Sheria ya Jeshi kuhusu mavazi ni ya kishamba na kizamani sana

Hakuna. Wanafikiri kuvuta bangi na kujichetua na magwanda ndiyo uanajeshi kumbe ni ushamba tu
Majesh yanayojielewa yanaondoa mafisadi wao wanapambana na nguo za mitumba[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ndugu, sipingi maoni yako kwamba ni Mambo ya kizamani.Kama unaona ni Mambo yaliopitwa na wakati,hakuna aliyekukataza kuvaa.Jeshi halijakurupuka kutangaza jambo hili.Imefika wakati wa kutoufautisha matamko ya kisiasa na ya kijeshi.Nawashauri wanaoona kwamba haya ni Mambo ya kizamani WAVAE Weekend njema
 
Sijasema wapige raia ila naona sio sawa raia kuvaa sare zinazofanana na majeshi.
Mbona CCM huvaa magwanda ya kijani wakati JWTZ nao Wana rangi hizo hizo?

Hoja hapa ni kuwa rangi ya vazi la raia fulani kufanana na rangi ya vazi ya jeshi haiwezi kuwa ni sababu ya kutosha kusema "amevaa vazi la jeshi"

Huu ndio ujinga na ushamba mkubwa kuliko wote unaosemwa na mleta hoja Sexless otherwise watuambie mstari wa vazi la jeshi na raia kwa kigezo cha rangi tu unauchorea wapi hasa kabla kuhukumu watu?
 
asanteni watanzania, hii inaonyesha watu wameelimika... mkoloni mweusi ajiandae naona watu vichwa vimeanza kupata moto. Walikuwa polis na sasa hata wanajeshi wameanza kuchafua taswira kwa wananchi. Huwezi ukampiga raia et kisa kavaa vazi ambalo hajaliiba ila tu limefanana na lako... hayo mavazi wanavaa kwa sababu ya kodi zetu halafu wanaleta mambo ya hovyo... jeshi umefika muda mbadiri sheria na taaribu zenu muda hauwasubiri oooooh,
 
Ngoja nitafte shuka la kijeshi nitandike muda wa mizagamuano [emoji23][emoji23]

Kijeshi jeshi zaidi
 
Mtu aliyevaa nguo zinazofanana na za jeshi huwa anavimba kuliko mjeda.

Wanaopenda kuvaa sare wakanunue za simba na yanga zinafaa kuvimba pia.
Nimeshona mpk sofa za mabakamabaka sasa kwa taarifa yako.
 
Hivi imagine Kila kitu kinafanana kasoro nembo huoni Kwa tz inaweza kutumika kutapeli au kuonea watu...huko vijijini raia wanajua kweli mambo ya nembo?
Umeshafanya utafiti ukajua tatizo ni kiasi gani au unatumia hisia tu na mawazo binafsi?

Hizi nguo ziko duniani kote mitumba na Mpya na dunia nzima majeshi yanatumia nguo zenye mwelekeo huo.
 
Mtu aliyevaa nguo zinazofanana na za jeshi huwa anavimba kuliko mjeda.

Wanaopenda kuvaa sare wakanunue za simba na yanga zinafaa kuvimba pia.
Yaani mnalifanya kama vile nitatizo la kitaifa wakati ktk Watu 60 unaweza kukuta wenye nazo hawazidi hata 500
 
Kaa kimya kama hujui.

Kombati ya jwtz ina nembo gani.

Hata sare zingine zina nembo gani,

Hiyo midomo yenu na Maandishi mnatumie vizuri

Vaa uone
 
Eti usajili wakikukuta na Tattoo napo wanasema umedisqualify,ukiuliza tatoo ina shida gani hawana majibu.

Wenzetu huko majeshi yao yana watu wana tatoo za hatari na wanatumikia jeshi safi bila tatzo,ishu ipo huku kwetu
Huko wanapokea hadi Mashoga, vp hapa kwetu nao wapokelewe?
 
Nadhani haujui madhara ya unachokitetea.
 
Lakini Kwa nini na wewe raia utake mavazi ya jeshi lakini??? SI uchokozi huoo ni kumshika mwanaume matako huko
Sio sare ya jeshi tu bali sare ya taasisi yoyote kama wewe sio mhusika unaivaa ili iweje? Hata sare shule kama wewe sio mwanafunzi kwanini uvae sare ya shule? kwa hali yoyote ile unataka kufanya ualifu ili ujifiche kwenye sare husika.Kama kuvaa sare inakupendeza vaa ya Mgambo basi.
 
Wao wenyewe wameshaona,kizazi kimeshaamka.
 
Nchi inanuka umasikini na ujinga ila sare za jeshi ni muhimu zaidi[emoji23][emoji23][emoji23]
Kweli bara la giza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…