Nadhani kinacholeta hofu siyo hayo mabadiliko,zaidi ni aina ya watumishi wa Tiss wanavyopatikana hususani nyakati hizi.
Huko nyuma nadhani ni kati ya 1982/1983 wakati wa kuzuia jaribio la mapinduzi, Kuna mtu alikuwa akiitwa Kapteni Tamimu,alikuwa moja wa wasukaji wa jaribio hilo, kwenye operesheni hiyo ya kuwakamata huyo jamaa aliuawa na watu wa usalama, na bila shaka waliompigia risasi akiwa anajaribu kutoroka hawakuwa polisi, ninaamini ni watu wa idara, hakuna aliyeshtakiwa kwa kumuua Tamimu kwa kuwa walikuwa wakitekeleza majukumu yao kwa uaminifu.
Kwa hiyo kutokea kwa jinai kwenye mazingira kama hayo huwa haiepukiki.
Tatizo la msingi ni namna wanavyowapata hawa watumishi wa idara hiyo.
Huko nyuma ilisemekana watu walioingizwa kwenye hiyo idara, sifa ya kwanza ilikuwa ni uwezo mkubwa wa kutumia akili, kwamba,walifuatiliwa vijana wenye akili sana na utulivu mkubwa ndio walipendekezwa kuingia kwenye hiyo idara.
Na pengine ndio sababu haikuwa rahisi kuwatambua na hata kujulikana na wengi kuwa kuna chombo cha namna hiyo hapa nchini.
Sasa mambo yamebadilika, mimi nikiingia huko nahakikisha na ndugu zangu nao wameingia bila kujali kama wana akili ama hawana. Matokeo yake hakuna tena usiri.
Watu wa hovyo wameharibu taswira nzuri ya Tiss. Mambo ya kutesa au kupotezana tumeanza kuyasikia zaidi kipindi hiki.
Ninaamini kama misingi ya mwanzo ya kuajiri hawa watu ikirudishwa, watanzania hawatakuwa na hofu hata na hayo mabadiliko, tatizo unamtengenezea kinga mtu mhuni asiyejiheshimu, ni kweli ataumiza watu wengi.
Tiss wamekuwa wanasiasa,
Leo mtu anaweza akafoji kitambulisho cha Tiss na akabaki salama, akatesa watu na Tiss wenyewe wapo wanangalia tu. Tuliyaona hayo kwa akina Sabaya,kama idara ingetimiza wajibu wake pengine asingeachwa akaumiza watu kiasi kile.
Mabadiliko ya maana yaanze na watumishi wa idara kwanza.
Wasiwe wanasiasa kama ilivyo sasa na wapatikane kwanza kwa vigezo vinavyotakiwa, haswa uwezo wa kiakili na siyo ukereketwa wa vyama vya siasa.