Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Hivi hizi sheria kuna watu maalum wanatungiwa au na hawa wanaosema ndiooooo. Pia wamo?. Maana wanasema ndio bila fikra yoyote! Tindu Lisu na Mnyika hakika ni wawakilishi wa Wananchi.
 
Moja ya Vipengele vinampa uwezo Police yoyote kuchukua Simu ya Mkeo au yako au ya Mtoto wako na Kuipekua.

Hii hoja moja inatosha kuonyesha Wabunge wa CCM hawako sawa.

Dah! Hii nchi imerogwa? Hivi hili Hawa ndio watunga sheria wetu?


Hivi ukikataa inakuwaje?
 
Moja ya Vipengele vinampa uwezo Police yoyote kuchukua Simu ya Mkeo au yako au ya Mtoto wako na Kuipekua.

Hii hoja moja inatosha kuonyesha Wabunge wa CCM hawako sawa.

Dah! Hii nchi imerogwa? Hivi hili Hawa ndio watunga sheria wetu?
...........CCM ni chama changu, na-declare interest, lakini tuna wabunge makanjanja wanasubiri kusema ndiyoooooooooo ama siyoooooooo, tena bila hata aibu, mfano, mswada wa Makamba na Boss wake, wachangiaji ni Mwanasheria Mkuu, Tundu Lissu, Mnyika, na Mbarawa/Makamba wao wanasubiri serikali inahitaji ndiyo ama siyo, sijui hata wanafanya nini, shame on them!!!!!!!!! kufikiri kwa tumbo kuna gharama kubwa kuliko fikra ingine yeyote
 
Hii sheria kandamizi ni kwa ajili ya jf tu na utawala unaotumia mbinu hizi kujihalalishia kuendelea kuwepo basi ni bora wakaondoka maana wataadhibiwa tu. Kuiba ni kosa lkn miaka yote tunaiba,kuua ni kosa lkn ndugu zetu albino wanauawa kila siku ingawa zijaona wakilitungia sheria kali. Hata hili tutapambana nao na wakitaka wafunge huduma za internet pumbavu zao wote. Mods sitaki mtoe taarifa zangu kwa hawa wahuni
 
Naamini kama muswada huu utapita na kutumika baada ya miaka 3 au 5 basi watumiaji wengi wa mitandao watakuwa magerezani au kutakiwa kulipa faini isiyo na ukomo....umekosewa na kuondoa uhuru wa kutoa maoni kwa mabaya na badala yake tuwe watu wa kusifia.

Katika suala la nguvu waliyopewa askari itakuwa tatizo sana maana tumeona lile tamko la waziri mkuu hata kama halikuwekwa katika maandishi na kuridhiwa na bunge lakini kilichotokea kila mmoja wetu ameshudia. Je kwa hii walopewa ya moja kwa moja nadhani wataitumia kinyume na ilivyotamkwa.

Rai yangu ni kwamba huu muswada ufanyiwe marekebisho kwa kuweka na kinga pia kwa watumiaji wa mitandao
 
Ni kweli mkuu, mitandao imekuwa na uongo na upotoshaji sana,

Nashindwa kumuelewa mleta mada anaposema sheria kama hii haiendan na demokrasia. Sijui ni demokrasia ipi inayoruhusu uongo na upotoshaji.

Usiisapoti huu muswada kwa kuangalia kipengele kimoja....mfano sidhani kama hili jina unalotumia humu ni la kwako bhasi uko hatiani kwa mujibu wa sheria hii
 
Kuna mambo mengi yanaitaj msaada kama vile suala la mauaji ya albino,,na kama kuhusu porn mnaogopa watoto kwan n nan amempa hcho kfaa cha internat kama s ww.
 
Yote haya yanafanyika ili kudhibiti Uhuru wa habari ktk hichi kipindi cha uchaguzi.......tutaona mengi mwaka huu
 
Tarehe 19 ya mwezi wa januari mwaka huu nilijaribu kuanzisha mjadala kwa nia ya kujipima ikiwa watanzania tunahitaji mabadiliko ya kisheria zinazohusu mitandao,

Sheria gani zifanyiwe mabadiliko na gani zisifanyike katika masuala yanayohusu matumizi ya mtandao kwa nia ya kuwashawishi watunga sera watuwekee sheria itakayokubalika na jamii nzima bila kuwepo na malalamiko lalamiko kutoka upande wowote... kwa kichwa cha habari; Topic: Sheria ya
kuruhusu udukuzi
haiko mbali Tanzania
tumejiandaaje ? sikupata wachangiaji wa kuendeleza mjadala...au sikueleweka....? Hatukujiandaa vyema na muswada tayari uko bungeni kwa hati ya dharura sasa tumeanza kulalamika lalamika

Tuwe na tabia ya kusoma na kusikiliza yanayoendelea kwa wenzetu na majirani zetu tanzania siyo kisiwa, yanayojiri kwa wenzetu yanatuhusu kwa njia moja ama nyingine..
 
mkuu kerubi,umenifurahisha sana kwa kweli.
Hawa jamaa kama huo uchafu utapitishwa na kuwa sheria,wajue kabisa ndio watakuwa wanamwagia petroli kwenye moto,maana kama ulivyoelezea,kuwa "ghost" kwenye mtandao ni rahisi sana,na tutafundishana humu humu,na hapo sasa ndio tutaweka madudu yote hadharani.

kama kawa mkuu.cha muhimu ni umakini wa hali ya juu.kama Osama vile.Usifanye activity yoyote kwenye laptop yako maalum ambayo itafanana na activities unazofanya kwenye vifaa vyako vya kawaida kiasi cha wao kuunga dots wakahisi ni mtu mmoja.Yaani we ukiwasha ile laptop yetu ni moja kwa moja JF,unatupia makombora,unaamsha fasta,tunaita hit and hide.Halafu unapima uzito wa kombora.Ukiona una makombora mazito mno kama Yericko,basi kwanza ile laptop yetu inatakiwa iwashwe eneo ambalo hujazoeleka.Unakwenda beach unatulia,unatupia katyusha,unamtumia invisible pm kumwambia "wakikuomba wape,usiingie matatizoni".ukimaliza unachomoa battery,ikibidi hata ile secondary kule ndani(CMOS) nayo unachomoa,unarudi nyumbani,unatulia na feature phone yako unatupia jicho la mbaali.na ukinunua ile laptop yetu chukua ya zamani yenye teknolojia dhaifu,no wifi,no bluetooth,etc maana hayo mawifi yana tabia ya kuexpose MAC address ingawa ni short range.si unajua haya mavifaa ya kisasa,more technology more vulnerability.labda wawe wanafuta.naongea purposely kuwatumia ujumbe hao jamaa kwamba hao watu wanaolenga kuwadhibiti wako kama wao.Siamini mtu kama Yericko haelewi hatari aliyo nayo.Lazima kajipanga.Huyo Gwajima tu tunaambiwa walikuwa wanaona simu yake kwenye mitambo ila wakifika located area hayupo.Hao watu wanaowalenga ambao wanakuja humu na kupakua mambo mazito,wengine ni wenzao huko juu wanajua how to escape.Kama mie wa mtaani tu najua haya,what about them?wataishia kusinzia kwenye keyboard au kukamata wapiga puli kwa picha za x!watu wanaikwepa NSA,itakuwa cyber crime unit ya polisi tz?!kalagabaho!@Yericko Nyerere mmemkosa kabsaa,niwaambieni.saa hizi keshatafuta "mshauri" wake wa masuala ya "kielektroniki".
 
Naona sasa Internet cafes zitashamiri mijini! Ukirusha mzigo huko unarudi kwenye handset yako kuchangia na kusoma comments.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ndiko tulikofika? All Assad na Gadaf walifanya hivyo, lakini hali ya kibinadamu ni ngumu na ya hatari sana,

Uchina na Urusi walijaribu havyo lakini utandaridhi vimewashinda,

Sasa kwetu si watafunga kila wanayemhisi tu bila ushahidi?
NA HAPO NDIPO PENYE MAtatizo
wengi wataumizwa bila hatia
 
Naona sasa Internet cafes zitashamiri mijini! Ukirusha mzigo huko unarudi kwenye handset yako kuchangia na kusoma comments.

Mimi nafikiri wengi hamkupata wasaha wa kusikiliza mjadala wa muswada husika hapo jana.

Huu muswada haumgusi mtumiaji huduma tuu bali hata mtoa huduma ina maana hata wamiliki wa blogs na websites watakuwa na wajibu na watawajibika kabisa kwa kutumia kwako internet cafe kutakuokoa wewe kutojulikana kama habari itakuwa ya uongo au ya kuchafua mtu utaiweka jf matatani kwa hiyo tunawajibu wa kuzingatia..

Mimi nawaomba JamiiForums Invisible Moderator watu wekee version mpya ya cyber crime act kila jukwaa maana hii.tunayo jadili ilifanyiwa marekebisho mengi sana jana kwa hiyo bila shaka baada ya jana itakuwa ilisha chapishwa upya na ni vyema moderation ya majukwaa hasa la siasa na habari mchanganyiko ikabadilika na wakaongeza ukali zaidi maana jf ndio itakuwa ya kwanza kuangaliwa kama sheria zinatekelezwa na mifano inaweza kuanzia jf kabisa...
Hatuna jinsi tena inabidi tufate tuu sheria iliyopo na ni wazi kuna hitajika mabadiliko kwenye sheria za jf ili kuendana na sheria za Cyber crime.
Wala tusiogope maana vitakavyo athiri jf ni uzushi,matusi.
Na watu wanatakiwa kujua katika hili jf ndio itaathirika kuliko wahusika
 
Last edited by a moderator:
Nielekezeni namna ya kujitoa jamii forums,ili nisishawishike siku moja nikapost kitu alafu wakanifanyizia
 
Back
Top Bottom