Sheria mpya ya TISS tusijifanye vipofu wakati kumbe tunatawaliwa ama tunaenda kutawaliwa kijeshi

Sheria mpya ya TISS tusijifanye vipofu wakati kumbe tunatawaliwa ama tunaenda kutawaliwa kijeshi

Chukua mfano wa Raila, tangu Kenya wapate uhuru yeye na baba yake ni wapinzani tu. Walitaka Uhuru wakapata uhuru ,(akiwamo Rais).

Wakataka majimbo wakapata majimbo (wao khasa walitaka ukabila, Dholuo wajitawale wamejitawala). Baadaye wakataka katiba mpya wakapata katiba mpya. Wakataka mahakama huru Wakataka kura huru wakapiga kura huru wakashindwa. Wakakata rufaa wakashindwa . Sasa wanaandamana kupinga bei ya mtori. Huyu utamchekea mpaka lini?

Na hapa tunaelekea huko, kumbuka migomo ya Muhimbili na vikundi vya UAMSHO. Kumbuka wasaliti wa makanikia.

Hivi utawachekea hadi lini? Sometimes, it's best to use other ways.
Duh 🙄
 
Nimetafakari sana na bado naendelea kutafakari kwa kina sana kuhusu sheria hii. Bado sijapata majibu kuhusu lengo hasa ya kuleta marekebisho haya, sijui lengo lao hasa ni nini?!?????
Napenda tena na tena kuwakumbusha watawala wa Tz ambao inaonekana dhahiri shahiri wengi wao wamelewa madaraka kwamba Makundi hatari ya watu kama vile Boko Haram, Al Shabab, IS, Al Qaeda, n.k, n.k, hayakuibuka hivi hivi tu huko katika nchi yalikoanzishwa Bali yameibuka kutokana na kukosekana kwa HAKI kwa raia wa kawaida/watawaliwa na kushamiri kwa vitendo vya DHULMA, MANYANYASO, UONEVU, na vitendo viovu vingi dhidi ya wananchi. Serikali ktk nchi husika zimekuwa hazitendi haki, zinanyanyasa raia kwa kuwatungia Sheria kandamizi kama hii sheria ya TISS. Matokeo yake wananchi wanafikia hatua ya kuchoka na kuamua kujitoa mhanga na kuchukua hatua ngumu za kujilinda na kujihami kwa kuanzisha makundi hatari kama Boko Haram au Al Shabab ambayo kimsingi yamefanikiwa pakubwa kuzidhibiti Serikali za kidhalimu ktk nchi zao. Kwa kutaka kupitisha Sheria hii ya TISS, kwa mbali naona kwamba makundi kama haya yakianzishwa kwa kasi hapa nchini, na kwa hakika yatapata uungwaji mkono pakubwa kutoka kwa wananchi wasiokubaliana na Sheria hii ya TISS.
 
Are you saying elQaeda wanataka tumehuru? Are you saying UAMSHO waliokuwa wanaua CCM na Polisi wapinzani hawaguswi Mbunge Mnyika akisema CCM wamejitakia, are you saying UAMSHO walitaka katiba mpya? You are just apologists for terrorists, watched TISS watulinde.
 
Naandika nafuta. Naandika tena kisha nafuta, basi ngoja niache. Ila nakukumbusha tu kwamba kama wewe upo Tiss au ni wakala wao utambue tu kwamba hakuna Serikali yoyote duniani ambayo imefanikiwa kupora haki zote za raia halafu bado ikabaki salama, hakuna, hakuna kabisa wala haijawahi kutokea na haitakuja kutokea, kamwe.
 
Chukua mfano wa Raila, tangu Kenya wapate uhuru yeye na baba yake ni wapinzani tu. Walitaka Uhuru wakapata uhuru ,(akiwamo Rais).

Wakataka majimbo wakapata majimbo (wao khasa walitaka ukabila, Dholuo wajitawale wamejitawala). Baadaye wakataka katiba mpya wakapata katiba mpya. Wakataka mahakama huru Wakataka kura huru wakapiga kura huru wakashindwa. Wakakata rufaa wakashindwa . Sasa wanaandamana kupinga bei ya mtori. Huyu utamchekea mpaka lini?

Na hapa tunaelekea huko, kumbuka migomo ya Muhimbili na vikundi vya UAMSHO. Kumbuka wasaliti wa makanikia.

Hivi utawachekea hadi lini? Sometimes, it's best to use other ways.
TISS huwa hawakurupuki, wanajua na wamefanya tafiti wana uhakika kwa 99% kuwa Watanzania hawana option zaidi ya kulalamika na kulia lia mitandaoni kama tunavyofanya hapa.

Natoa mfano mdogo, marehemu Membe (Mungu amrehemu) ilikuwaje anapewa nafasi za uongozi wakati Katiba inakataza wanajeshi kushiriki siasa. Nani asiyejua kuwa jeshi la intelejensia hakuna kustaafu?

Nafasi ya RC na DC ni za kisiasa na wanashiriki kamati za siasa kwenye ngazi zao lakini wapo wanajeshi wameteuliwa kwa nafasi hizo.....

Hivyo. Hapa kinachofanyika now ni kwamba mkondo wa maji umeshashika njia unaondoka na CCM. Wanachokifanya ni kulazimisha kupitisha sheria zinazowasaidia kujisimika madarakani. Kisichowasaidia ni kwamba wao ni wanadamu kama sisi hivyo hawawezii kupambana na Nguvu isiyoonekana.

Ni suala la kuendelea kuwazomea kwa haya wanayoyafanya kwani hawana nia njema na Tanzania yetu
 
Are you saying elQaeda wanataka tumehuru? Are you saying UAMSHO waliokuwa wanaua CCM na Polisi wapinzani hawaguswi Mbunge Mnyika akisema CCM wamejitakia, are you saying UAMSHO walitaka katiba mpya? You are just apologists for terrorists, watched TISS watulinde.
Ni kwa nini basi hao uliowataja kuwa ni UAMSHO walikuwa wanaua Polisi na CCM tu?? Kwa nini walikuwa selective kuua Polisi na Ccm pekee na kuwaacha wengine???
 
Are you saying elQaeda wanataka tumehuru? Are you saying UAMSHO waliokuwa wanaua CCM na Polisi wapinzani hawaguswi Mbunge Mnyika akisema CCM wamejitakia, are you saying UAMSHO walitaka katiba mpya? You are just apologists for terrorists, watched TISS watulinde.
Akwilina aliuawa na magaidi?
 
Kwa hiyo endapo TISS ndio hivi inatik, halafu POLISI qanafanikiwa kupenyeza Boss kutokea TISS na JWTZ hali kadhalika, maana yake itakuwa TIFWILI,yaani watakachoamua wao hichohicho, aaahaa, jamani, mbona maisha haya walau twaishi kwa upendo tu, why mnajiandae saaana jamani! Sio vizuri.

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
Boss wa Polisi wa sasa msidhani ni root ya huko alipotawazwa ubosi
 
Bunge linalazimisha kutengeneza mazingira ya mapinduzi. Coup huwa inatafutwa kwa justification au greedy, sasa bunge la CCM linarundika sababu mara CAG anatoa ripoti wanafungia maandazi hawachukui hatua, mara sheria za kuzuia mashkta kwa watu fulani na mengine mengi.
Careless beings
Itakuwa pouwa saana
 
Wanataka nchi iwe chini ya deep state moja KWA moja kiuongozi yaani hao jamaa wawe na mkono wa mmoja KWA moja KWA watawala namna ya kuiongoza nchi!

Kama hili au lile hawataki bas ukilazimisha unaenda na maji!

SASA Bas;

Kama ikitumika ku vema kuwabana viongozi waliopo madarakani Bas check and Balance itafanikiwa KWA asilimia zote! Elimination method itakua common KWA sana na imehalalishwa!!

Lakini kama just kama ikitumika vibaya,Aiseh hapatoshi kupotea nje nje kama kuku au kifaranga, jamaa wana malengo yao ya kuonyesha makucha wazi wazi hasa katika kipindi cha mabadiliko ya kimfumo ya kiutawala nchini!!!

Ngoja tuone!!
Tangu mwaka 2016, mara tu baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 utawala wa nchi umekuwa chini ya vyombo. Ndiyo maana kumekuwa na shutuma nyingi za unyanyasaji wa raia wenye mitazamo tofauti ya kisiasa, kesi za kubambikiza, utekaji na hata mauaji ya kisiasa. Mambo yote haya ni kinyume cha sheria na waliotekeleza wametenda jinai. Aidha, tunakoelekea ushindani wa kisiasa unapamba moto baada ya walioko madarakani kupoteza ushawishi miongoni mwa raia kwa kiwango kikubwa sana. Kilichobaki sasa ni kurasimisha ya matendo haramu na ya kijinai yaliyofanyika huko nyuma ili kuviwezesha vyombo kuwanusuru watawala wa sasa bila vyombo hivyo kujirundikia makosa ya jinai ambayo siku moja yanaweza kufuatiliwa.
 
Kosa na moja ya madhaifu ya kihistoria ni kuwa "mbwa mkali" wa CCM na kwa maslahi yao: badala ya Taifa.

Huwezi niambia kuna competent instruments halafu wahuni wanajigawia vyeo, wehu wanashika dola, rasilimali za nchi zinaporwa kila siku na kila mahali, watu wanapotezwa, kwenye diplomasia ya uchumi tunapigwa nk nk
Wao kama ilivyo jeshi la Polisi wanahitaji total overhaul. Sio protection au legalization; hii ni impunity sasa.
Wame abuse power before, je sasa unawaongezeaje kinga na wigo wa kijinai??
 
Mwanzo walikuwa wanateka, wanatesa na wanaua kama wasiojulikana, kinachobadilika sasa ni kuyafanya hayo kwa mujibu wa sheria.
P
Baba wa Taifa alithamini sana uhai wa raia ndiyo maana yalipobainika mauaji ya raia Shinyanga wanasiasa waliwajibika na watendaji wakiwepo wanausalama wakaachishwa kazi na kufunguliwa mashtaka. Ule ulikuwa usalama wa taifa na raia wake. Awamu ya tano iliigeuza idara ya usalama wa taifa kuwa chombo cha kudhibiti na kuua ushindani wa kiasi na uanaharakati wa kutetea haki za kiraia kibinadamu.
 
Hao jamaa wa TISS wataanza kuua watu hasa wapinzani wa watawala na hawatochukuliwa hatua yoyote ile kwa sababu sasa wana Kinga.

Na wanaCCM watakuwa wajinga wakidhani kuwa hii itaenda kuwagusa wapinzani tu, atatokea mtawala kichaa ataanza kuwashughulikia kupitia watu wa usalama wa Taifa na hawatakuwa na yeyote wa kumhold accountable
Wana-ccm wengi hawana hiyo akili ya kila mmoja kutafakari hii sheria kama mtu binafsi. Wengi wanachotazama zaidi ni kuwa sheria itakiwezesha chama chao kung'ang'ania na kuhodhi madaraka ya dola. Hawaangilii mambo yaliyowapata wenzao kama wanachama na raia mmoja mmoja: Bashe, Serumba, Malima, Ndugai na pengine hivi karibuni yanayoweza kumpata Balozi Karume kwa kuzungumza maoni yake binafsi kuhusu chaguzi za visiwani.
 
Baba wa Taifa alithamini sana uhai wa raia ndiyo maana yalipobainika mauaji ya raia Shinyanga wanasiasa waliwajibika na watendaji wakiwepo wanausalama wakaachishwa kazi na kufunguliwa mashtaka. Ule ulikuwa usalama wa taifa na raia wake. Awamu ya tano iliigeuza idara ya usalama wa taifa kuwa chombo cha kudhibiti na kuua ushindani wa kiasi na uanaharakati wa kutetea haki za kiraia kibinadamu.
Kwenye ile Kesi ya Mauaji Mwanza ya mwaka 1976, Dingi wangu alikuwepo, salama yake ni Wakili Murtaza Lakha, akachomoka, lakini wengine wote walikula mvua za kutosha!. Sasa hakuna kushitakiwa!.
P
 
Kwani kwasasa haiwalindi? Mbona wamempoteza Ben watcheight? Mbona wamemtandika Lissu risasi? Kuna aliyeshitakiwa? Kwani hii sheria ndiyo itawaruhusu kuua hadharani huku watu wakiwaona na kutembea bila wasiwasi kama wafanyavyo polisi wakiwa field? Si wataendelea kufanya kwa kificho hicyo hivyo? Sasa mantiki ya kuwa na sheria ya kuwalinda ni nini? Kwani kuna aliyewahi kushitakiwa? Kama yupo unaweza kuweka hiyo case hapa?
Kwa sasa sheria haiwalindi bali wanapotenda jinai kwa maslahi ya watawala mamlaka za kusimamia utekelezani wa sheria zinafumba macho na hakuna njia ya mtu mwingine kuwalazimisha kuchukua hatua. Hii ni IMPUNITY, siyo kinga. Aidha kwa vile jinai haifa hofu imetanda kwamba mabadiliko ya kiutawala yanaweza kutokea wakati wowote. Hivyo lengo la marekebisho ya sheria ni pamoja na kuwapa nguvu hao wenye tuhuma za jinai na 'impunity' kusaidia kuzuia uwezekano wa mabadiliko ya utawala.
 
Huu muswada uliandaliwa kipindi Cha mwendazake, sijui bi mkubwa kaupendea nn aisee... yaani tunaenda kuunda majambazi watakaokuwa wanafanya ujambazi kisheria... Wakikupora sawa tu, wakikuua sawa tu..wakikuteka sawa tu... yaani kiukweli cjui sasa kama polisi watakuwa na kz gn sasa... Mmmmhhhh hii nchi ngumu sana aisee
Kama alivyobeba kesi y Mbowe ya Kurithi naona wamemwingiza chaka tena.

Sema kaona faida yake kunako 20-25
 
Huu muswada uliandaliwa kipindi Cha mwendazake, sijui bi mkubwa kaupendea nn aisee... yaani tunaenda kuunda majambazi watakaokuwa wanafanya ujambazi kisheria... Wakikupora sawa tu, wakikuua sawa tu..wakikuteka sawa tu... yaani kiukweli cjui sasa kama polisi watakuwa na kz gn sasa... Mmmmhhhh hii nchi ngumu sana aisee
Awali hakuwa na tamaa ya nafasi ya juu ya uongozi wa nchi. Lakini mara tu baada ya kuonyesha kutokuwa tamaa hiyo inaelekea kuna watu walishtuka na kujawa na hofu ya mustakabali wao kisiasa na kiutumishi. Inaelekea aliwekwa kiti moto na kuaminishwa kuwa kwa mtaji huo alikuwa anahatarisha uhai wa chama chake na uimara (stability) wa nchi! Bila shaka walioshiriki kwa karibu zaidi kumbadilisha mtazamo ni hao hao ambao katika utawala wa awamu ya tano walitumiwa vibaya kuuhami uongozi wa kisiasa dhaifu ambao ulivilamisha vyombo kufanya uhalifu wa makosa ya jinai kwa kisingizio cha kutekeleza majukumu ya usalama wa taifa! Aidha kiongozi ameaminishwa pia kutumia kuna fursa ya upande wa pili wa nchi kuendelea kutoa kiongozi mkuu wa nchi!. Kwa mantiki hii, zipo dalili za Chama cha upinzani chenye nguvu upande mmoja tu nchi kuungana na chama chenye serikali kuiunga serikali mkono serikali iliyopo madarakani. Aidha chama hicho cha upinzani kimetamka kuwa haina nia ya kuwa na mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano 2025.
 
Back
Top Bottom