Sheria ya Jeshi kuhusu mavazi ni ya kishamba na kizamani sana

Sheria ya Jeshi kuhusu mavazi ni ya kishamba na kizamani sana

😄 🤣 tembea uone baba
Kuna border ya jirani zetu huko, wale waliuana sana wakatuletea na majambazi ya silaha
Huko unauziwa mpaka AK47 hata rocket launcher ukitaka unabadilishiwa kwa gunia 4 za mahindi 😄
Halafu nilienda Beirut miaka ya nyuma watoto wanachezea hand grenades
Yaani Dunia ina mambo hii

🇺🇸 unaweza kuwa na jeshi la mtu mmoja yaani unanunua tu unaweka
Kweli tembea uone maajabu 😂😂
 
Kweli tembea uone maajabu 😂😂
Washaanza kurudisha
Screenshot_20230901-143957.png
 
Dah! Wewe mbona ni mjinga sana aisee? Kanzu ni vazi la ibada???
Kanzu sio vazi la ibada bali ni vazi linalovaliwa zaidi na waarabu huko Arabuni na hushonwa kwa staili tofauti tofauti baina ya nchi na Nchi !
 
Mtu kama wewe ilibidi hata usiandike. Sijui unavyosema Nchi gani sijui unasema wapi, labda wewe umetembelea Burundi au Congo huko ndiyo hutaona. Unajua nchi yetu ni ya kishamba sana, wewe fikiria tangu mwaka 1961 tupate kujitawala hadi leo hakuna hata fashion shop yoyote ile ipo Tanzania, niambie ipi? Under Armor wanauza fashion nyingi za aina hiyo, wanaweza kuwa na shop Tanzania? GAP etc. Acha upumbavu; umezoea mitumba unaona fashion
Wewe mpumbavu acha kufananisha Tanzania na hizo nchi zingine. Kama una hamu ya fashion shop hamia kwenye nchi ambazo zipo. Watu wanaumiza vichwa kuona tunaendelea kuishi kwa amani halafu wewe unaleta ubishi wa kingese. Huo upumbavu mpelekee mama yako aliyeshindwa kukulea kwa maadili mema.
 
Nimemsikiliza askari aliyekuwa akihojiwa na CloudsTV anasema sheria ya mavazi ya jeshi unasema;-
"Ni marufuku raia kuvaa sare za jeshi ama mavazi yanayofanana na sare za jeshi". Ili iweje?

Yaani ktk zama hizi za sayansi na teknolojia bado jeshi letu linataka kujitofautisha na raia kwa mavazi? Mwanajeshi ajitofautishe kwa umahiri wa kung'amua na kuzima nia na jaribio la adui kutaka kuivamia nchi yetu. Baasi! Siyo hizi blah blah za kuwalingishia raia gwanda za jeshi.

Kule nchi za watu mpk walevi na mateja wanavaa mavazi yanayofanana na sare za majeshi ya nchi zao. Mbona hatujasikia wakipata shida ya kiusalama?

Tuachane na ushamba huu. Nakumbuka hata bendera ya taifa kabla ya Kikwete kuwa rais ilikuwa ni marufuku kukutwa hata na leso inayofanana na bendera yetu ya taifa. Mhe. Kikwete akaondoa ushamba huu.

Ni wakati wa kuondoa ushamba wa kuzuia raia mavazi yanayofanana na sare za kijeshi sasa.
Upo sahihi...kuna na ile ya "ni marufuku kupiga picha hapa" [emoji3]...wakati ambapo nikitumia Google earth naweza kuona kila kitu mpaka mtu aliyekuwa anaenda chooni wakati satellite ilipochukua picha last time!

These people need to change!
 
badala ya kubeza na kufokea wanajeshi tungelishauri jeshi letu kupitia bunge kutunga sheria mpya zihusuyo mavazi yake.
ili kutokwanza raia wenye mapenzi na rangi za nguo hizo za jeshi basi uandaliwe utaratbu mzuri wa mtu kuzivaa,endapo atauvunja basi awajibike mfano-

1-ni ruksa kuvaa isipokuwa uniform kamili,yaani mpaka ishindikane kutofautisha raia na mwanajeshi/askari aliyeko kazini.

2-ni marufuku kuvaa nguo hiyo na malapa,singilendi,kuivaa mlegezo,au kulewa ukiwa nayo.

3-usiivae nguo hiyo na alama yoyote ya cheo,au alama nyingine zinazowakilisha cheo na mamlaka ya maafisa na askari.

4-marufuku kuonekana umevaa nguo hiyo kisha unakata viuno,umelewa sana mpaka umeanguka😂😂.

5-ukivaa chochote kati ya nguo hizo koti,mkoba ama begi,ama rain coat hakikisha ni visafi kweli kweli.

hii ingejengea zaidi jeshi heshima kuliko kuendelea kulichoresha kama ilivyo sasa.
 
Kila nchi inaongozwa kwa utaratibu huwezi kuamka tu huko Umeshiba maharage unafikira kuvaa Combart za jeshi Watu wametoa machozi,jasho na damu kuzipata hizo.

Licha ya hivyo Tukumbuke kuwa kila mtu akianza kujiamria kutumia Mavazi ya Jeshi au taasisi yoyote kwa kuamua tu sidhani kama itakuwa sahihi.

Na hakuna nchi ambayo mtu anaamua tu kuvaa combart its Either ni msanii ama mwanamziki ambao kwa sheria hiyo hiyo ya Penal code 178 imeruhusu mtu yyte kutumia ila kwa kibali maalum cha kuzitumia kwa shughuli za kisanii

View attachment 2734897
Sheria hii ifanyiwe marekebisho, adhabu iongezwe!
 
Mwanafunzi hapendi kuvaa sare za shule

Madereva na makonda hawapendi kuvaa sare zao za kazi

Majeshi hawapendi kuvaa sare zao za kazi

Ninyi wananchi ambao hamna sare mnanini hadi kutaka kuvaa sare au nguo zifananazo na majeshi?

Ushauri wangu kwa wale wote wanaopenda kuvaa sare za wenzao za kazi. Wachukuwe za madereva daladala maana wao hawapendi kuvaa!
 
Acha dharau wewe kenge unalifikilia jeshi kwa mihemko yako na wivu zako kujifanya unajua kumbe tahira mmoja hivi. Hujui kila taifa lina muundo na taratibu zake za maisha na maamuzi. Kwetu watu walionekana kutumia sare za jeshi kutapeli watu then unakurupuka na ujinga wako. Ulienda shule kujifunza ujinga unashindwa kung'amua cultural diversities beyond the global world unataka kufananisha tz na marekani ww mjinga nini. Siku nyingine usilete ujuaji dhidi ya jeshi la medani.
Mjeshi naona umewaka hatari
 
Back
Top Bottom