Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
- Thread starter
- #101
Kuna vitu vipo wide na unaweza wewe tafsiri yako binafsi ikawa tofauti na tafsiri ya mtu mwingine; hence mtu anapokuuliza wewe kwa muktadha wako kwenye context hii unamaanisha nini ili tuwe kwenye same page na kuweza kujadili kilichopo kwenye hio page..., Sasa hapa kwenye hii paragraph umetoa issue za mimi kuajiri / kuajiriwa na kujua Sheria..., Inawezekana nimeajiriwa katika Msikiti hence kwangu mimi Mwanaume ndio kichwa hata iweje lazima nitoe huduma (hio ipo kwenye Imani wala siwezi kuibadilisha)....
Sasa sababu haujajibu nina-assume unamaanisha Sheria ambayo iwe sheria lazima iwe na penalty kwa mtu kuivunja kutokana na Misingi watu waliyojiwekea.., au niende further unamaanisha Kifungu Na. 63 cha Sheria ya Ndoa...... Kwa Maneno yasiyo Rasmi.....
Now kama hicho ndicho unachomaanisha..., suala ni kwamba kila case inaweza ikatatuliwa kutokana na mazingira yake..., sidhani kama Samia anaweza kumshitaki mume wake eti hajamnunulia Nyumba, au Kumpa Chakula (sababu hana uhaba huo)..., LAKINI mfano keshokutwa SAMIA (kwa kutokutumia IMANI yao bali Sheria za Nchi) akiamua kudai Talaka yake anaweza kusema huyu Bwana hatoi Huduma yoyote hivyo mimi kuendelea kuwa mke wake na kunizibia opportunity za kuwa na Bwana mwingine wakati yeye hatimizi / hachangii wellbeing yangu kwa lolote nataka uhuru wangu na aniache... Kwahio hapo atakuwa ana point... KULIKO kufuta hiki kipengele huenda ikatokea watu kuoa mtaa mzima (hence kuwazibia uhuru wao kwamba ni wake zao) wakati hawachangii lolote kwa kumfunga huyu so called mke...
Issue ya kukopa kwa Dhamana ya Mume: Sheria hii imewekwa kutokana na hii scenario
Sasa mfano watoto wanataka kwenda shule na mume ametoroka (kweli mama asiweke rehani gari aliloacha mume wake hapo kwenye garage)? lakini nina uhakika kama huyu Mama (SAMIA) atafanya hivyo kwa kuuza nyumba ya mume wake ili anunue lipstick Mahakama haiwezi kusema ni sawa kilichofanyika...; Ingawa akisema huyu Bwana hana mchango wowote kila mtu achukue hamsini zake anaweza kuweka kigezo cha kutokumuhudumia kama sababu ya kuachana nae....
Kumbe ulichokuwa unauliza ulikuwa unakielewa. Vizuri.
Unafikiri kwa nini sheria ya kumhudumia Mwanamke iliwekwa?