Sheria ya kusoma shule kuu ya sheria yaondolewa

Ujinga kabisa, Bila shaka imeondolewa Kwa ajili tu ya TLS ya Mwabukusi.

Yaan ili mradi umalize Shahada yako chuo Cha matopeni na GPA yako ya 3.0, unajiita mwanasheria Msomi na wewe unakua na muhuri wako, unaanza kula Hela za watu.
 
Lini mtu asiye wakili hakuweza ajiriwa ktk utumishi wa umma? Utakua mtoto wewe.
 
The amendment therein haizungumzii uliyopost mkuu, ukitaka kuwa mwanasheria njia bado ni ile ile. Vijana mlio vyuoni someni kama hakuna kesho, Utajuaje kuexecute or present critical cases kotini usipojua vitendo. LST ndiyo kichungi, jikaze na utafaulu tu, ile shule ni simple sana kwa mtu aliyemakinika.
 

Kwamba uhalisia wako umejengwa kwenye kudhania?



Bure kabisa!
 

Kwani wewe ni nani kujipa u halali wa kuhalalisha lolote?

Wapi nani alikwambia anataka mtihani nje ya utaratibu?

Au hata hiyo mitihani itokeje nje ya utaratibu?

Mada hata umeielewa tokea kwenye kijiwe cha boda boda pale?
 
Ww ni bushlawyer au bushshamba? Hv unaelewa kilichobadilishwa!?
 

Ulichoandika hapa unamaanisha kufaulu LST hakuna formula.

Ni mwendo wa ku bet au kuangaliana usoni?

Hilo ni kinyume cha utaratibu na ndiyo maana kuna TCU kwa ajili ya harmonization.

Elimu ya juu siyo Simba na Yanga ndugu!
 
Hiko ndio kilio kwa nchi yetu kuwa sehemu zote tupate aina ya watu walioko LST. Hawa wajinga wachache huwa hawakosekani uzuri hupuuzwa
 
Ulichoandika hapa unamaanisha kufaulu LST hakuna formula.

Ni mwendo wa ku bet au kuangalia a usoni.

Hilo ni kinyume cha utaratibu na ndiyo maana kuna TCU kwa ajili ya harmonization.

Elimu ya juu siyo Simba na Yanga ndugu!
Sio kubet bali kuonyesha kuwa ukiwa hapo wapo serious hakuna kuangalia mtu usoni. Utafaulu kama utakua vizuri, na utafeli kama utakua hovyo.
Ni sawa na TO wa advance ategemee akienda chuo kwa mazingira yoyote atafaulu tu, hiyo haipo
Ndio maana wapo TO ambao wamewahi ku-disco University
Na wapo waliopata Div 2 or 3 lakini wakaondoka na first class.
 

TO ndiyo kina nani ndugu?

Hata hivyo tuko busy na mliowateka.

Samahani lakini

Cc: Stroke fyi
 
Bora wamefuta kwa sababu watoto wa masikini walikosa
ajira kwa kulazimishwa kutafuta postgraduate diploma in Law wakati
amesha soma L.L.B 4 years.
Hizo ni sheria tu, na sheria nyingi za nchi yetu hazitekelezwi. Sioni kama kuna taasisi itamuona mtu amefaulu hapo shule ya sheria imuache na imchukue mtu kwenye shahada ya sheria ambayo kuipata kwa sasa huko vyuoni ni rahisi sana hata kwa kufanyiana assignments hata kama haitajiki kwa kazi za uwakili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…