Nimetafakari sana na bado naendelea kutafakari kwa kina sana kuhusu sheria hii. Bado sijapata majibu kuhusu lengo hasa ya kuleta marekebisho haya, sijui lengo lao hasa ni nini?!?????
Napenda tena na tena kuwakumbusha watawala wa Tz ambao inaonekana dhahiri shahiri wengi wao wamelewa madaraka kwamba Makundi hatari ya watu kama vile Boko Haram, Al Shabab, IS, Al Qaeda, n.k, n.k, hayakuibuka hivi hivi tu huko katika nchi yalikoanzishwa Bali yameibuka kutokana na kukosekana kwa HAKI kwa raia wa kawaida/watawaliwa na kushamiri kwa vitendo vya DHULMA, MANYANYASO, UONEVU, na vitendo viovu vingi dhidi ya wananchi. Serikali ktk nchi husika zimekuwa hazitendi haki, zinanyanyasa raia kwa kuwatungia Sheria kandamizi kama hii sheria ya TISS. Matokeo yake wananchi wanafikia hatua ya kuchoka na kuamua kujitoa mhanga na kuchukua hatua ngumu za kujilinda na kujihami kwa kuanzisha makundi hatari kama Boko Haram au Al Shabab ambayo kimsingi yamefanikiwa pakubwa kuzidhibiti Serikali za kidhalimu ktk nchi zao. Kwa kutaka kupitisha Sheria hii ya TISS, kwa mbali naona kwamba makundi kama haya yakianzishwa kwa kasi hapa nchini, na kwa hakika yatapata uungwaji mkono pakubwa kutoka kwa wananchi wasiokubaliana na Sheria hii ya TISS.