Sheria mpya ya TISS tusijifanye vipofu wakati kumbe tunatawaliwa ama tunaenda kutawaliwa kijeshi

Sheria mpya ya TISS tusijifanye vipofu wakati kumbe tunatawaliwa ama tunaenda kutawaliwa kijeshi

Sasa watakuwaje juu ya sheria ? Wataua...kwa visasi ...watajificha utekekezaji ....na interest ya nchi ....hiyo haiwezekani ....Lazima uwajibikaji uwepo ili sheria iwe one guide kwenye utendaji m....itakuwa fujo sasa ...nani alieomba hayo mabadiliko ? Tiss kama taasisi kutokana research ....yao ugumu kutengeneza Majukumu au Rais kama taasisi ??
Kuna kikundi cha watu .... na sio TISS wala RAIS aliepo madarakani. Hatuna utaratibu wa kufata sheria hata kama zipo na zenye jufaa
 
Huu muswada uliandaliwa kipindi Cha mwendazake, sijui bi mkubwa kaupendea nn aisee... yaani tunaenda kuunda majambazi watakaokuwa wanafanya ujambazi kisheria... Wakikupora sawa tu, wakikuua sawa tu..wakikuteka sawa tu... yaani kiukweli cjui sasa kama polisi watakuwa na kz gn sasa... Mmmmhhhh hii nchi ngumu sana aisee
Tupe uthibitisho kuwa aliuandaa Mwendazake.

Upo uwezekano hata wizi unaoendelea serikalini mkasema ulianzia kwa Mwendazake
 
Bunge linalazimisha kutengeneza mazingira ya mapinduzi. Coup huwa inatafutwa kwa justification au greedy, sasa bunge la CCM linarundika sababu mara CAG anatoa ripoti wanafungia maandazi hawachukui hatua, mara sheria za kuzuia mashkta kwa watu fulani na mengine mengi.
Careless beings
Ndo unaona hata Wapinzani wamekaa.kimya kuhusu ripoti ya CAG kutokujadiliwa. Wao wameshikilia tujadili Lissu kwenda kufata gari lake Polisi! Au utasikia "mfateni chato"
 
View attachment 2643253

Nimeweka hii snapshot inayoonesha muswada wa mabadiliko ya sheria ya chombo chetu cha Intelejensia.
Kwenye mapendekezo hususan kifungu cha 19 wanasema hapo kuwa, jinai inaweza kufanywa na TISS personels wakiwa wanatekeleza majukumu yao kwa uaminifu....

Jambo linalonistua ni kwamba, wengi hudhani jeshi kutawala ni mpaka pale jeshi linapopindua serikali ya kiraia. Huu muswada umeleta tafsiri mpya ya utawala wa kijeshi. Tufuatilie kwa akili kubwa sana haya mambo yanavyopangiliwa kwa uangalifu kuelekea imla ya kijeshi...

Nipate elimu kutoka kwenu wanaJF

  1. Kuna ukamilifu gani kwenye jinai?
  2. Kuna uaminifu gani kwenye jinai
  3. Kipimo gani kinatumika kufahamu kuwa jinai fulani imefanyika during utekelezaji wa majukumu kwa uaminifu
  4. Aina gani ya jinai inayoombewa mabadiliko? Ya kutesa au kuua?
  5. TISS ni jeshi au kitengo cha uraia kinachofanya shughuli za kijeshi? Sheria za kimataifa zinasemaje kuhusu utendaji wa jeshi kwa raia?
  6. Huu muswada nani wameomba hayo marekebisho yaani ni TISS au Rais (taasisi/sponsor)?
Lengo na dhumuni la uzi huu siyo kubeza ama kuponda kazi kubwa wanayofanya TISS kwa nchi yetu, bali ninalengq kuangalia motive ya huu muswada ambao umekuja kana kwamba ni by the way lakini uzito wa sentensi zilizotumika kuuandaa ni wake up call kurecall matukio ya kijinai ambayo chombo chetu kitukufu kimehusishwa ama kunyooshewa vidole.

Kwa mahaba mema kwa nchi yangu, I submit

CC: Mzee Mwanakijiji Pascal Mayalla Retired raraa reree Extrovert Bujibuji Simba Nyamaume Mshana Jr zitto junior lumumbai Kiranga Erythrocyte mwanamwana MwanaWA Ebrania Gily Demi
Wakipitisha huo muswada pia waruhusu Kila raia amiliki silaaha ya kujilinda kama USA au SA
 
Ulishaona wanakamatwa kama wanavyokamata wanajeshi au polisi? Lini uliona mfanyakazi wa "teeth" amepelekwa mahakamani kwa kosa la kijinai ,sabaya "andakava igo sirii" alivyodakwa hata kama ni wa kwao lakini walimkana.
Nina watu watatu ninao wajua walimatwa na mahakamani walifikishwa mmoja nakueleza kwa ufupi
Alimatiwa moro na jopo la mapolis kwanza ulipigika mkono mmoja mzuri sana 1 kwa waratu polis

Mpaka wakamua kutumia pingu za kurusha

Jamaa aliingia katika dili la viwanja na akatumia vibaya jina kwa waarabu noro
 
Huu muswada uliandaliwa kipindi Cha mwendazake, sijui bi mkubwa kaupendea nn aisee... yaani tunaenda kuunda majambazi watakaokuwa wanafanya ujambazi kisheria... Wakikupora sawa tu, wakikuua sawa tu..wakikuteka sawa tu... yaani kiukweli cjui sasa kama polisi watakuwa na kz gn sasa... Mmmmhhhh hii nchi ngumu sana aisee
Uliliwa kiboga na mwendazake wewe sio bure
 
Kikawaida TISS wasingetakiwa kuwepo lakini hali halisi si kawaida. Kuna elqaeda walitikisa dunia kuna uamsho walitikisa zanzibar kuna raila na askofu mackenzie wanatikisa Kenya. Sheria zote haki zotezote taratibu zote zipo yeye hataki. Huna jinsi. Au mko vitani na mabeberu msaliti anatoa siri zenu. Huna jinsi. Kama si hivo walactusingehitaji TISS.

Kama wapo inakuwaje ufisadi mkubwa unatokea au nao ni sehemu ya wapigaji?
 
Op zote zinaenda kuwa rasmi sasa....

Siyo unaona mkonga kitaani kwako unaanza kurecord na kutuma kwa mitandao...

Kile kimbelembele cha polisi kuingilia mishe za za watu kinaenda kuisha....

Hii ni nzuri, wapewe huo uwezo na siyo kutegemea polisi

Mfanyakazi anawajibika kwenye majukumu yake ya kazi unamletea mambo ya JINAI..

Pigeni kelele, Itapitishwa!
 
TISS siyo jeshi hakuna jeshi la usalama wa taifa hiyo ni taasisi tu kutoka ofisi ya Rais majeshi yametajwa katika katiba
kwahiyo rekebisha usiseme itatawala kijeshi sema itafanya utekaji na kuua maana hata kukamata siyo kazi yao
 
Nchi inaongozwa na Mapaka👇😁😁😁
AEb8rs.jpeg
16525976734300.jpg
AEb8rsjc_1.png
ummY_jc.jpg
 
View attachment 2643253

Nimeweka hii snapshot inayoonesha muswada wa mabadiliko ya sheria ya chombo chetu cha Intelejensia.
Kwenye mapendekezo hususan kifungu cha 19 wanasema hapo kuwa, jinai inaweza kufanywa na TISS personels wakiwa wanatekeleza majukumu yao kwa uaminifu....

Jambo linalonistua ni kwamba, wengi hudhani jeshi kutawala ni mpaka pale jeshi linapopindua serikali ya kiraia. Huu muswada umeleta tafsiri mpya ya utawala wa kijeshi. Tufuatilie kwa akili kubwa sana haya mambo yanavyopangiliwa kwa uangalifu kuelekea imla ya kijeshi...

Nipate elimu kutoka kwenu wanaJF

  1. Kuna ukamilifu gani kwenye jinai?
  2. Kuna uaminifu gani kwenye jinai
  3. Kipimo gani kinatumika kufahamu kuwa jinai fulani imefanyika during utekelezaji wa majukumu kwa uaminifu
  4. Aina gani ya jinai inayoombewa mabadiliko? Ya kutesa au kuua?
  5. TISS ni jeshi au kitengo cha uraia kinachofanya shughuli za kijeshi? Sheria za kimataifa zinasemaje kuhusu utendaji wa jeshi kwa raia?
  6. Huu muswada nani wameomba hayo marekebisho yaani ni TISS au Rais (taasisi/sponsor)?
Lengo na dhumuni la uzi huu siyo kubeza ama kuponda kazi kubwa wanayofanya TISS kwa nchi yetu, bali ninalengq kuangalia motive ya huu muswada ambao umekuja kana kwamba ni by the way lakini uzito wa sentensi zilizotumika kuuandaa ni wake up call kurecall matukio ya kijinai ambayo chombo chetu kitukufu kimehusishwa ama kunyooshewa vidole.

Kwa mahaba mema kwa nchi yangu, I submit

CC: Mzee Mwanakijiji Pascal Mayalla Retired raraa reree Extrovert Bujibuji Simba Nyamaume Mshana Jr zitto junior lumumbai Kiranga Erythrocyte mwanamwana MwanaWA Ebrania Gily Demi
Hiii document ilianza kuandikwa wakati wa Magufuli ambaye alitaka kuwa mungu- mtu kama akina Kabudi, Kangi Lugora na Aggrey Mwanri walivyokuwa wanamuona.

Nashauri haya mambo ya hovyo yaliyoanzishwa na Magufuli yafukiwe tu kaburini kama tulivyomfukia Magufuli mwenyewe Chato.
 
Nadhani kinacholeta hofu siyo hayo mabadiliko,zaidi ni aina ya watumishi wa Tiss wanavyopatikana hususani nyakati hizi.
Huko nyuma nadhani ni kati ya 1982/1983 wakati wa kuzuia jaribio la mapinduzi, Kuna mtu alikuwa akiitwa Kapteni Tamimu,alikuwa moja wa wasukaji wa jaribio hilo, kwenye operesheni hiyo ya kuwakamata huyo jamaa aliuawa na watu wa usalama, na bila shaka waliompigia risasi akiwa anajaribu kutoroka hawakuwa polisi, ninaamini ni watu wa idara, hakuna aliyeshtakiwa kwa kumuua Tamimu kwa kuwa walikuwa wakitekeleza majukumu yao kwa uaminifu.
Kwa hiyo kutokea kwa jinai kwenye mazingira kama hayo huwa haiepukiki.
Tatizo la msingi ni namna wanavyowapata hawa watumishi wa idara hiyo.
Huko nyuma ilisemekana watu walioingizwa kwenye hiyo idara, sifa ya kwanza ilikuwa ni uwezo mkubwa wa kutumia akili, kwamba,walifuatiliwa vijana wenye akili sana na utulivu mkubwa ndio walipendekezwa kuingia kwenye hiyo idara.
Na pengine ndio sababu haikuwa rahisi kuwatambua na hata kujulikana na wengi kuwa kuna chombo cha namna hiyo hapa nchini.
Sasa mambo yamebadilika, mimi nikiingia huko nahakikisha na ndugu zangu nao wameingia bila kujali kama wana akili ama hawana. Matokeo yake hakuna tena usiri.
Watu wa hovyo wameharibu taswira nzuri ya Tiss. Mambo ya kutesa au kupotezana tumeanza kuyasikia zaidi kipindi hiki.
Ninaamini kama misingi ya mwanzo ya kuajiri hawa watu ikirudishwa, watanzania hawatakuwa na hofu hata na hayo mabadiliko, tatizo unamtengenezea kinga mtu mhuni asiyejiheshimu, ni kweli ataumiza watu wengi.
Tiss wamekuwa wanasiasa,
Leo mtu anaweza akafoji kitambulisho cha Tiss na akabaki salama, akatesa watu na Tiss wenyewe wapo wanangalia tu. Tuliyaona hayo kwa akina Sabaya,kama idara ingetimiza wajibu wake pengine asingeachwa akaumiza watu kiasi kile.
Mabadiliko ya maana yaanze na watumishi wa idara kwanza.
Wasiwe wanasiasa kama ilivyo sasa na wapatikane kwanza kwa vigezo vinavyotakiwa, haswa uwezo wa kiakili na siyo ukereketwa wa vyama vya siasa.
 
Back
Top Bottom