Enyi wabunge wetu,tunaowachagua kwa kura zetu,tunaomba hili lisipite.Sheria hii inawalenga hata nyinyi na watu wengine nyeti serikalini ambao kwa uzalendo wao kwa taifa,na kukerwa na maovu ya wenzao serikalini, wanaamua kutumia fake ID'S even sometimes fake names and profile details ili kuizindua jamii.
Sote tu mashahidi mtandao kama JF umechangia kiasi gani ishu kama za escrow etc. Serikali yenyewe inapata habari nyingi humu na kuelewa mitazamo ya watu juu ya mambo mbalimbali, jambo linalowasaidia kufanya maamuzi sahihi. Juzi juzi tu hapa JF kulitolewa information na ID fulani kuhusu uwepo wa magari yanayofanana namba za usajili,siku chache baadae tukasikia TRA ikitoa tangazo kuita wahusika wakajieleze. Tayari raia huyu mwema ametoa taarifa ambayo dola ikifanyia kazi itaokoa mamilioni ya kodi zinazokwepwa.
Tena ni suala lenye faida kwa serikali,wala mtoa mada kama ni raia wa kawaida hafaidiki na chochote binafsi. Sasa mtu ukijua JF inaweza kubanwa kutoa IP address yako, mnafikiri watu watatuma vitu vya aina hii? Mmefikiria upande wa ufisadi unaowaumizeni tu, hamjafikiri kuwa nyie ndio wanufaika wakubwa wa info zilizomo humu. Mimi mwananchi wa kawaida utanibana nitakaa kimya,but remember, watoaji wakubwa wa habari nyeti mitandaoni ni nyie nyie watu wa serikali kwa kutoridhika na mambo huko juu. Hawa hamuwawezi,mkiwabana wasitoe nyongo zao humu,they'll give you a direct fight, wala hawatakubali.
Kupenda mabadiliko pale asiporidhika ni nature ya binadamu.You can't fight nature,you have to live with it.The only way ni kumridhisha.Kama wananchi hawaridhiki na uongozi wao, mabadiliko ni lazima. Hata mfungie hadi tv stations,we will find another way to communicate and give you a fight. Hii fight hamtaikwepa kwa kubana media, itakuwepo tu, suala si mimi kumiliki pc yenye net,bali suala ni mimi kurudi nyumbani na kukuta wanangu wana njaa huku sina hela,na huku natumikia kazi kikamilifu bila kupata ninachostahili.Suala ni kuniridhisha,nitulie. Vita iko mioyoni mwetu, sio kwenye server za JF.
Open up your mind nyinyi viongozi vipofu msiojua maamuzi sahihi ni yepi.Always mnarukia kuficha matatizo badala ya kutibu.Wabunge kataeni huu mswada kwa manufaa yenu wenyewe. Watanzania wenzangu October tusichague mgombea yeyote mwenye any connection na uongozi huu wa awamu ya nne. Naukataa sana utawala huu, unaiharibu nchi sana, haufai, si rais, waziri, rc, e.t.c yaani vitu ambavyo sijawahi kuvifikiria vitatokea, vinatokea kwenye awamu hii. Hivi hakuna think tanks huko serikalini? Mbona serikali hii ya kienyeji enyeji hivi? Hekima ya kuona mbali iko wapi?
Jamani, hivi watz tulichaguaje hawa watu? Jesus Christ!