka hii snapshot inayoonesha muswada wa mabadiliko ya sheria ya chombo chetu cha Intelejensia.
Kwenye mapendekezo hususan kifungu cha 19 wanasema hapo kuwa, jinai inaweza kufanywa na TISS personels wakiwa wanatekeleza majukumu yao kwa uaminifu....

Jambo linalonistua ni kwamba, wengi hudhani jeshi kutawala ni mpaka pale jeshi linapopindua serikali ya kiraia. Huu muswada umeleta tafsiri mpya ya utawala wa kijeshi. Tufuatilie kwa akili kubwa sana haya mambo yanavyopangiliwa kwa uangalifu kuelekea imla ya kijeshi...

Nipate elimu kutoka kwenu wanaJF

  1. Kuna ukamilifu gani kwenye jinai?
  2. Kuna uaminifu gani kwenye jinai
  3. Kipimo gani kinatumika kufahamu kuwa jinai fulani imefanyika during utekelezaji wa majukumu kwa uaminifu
  4. Aina gani ya jinai inayoombewa mabadiliko? Ya kutesa au kuua?
  5. TISS ni jeshi au kitengo cha uraia kinachofanya shughuli za kijeshi? Sheria za kimataifa zinasemaje kuhusu utendaji wa jeshi kwa raia?
  6. Huu muswada nani wameomba hayo marekebisho yaani ni TISS au Rais (taasisi/sponsor)?
Lengo na dhumuni la uzi huu siyo kubeza ama kuponda kazi kubwa wanayofanya TISS kwa nchi yetu, bali ninalengq kuangalia motive ya huu muswada ambao umekuja kana kwamba ni by the way lakini uzito wa sentensi zilizotumika kuuandaa ni wake up call kurecall matukio ya kijinai ambayo chombo chetu kitukufu kimehusishwa ama kunyooshewa vidole.

Kwa mahaba mema kwa nchi yangu, I submit

CC: Mzee Mwanakijiji Pascal Mayalla Retired raraa reree Extrovert Bujibuji Simba Nyamaume Mshana Jr zitto junior lumumbai Kiranga Erythrocyte mwanamwana MwanaWA Ebrania Gily Demi
Nina wasi wasi kufungwa kwa Sabaya kumewafanya wanaomuunga mkono Sabaya yasije kuwakuta tena.

Inaonekana wana nguvu.

Je wamejipanga kurudia yale yale?
 
Kwani kwasasa haiwalindi? Mbona wamempoteza Ben watcheight? Mbona wamemtandika Lissu risasi? Kuna aliyeshitakiwa? Kwani hii sheria ndiyo itawaruhusu kuua hadharani huku watu wakiwaona na kutembea bila wasiwasi kama wafanyavyo polisi wakiwa field? Si wataendelea kufanya kwa kificho hicyo hivyo? Sasa mantiki ya kuwa na sheria ya kuwalinda ni nini? Kwani kuna aliyewahi kushitakiwa? Kama yupo unaweza kuweka hiyo case hapa?
Exactly
 
Back
Top Bottom