Sheria ya Kikristo inasemaje kwa mtoto wa nje ya ndoa?

Sheria ya Kikristo inasemaje kwa mtoto wa nje ya ndoa?

wewe ni mwanasheria, tuanzie hapo.

kwa habari ya hawa watu, achana na sheria ya mtoto 2009, achana na indian succession Act au predecents za hivi karibuni zinazosema mtoto anarithi. kwa hawa waislam, sheria inayotumika pindi mtu akisema ni muislam ni kuran, na kwenye kuran imekataza kumrithisha mtoto wa kambo. maamuzi yote yaliyotoka ni ya Mahakama kuu, jaji wa mahakama kuu hafungwi, hata kama kama kuna kesi inasema watoto wote wanarithi, haimzuii jaji mwingine kudepart aendane na kuran hata kama sheria ya mtoto ipo.
Siku hizi hayapo haya huko mahakamani.
 
kwa nn itumie sheria ya serikali dini kama dini kwa nini ikose sheria zake binafsi?
Uislamu ni Mfumo wa maisha ya kiarabu kwa ujumla wake.
Ukristo ni dini ambayo inampa muhusika Uhuru wa kutenda mema na kuchukia Mabaya.

Ukristo unamasuala ya dini na masuala ya utamaduni wa eneo husika.
Mfano suala la mirathi limeachwa kwenye utamaduni husika kwa kuwa Mungu halupangii Matunizi ya Mali zako na namna ya kuzitumia ni suala binafsi au mahali ni suala la utamaduni sio dini, uwe umelipa mahali haujalipa ndoa utafunga kwa kuwa dini haihusiki na mahali.

Ukristo umejikita kwenye Jambo la msingi ambalo ni kumpenda Mungu na jirani na kuwatendea ipasavyo wengine.
 
Sheria ipo Hadi Leo.Muislam akiamua kuwa akifa mali yake igawanywe kiislam itagawanywa. Endapo familia yake ikiamua kuwa mirathi igawanywe kiislam pia itagawanywa.Serikali haijawahi kuingilia mambo yanayohusu Imani kukwepa kuvunja ibara ya 19 ya Katiba ya Tanzania.
 
Sheria ipi ? Hizi za kuletwa na wazungu . Mtoto wa zinaa ni wa zinaa milele hata iweje .

Jamii za kiafrica zinatambua hilo kuna kumtakasa kwa vile sio halali .
Hizo unazodai zimeletwa na wazungu ndio sheria zinazitumika sasa kwenye maamuzi! Kumbuka mirathi ya kikristo haigawanywi makanisani bali mahakamani!
 
Hizo unazodai zimeletwa na wazungu ndio sheria zinazitumika sasa kwenye maamuzi! Kumbuka mirathi ya kikristo haigawanywi makanisani bali mahakamani!
Zinatumika nchini kwako ila zina makosa kibao, sikiliza ndugu yangu mbona wanakataa kuweka pesa chafu kweny mzunguo wanasema ni kutakatisha pesa (money laundering) .

Ukichambua sheria zao zinabadilika kutwa basi hamna maana a ndoa watu wazae tu , hili la kuondoa Taasisi ndoa ndio lengo la mzungu.
 
Dah!... masikini huyo mtoto anaadhibiwa kwa kosa lisilomuhusu.
Nadhani ni namna ya kuregulate kupunguza michepuko, wakati Babu zetu walikuwa na wake wa kutosha ila saizi tunalazimishwa mke mmoja at the same time ushoga inaonekana ni haki ya faragha ya mtu ila kuoa mke zaidi ya mmoja ni dhambi
 
The issues born out of wedlock are innocent creatures. There is a Swahili phraseology "kitanda hakizai haramu' which literally means there are no bastard children. But there are bastard parents. The child is not culpable for its parents' shortComings nor can he or choose the situation they are born into. Thus, it is not a child's fault being born in the situation. Children born out of wedlock are the biological children just like those born within the matrimonial home. They are entitled to equal shares of their common father with fellow siblings.

"Mtoa mada jibu unalo litaka hilo hapo. Rejea kesi ya Judith Patrick, probate and administration cause No. 50 of 2016, High Court, Dar es salaam District Registry"
 
Habari za uzima, naamini mmeamka salama, wale walio na magonjwa Allah akawape wepesi na mlio hospitali Mungu akawape wepesi pia mtoke huko, sio kuzuri na hakuzoeleki.

Rejea kichwa cha habari hapo juu, wenye ufahamu - mzazi wa kiume akifa watoto wa nje kwa dini ya kikristo wanarithi?
Hilobswali ni gumubsa jwa wanaojiita wakristo. Kwa kuwa hawafati sheria za biblia, wanafata sheria zilizotungwa na watu.
 
Zinatumika nchini kwako ila zina makosa kibao, sikiliza ndugu yangu mbona wanakataa kuweka pesa chafu kweny mzunguo wanasema ni kutakatisha pesa (money laundering) .

Ukichambua sheria zao zinabadilika kutwa basi hamna maana a ndoa watu wazae tu , hili la kuondoa Taasisi ndoa ndio lengo la mzungu.
Mkuu ukijihamishia mawazo kwenye uhalali wa ndoa utapata utata sana, baki kwenye haki za mtoto.

Mtoto hana uhusiano na "dhambi" za wazazi, ndio maana anapozaliwa hata wakristo tutamwita ni Malaika.

Kuzaliwa nje ya ndoa hakumfanyi asiwe na baba/mama!

People just need to plan their estates well!
 
Hata pesa hazina tatizo ila ukitakatisha hazifai kutumia, sijasema mtoto ana dhambi ila hana uhalali kwa baba yake ni mama tu , mtoto hamna njia utamtakasa akawa halali maana umempata kwa zinaa
 
Hata pesa hazina tatizo ila ukitakatisha hazifai kutumia, sijasema mtoto ana dhambi ila hana uhalali kwa baba yake ni mama tu , mtoto hamna njia utamtakasa akawa halali maana umempata kwa zinaa
Ndio hivyo sasa huna la kufanya, tutawatetea kwa mujibu wa sheria zilizopo!
Tukiwapuuza wataishia kuwa chokoraa, wakatili na kuongeza daraja la umaskini!

Hatuwezi acha watu wazae hovyo halafu wasiwe responsible for their own acts, mali za mzazi husika lazima zimguse mtoto wake.
 
Ishmael hakupewa chochote na Ibrahim zaidi ya kile kibuyu cha maji ya kunywa.

Tuliona jinsi Mungu alivyokubaliana na msimamo wa Sara (Mwanzo 21:9-12).

Vile vile tuliona jinsi ambavyo Yeftha alipokosa urithi kwa sababu alikuwa ni mtoto wa nje ya ndoa (Waamuzi 11:1-3).

Sasa hapo inabidi tu ubinadamu utumike na kwamba watoto wote ni sawa.
 
Ndio hivyo sasa huna la kufanya, tutawatetea kwa mujibu wa sheria zilizopo!
Tukiwapuuza wataishia kuwa chokoraa, wakatili na kuongeza daraja la umaskini!

Hatuwezi acha watu wazae hovyo halafu wasiwe responsible for their own acts, mali za mzazi husika lazima zimguse mtoto wake.
Sasa ndi unatakiwa kusoma ili ujue unaweza kufanya mtoto wakom apate haki kwa mujibu wa mafundisho. kil tatizo lina mbadala.

unatakiwa kumpatia sehemu ya mali zako ukiwa hai mapema ukishajua ulifanya hivyo hata kuwaandika kabisa kuna nafasi ya wosia ...Katika uislamu wosia ni sehemu ya zaida ila hata usipoandika mali zitagawanywa kwa mujibu wa sheria na haki zao watapata wale watto wa ndoa .

Bado unawajibu wa kumtunza kama mwanao , kumsomesha sio batili .
 
Uandike wosia, usiandike wosia, umgawie kabla au la; wewe jua tu tunajukumu la kulinda haki ya mtoto kwenye mali za marehemu mzazi wake!
 
Uandike wosia, usiandike wosia, umgawie kabla au la; wewe jua tu tunajukumu la kulinda haki ya mtoto kwenye mali za marehemu mzazi wake!
Mtoto sio halali anaweza kupewa na ndugu ila sio mlengwa , miongoni mwa wenzie wanaweza kumpa kwa kuridhia .
 
Vipi kuhusu Baba nae anaweza kupata urithi kwa mtoto wa nje ya ndoa Kama akifa..
 
Habari za uzima, naamini mmeamka salama, wale walio na magonjwa Allah akawape wepesi na mlio hospitali Mungu akawape wepesi pia mtoke huko, sio kuzuri na hakuzoeleki.

Rejea kichwa cha habari hapo juu, wenye ufahamu - mzazi wa kiume akifa watoto wa nje kwa dini ya kikristo wanarithi?
Endesheni mambo kwa kadiri ya ufahamu wenu, acheni kurejelea mambo ya kidini kwenye mambo nyeti kama mustakabali wa mtoto.
Awe kazaliwa ndani ama nje, huyo ni mtoto. Ukristo ama Uislamu ukiingia hapo ili kuamua hatima ya mtoto, basi ni kwa sababu wazazi wake ni WAPUMBAVU.

Asante.
 
Back
Top Bottom