Sheria ya Kikristo inasemaje kwa mtoto wa nje ya ndoa?

Sifahamu,lakini mimi nimezaliwa nje ya ndoa,
Namshukuru sana baba yangu kwasababu amefanya majukumu yake 💯% sawa sawa na watoto wake wengine hajapunguza, zaidi kaongeza kwangu.......alinichukua na kunilea mimi ndani ya ndoa yake,nikiwaa na mwaka 1 tu hivyo mama yangu mzazi hajanilea mimi hata sijawah kuishi naye,

Wanaume msiwazae watoto nje ya ndoa kwasababu wanateseka sana kwakukosa upendo kutoka kwa ndugu zao,kama kutengwa n.k

Mimi ni baba pekee ananipenda ila kuanzia mama Hadi watoto yaan ndugu zangu hawanipend kabisa na huthubutu hata kusema hadharan mimi siyo ndugu Yao. Ila nimeishi nao,wamenilea kwa nguvu ya baba kwasababu baba SI ndye mwenye nguvu NYUMBANI

Kwahyo ushauri wangu kwa wanaume na wanawake msizae hovyo kama hampo kwenye ndoa au hamna mpango wa kuoana,

Mimi Leo Sina kaka Wala dada Wala Nan kwasababu hawanihitaji,

Ila ninachojua baba yangu ananipenda sana,na huyu ndiye rafiki yangu pekee nimebaki naye,basi namuombea kwa Mungu amjaalie maisha marefu niendelee kumuona.

Kuhusu urithi mimi sihitaji urithi

Huyo ni mtoto wako huo ni mkojo wako brooo

Unaweza kumtengenezea mipango mizur ukiwa bado upo hai......
 
na kwa bahati mbaya kwao au nzuri kwako, watoto kama wewe ndio huwa wanakuja kufanikiwa sana, Mungu huwa hawaachi hata kama wanadamu wanawakataa. mtoto akizaliwa hana hatia, hutakiwi kumhukumu kwa sheria za dini wala za dunia, ni kiumbe wa Mungu na Mungu anampenda na huwa anawapigania hata katika masumbufu yote wanayopitia. wanapitia shida nyingi na ni shida hizo huwa zinawakomaza na wanakuwa na mafanikio sana baadaye.

Mke wangu ni mtoto wa kambo. huyo baba yao aliwazaa wawili kwa mama yao, na alikuwa na ndoa yake. alikuwa mtu mwenye mafanikio. alipokufa, mke wangu ambaye alikuwa anatunzwa kabisa na huyo baba, kwenye kikao akatamkiwa kuwa wewe sio mtoto wa huyu baba, akaondolewa; kwenye msiba yaani. shida ilikuwa, walitaka wapunguze idadi ya watu watakaorithi. wife alikuwa na miaka kama 11 tu wakati huo. ameishi kwa mateso sana na single mamamkwe. ajabu yake, waligawana hiyo mimali yao, wameitapanya yote, mke wangu alikuja kusoma shule kwa shida akafanikiwa, amekuja kuolewa na mimi mwenye mafanikio pia, tumejenga maisha yamekuwa mazuri mbali kuliko ya wale waliomfukuza siku ya msiba. sasa miaka kama 5 iliyopita, mmoja mmoja akawa anakuja kutusalimia, anasema yeye ni kaka na wengine dada wa mke wangu, ati mke wangu ni mtoto wa baba yao. na kweli ukiwaangalia wanafanana mno, hadi mashangazi zake wamefanana kila kitu. ni kwasababu tu Biblia imetuamuru tusilipe baya kwa baya, sisi tunawalipa mema, na ninawaita mashemeji. ila wanajisikia vibaya hadi leo namna walivyomtreat wife.
 
Kimsingi watoto wote wako sawa hata kama umezaa kumi kwa mama tofauti ni lazima wote wapate urithi toka kwa baba yao. Hali kadhalika mwanamke naye kama amezaa na wanaume tofauti watoto wake wote ni sawa ila mwanaume hawajibiki kuwagawia urithi watoto wa mke wake ambaye hakuzaa naye.
Mkuu kwa mfano nimeoa mwanamke tayari ana mtoto na nikazaanae tena watoto wanne tuka bahatika kuwa matajir na vitega uchumi mfano Hoteli, kituo cha mafuta na Nyumba kumi, Sasa Mke na mume wamefariki je yule mtoto ambaye hakuzaliwa na Baba je na yeye ana haki ya kudai urithi wa mali za Mama yake?
 
hana haki yeyote. ila anaweza kupata nje ya haki za warithi, yaani baba aamue kwa siri amwandikie zawadi kwa njia ya wosia, na wosia huo usizidi 1/3.

sio hilo tu. wewe hapo ukichepuka kwenye ndoa, mtoto akazaliwa, ukifa huyo wa nje ni mtoto wa kambo, hatarithi. ana kosa gani? wakati kosa ni la baba mzinzi.
 
Mkuu kwa mfano nimeoa mwanamke tayari ana mtoto na nikazaanae tena watoto wanne tuka bahatika kuwa matajir na vitega uchumi mfano Hoteli, kituo cha mafuta na Nyumba kumi, Sasa Mke na mume wamefariki je yule mtoto ambaye hakuzaliwa na Baba je na yeye ana haki ya kudai urithi wa mali za Mama yake?
kibinadamu/kimalezi huyo mtoto anastahili kurithi hizo mali pamoja na watoto waliomfuata kwa mama yake, ila tu kama mtoto huyo alikulia hapo alipoolewa mama yake. Kama mtoto huyo hamkulea na alikulia nje ya himaya yenu hapo urithi haumhusu labda wadogo zake au ndugu waamue naye agawiwe. Ushiriki wa mtoto kwenye upatikanaji wa mali alikoolewa mama yake unampa uhalali wa kurithi sawa na watoto wengine. Ndio maana siku hizi ukioa mama mwenye watoto atalazimika kuwaacha kwao akaanze kuzaa upya kwa mume mwingine ili watoto wa boma wajulikane
 
kwa kifupi, wale watoto wa kwenye ndoa wakisimamia mstari, kwamba sheria ifuatwe, hatarithi chochote. na wapo sahihi kwa mujibu wa dini hiyo.
 
All in all urithi unatakiwa ugawiwe kwa watoto bila kujali walizaliwa vipi maadam tu wamekulia kwenye boma walikolelewa
 
kuran imekataza ndugu, na huwezo kuammend kuran. na hutakiwi kwenda kinyume nayo, wewe kama muislam jua watoto wako wa kambo hawana kitu, kama unawapenda andika wosia mapema na wosia wake hata kama watoto wapo 50, usizidishe 1/3 ya mali zako kuwapa kama zawadi ila sio watu wanaostahili urithi toka kwa baba.
 
Sheria ya kikristo; Mtoto wa nje ya ndoa hana haki ya kurithi mali za baba yake, atahesabiwa kwenye mali za mama yake tu!

Lakini hii sheria inasaidia kupunguza wale michepuko wanaopenda kutega mimba kwa waume wenye pesa

Lakini inaleta shida kwa watoto waliozaliwa nje ya ndoa kuendesha maisha yao wakiwa wadogo baada ya baba kufariki
Ushauri; Mwanaume ukizaa nje ya ndoa mpe mtoto urithi mapema kuepusha matatizo ukifariki.
Hiyo sheria haipo Tanzania. Mtoto wa nje ya ndoa ana haki ya kurithi mali za baba yake.
 
kuran imekataza ndugu, na huwezo kuammend kuran. na hutakiwi kwenda kinyume nayo, wewe kama muislam jua watoto wako wa kambo hawana kitu, kama unawapenda andika wosia mapema na wosia wake hata kama watoto wapo 50, usizidishe 1/3 ya mali zako kuwapa kama zawadi ila sio watu wanaostahili urithi toka kwa baba.
Nipe kifungu cha Quran kinavyosema juu ya hili. Mpaka leo kuna Maulamaa hawakubaliani na hili.
 
Hakuna sheria ya malezi ya mtoto au watoto wa nje ya ndoa. Cha zaidi utatafutiwa vimistari vya wizi wizi na ya kutunga kwa hadithi na visa vya hapa na pale but hakuna sehemu imeongelea direct kuhusu malezi ya mtoto nje ya ndoa sababu maagizo yapo kabisa kuwa mahusiano halali ni yale ya ndani ya ndoa tu.

Nje ya ndoa chochote ni batili.
Soma sheria ya mtoto. As long as kazaliwa wazazi wanawajibika kumpatiq mahitaji yote ikiwemo kurithi mali za wazazi. Yeye hana kosa kuletwa duniani kwa hiyo asihukumiwe kwa makosa ya wazazi wake.
 
Nipe kifungu cha Quran kinavyosema juu ya hili. Mpaka leo kuna Maulamaa hawakubaliani na hili.
kwa taarifa yako, hiyo hoja ndiyo inayofanya sheria ya mirathi Tanzania au hata ile ya ndoa, isirekebishwe,kwasababu utakinzana na kilichopo kwenye icho kitabu chenu ambacho mnasema hakitakiwi kurekebishwa. kwenu ninyi kurekebisha kile kuran imesema mnasema ni kufuru. hadi leo tumeishia watoto wa kambo kunyimwa haki, na binti akivunja tu ungo mnataka aolewe, watoto wenyewe wanavunja hata wakiwa na miaka 10.

aisha alivunja kiwa na 9 na mood aliendelea naye. this is the problem.
 
Sheria ya kikristo; Mtoto wa nje ya ndoa hana haki ya kurithi mali za baba yake, atahesabiwa kwenye mali za mama yake tu!

Lakini hii sheria inasaidia kupunguza wale michepuko wanaopenda kutega mimba kwa waume wenye pesa

Lakini inaleta shida kwa watoto waliozaliwa nje ya ndoa kuendesha maisha yao wakiwa wadogo baada ya baba kufariki
Ushauri; Mwanaume ukizaa nje ya ndoa mpe mtoto urithi mapema kuepusha matatizo ukifariki.
Indian succession Act uliwahi kuisikia? ndiyo tunayotumia. pia, wakristo hawabanwi na kile kilichopo kwenye Biblia kwasababu Biblia hayo mambo haikuweka, iliweka tu kwamba tuishi kwa upendo, vile unataka mtu akufanyie na wewe mfanyie hivyohivyo. kama wewe ungekuwa mtoto wa kambo unaona ukinyimwa urithi kingekuuma basi usimnyime mwenzio. na hii inatufanya tuwe flexible hata kwenye maamuzi ya Mahakama kuu ambayo yameshaeleza kwamba watoto wote ni sasa, wale wa kambo na wasio wa kambo.
 
kwa taarifa yako, hiyo hoja ndiyo inayofanya sheria ya mirathi Tanzania au hata ile ya ndoa, isirekebishwe,kwasababu utakinzana na kilichopo kwenye icho kitabu chenu ambacho mnasema hakitakiwi kurekebishwa. kwenu ninyi kurekebisha kile kuran imesema mnasema ni kufuru. hadi leo tumeishia watoto wa kambo kunyimwa haki, na binti akivunja tu ungo mnataka aolewe, watoto wenyewe wanavunja hata wakiwa na miaka 10.

aisha alivunja kiwa na 9 na mood aliendelea naye. this is the problem.
Sasa mbona kama unapingana na mimi. Nimemuambia alete hicho kifungu cha Quran kinachosema kuwa mtoto wa nje harithi kwa baba yake, kama hakuna, hizo sijui hadithi hazina mashiko. Kwa sheria za Tanzania, hata mtoto wa nje ya ndoa ana haki ya kurithi mali za baba yake.
 
wewe ni mwanasheria, tuanzie hapo.

kwa habari ya hawa watu, achana na sheria ya mtoto 2009, achana na indian succession Act au predecents za hivi karibuni zinazosema mtoto anarithi. kwa hawa waislam, sheria inayotumika pindi mtu akisema ni muislam ni kuran, na kwenye kuran imekataza kumrithisha mtoto wa kambo. maamuzi yote yaliyotoka ni ya Mahakama kuu, jaji wa mahakama kuu hafungwi, hata kama kama kuna kesi inasema watoto wote wanarithi, haimzuii jaji mwingine kudepart aendane na kuran hata kama sheria ya mtoto ipo.
 
Hizo story za vijiweni. Juzi tu watoto wa kaka yangu wa nje wamepata urithi wa mali za baba yao mahakamani ingawa kaka ni muislam.
 
Inategemea mirathi imegawanywa kwa utaratibu gani. Wapo waislam ambao hugawa mirathi kwa utaratibu Wa kiserikali au kimila.Ila kwa Sheria ya kiislam mtoto Wa nje ya NDOA hapati chochote.
 
Habari za uzima, naamini mmeamka salama, wale walio na magonjwa Allah akawape wepesi na mlio hospitali Mungu akawape wepesi pia mtoke huko, sio kuzuri na hakuzoeleki.

Rejea kichwa cha habari hapo juu, wenye ufahamu - mzazi wa kiume akifa watoto wa nje kwa dini ya kikristo wanarithi?

Ukristo hauna sheria Mkuu.
Ukristo kanuni kuu ni Neema(upendo wa agape).
Hivyo kwenye Ukristo hakuna mtoto wanje wala wa ndani. Watoto wote ni sawa mbele za Mungu.

Kwa wakristo kilichoumbwa na Mungu sio haramu.
 
Inategemea mirathi imegawanywa kwa utaratibu gani. Wapo waislam ambao hugawa mirathi kwa utaratibu Wa kiserikali au kimila.Ila kwa Sheria ya kiislam mtoto Wa nje ya NDOA hapati chochote.
Sheria za kiislam zinaaply wapi? Mirathi zote lazima zifunguliwe kisheria mahakamani. Na kwa sasa mahakama hawatumii sheria za kiislam sababu zinambagua mtoto kinyume na sheria ya mtoto na haki za kibnadanu.
 
Back
Top Bottom