Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
SHERIA YA MALEZI ISEME; KAMA MWANAMKE HAWEZI KULEA MTOTO AMPELEKE KWA BABA YAKE, HIYO NDIO MANTIKI NA SIO VINGINEVYO.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Unajua kuna Wakati mpaka unashangaa wanaotunga hizi sheria uwezo wao wa kufikiri ukoje nazungumzia hizi sheria za mahusiano hasa ya Mume na Mke, na Baadhi ya sheria za ndoa na Familia. Unajiuliza unakosa majibu.
Unajua MTU anaweza kuwa na madigrii ya kutosha ya sheria lakini kichwani akawa hajui hata maana ya Sheria, yaani yeye sio mwanasheria. Yeye kasoma soma tuu na kukariri kama kasuku. Haya ndio Matokeo yake.
Ukitaka kujua MTU huyu ni mwanasheria basi angalia Facts zake, Sifa kuu ya mwanasheria ni kujenga Facts.
Sheria ya kumfunga mtu ati kisa ametelekeza mtoto au kumlipisha faini imetungwa Kwa hisia zisizozingatia mantiki.
Watungaji wa sheria lazima waelewe kuwa sheria zinatungwa ili kuifanya jamii iwe bora na Kwa maslahi ya kizazi kijacho na sio vinginevyo. Sasa unapotunga sheria Kwa Hisia bila kujali nini kitatokea ni kuleta matatizo ndani ya jamii. Na Hilo tumeshaanza kulishuhudia.
Watunga Sheria wanapaswa wajue kuwa linapokuja swala la mambo ya Uzazi;
I) Mhusika Mkuu ni Mwanamke.
ii) Mwanamke ndiye anaamua abebe mimba au asibebe.
iii) Mwanamke ndiye mwenye Kalenda,
iv) Mwanamke ndiye anaamua Azae au asizae.
Sheria ya kumfunga au kumlipisha faini mwanaume aliyetelekeza Watoto ni sheria isiyo na mantiki Kwa sababu;
1. Haijazingatia Haki za Pande zote mbili, Ila imeegemea upande mmoja.
Haielezi je ni vipi Mwanamke akitelekeza watoto atapewa adhabu gani,
2. Sheria hiyo ingekuwa na mantiki kama ingeeleza upatikanaji wa mtoto lakini mantiki ya sheria hiyo inaruhusu mtoto kupatikana Kwa Njia zozote bila kujali ni Njia za maadili au zisiwe na Maadili. Kumaanisha Sheria hiyo haitambui kitu kiitwacho maadili, hivyo hata hiyo sheria haiwezi kuwa ya maadili.
Sheria ambayo msingi wake au chimbuko lake sio maadili haiwezi kuwa yamaadili na haiwezi kutatua Jambo la kimaadili. Hiyo hauhitaji kwenda darasani kusoma.
3. Sheria hiyo ili iwe ya Haki lazima sheria zingine ziruhusiwe ambazo sio sheria za Maadili. Kama nilivyosema hapo juu.
Sheria ambazo zitatakiwa kuingizwa ili kumpa Mwanaume Haki ni pamoja na hizi;
I) iruhusiwe biashara ya Ukahaba na sheria zitungwe zitakazolinda Haki za makahaba na Wateja wao, mfano Mteja(mwanaume) akinunua Kahaba atanunua Huduma ya ngono tuu na sio vinginevyo, na kama itatokea mimba basi mimba hiyo haitakuwa sehemu ya makubaliano ya biashara iliyofanyika. Na mteja hatakuwa responsible na mimba na mtoto huyo atakayezaliwa.
ii) Iruhusiwe mimba kutolewa. Sheria zitungwe ili kuruhusu na kuratibu utoaji WA mimba hasa zilizoingia pasipo ridhaa ya mmoja wa waliopo kwenye mahusiano.
Ili mtoto atakapozaliwa asije akakosa Haki zake kisa mmoja wa wazazi wake hakutaka na wala Hana shida na huyo Mtoto.
Lazima yawepo makubaliano baina ya Mwanamke na Mwanaume kuwa tunahitaji mtoto, na wote waridhie. Ndipo mtoto apatikane.
Kisha yeyote atakaye vunja makubaliano hayo ndiye anapaswa kuchukuliwa hatua Kali za kinidhamu Kwa maslahi ya mtoto.
Wenye Akili zao wakasema, makubaliano hayo yawe ndani ya Ndoa, ili kuwaleta Mwanamke na Mwanaume kuishi pamoja, kwaajili ya kufanya majukumu ya kutunza familia na hapa nazungumzia Watoto mpaka umri watakaojiweza.
Wenye Akili waliotutangulia ambao hawakusoma sheria Ila walizaliwa na sheria wakasema, Kwa vile mwanaume ndiye mwenye familia basi itabidi apewe majukumu makubwa na kumpa mamlaka makubwa ili kumpa uwezo wa kuiendesha familia. Hivyo ni jukumu la mwanaume kumtunza Mkewe na watoto. Ni Sawa kabisa.
Lakini wakatokea waliokariri sheria Kwa kusoma, wao wakaja na sheria zinazoleta usawa ndani ya familia na kusahau kuwa sheria unapoleta usawa basi hata majukumu na wajibu vitapaswa kuwa Sawa. Mfano ukishaleta usawa ndani ya familia automatically umempunguzia mwanaume majukumu Kwa kuya- neutralize kisha umemuongezea Mwanamke majukumu hivyo wote watakuwa Sawa, matokeo yake ni kuwa Ile sheria ya mwanaume anapaswa kuhudumia familia yaani MKE na watoto itakuwa imekufa.
Kwa sababu wakariri sheria Hawana wajualo, watakuwa wanamlazimisha Mwanaume ahudumie MKE na watoto Wakati huohuo wamempunguzia mamlaka na uwezo wake.
Taikon kama Mwanasheria wa asili bila ya kuyasomea, naelewa kuwa lengo la baadhi ya sheria labda ni kutengeneza namna ya kuwasaidia Wanawake kuondokana na madhila, na manyanyaso au mateso wayapatayo, lakini namna Bora ya kuwasaidia Wanawake sio kumkandamiza mwanaume. Huko ni kuiharibu jamii.
Watu kama ustawi wa jamii ambao kimsingi lazima wawe na taaluma ya sheria lazima mjiulize, hivi sheria za Haki za mtoto au Mwanamke zimelinda Haki za mwanaume, je matatizo yanapungua au yanaongezeka? Ikiwa yanaongezeka tatizo ni nini?
Sheria zisipokuwa za Haki matatizo ndani ya jamii lazima yazidi, na hauwezi kutumia nguvu kuondoa matatizo ndani ya jamii pasipo kujua kiini cha matatizo.
Mfano unaposema labda tatizo ni ukosefu wa Elimu, je ni kweli wenye Elimu hasa za sheria wao hawasumbuliwi na mambo haya? Jibu ni hapana. Ingawaje Elimu ni muhimu lakini lazima iwe bayana kuwa hata Elimu ingetolewa lakini kama hakuna sheria za Haki matatizo lazima yazidi kuongezeka.
Unapomfunga Kijana au Mwanaume aliyetelekeza Mtoto, umejiuliza haya;
I) Je kulikuwa na makubaliano yoyote ya mtoto kupatikana baina ya Wahusika hao Wawili?
Kama makubaliano Yao yalikuwa kustareheshena na Mwanaume hakuwa na Mpango kutoa mimba na Kupata mtoto, kosa la mwanaume ni lipi?
Oooh! Ni kufanya tendo bila kutumia Kinga. Vizuri, kama Kinga zinaruhusiwa iweje Abortion isiruhusiwe?
Lengo kuu la kinga ni lipi na linalotofautiana na Abortion?
Zipo Njia nyingi za kinga ikiwepo Kalenda, ikiwa mwanaume hafanyi tendo la Ndoa na mtoto Mdogo, kumaanisha Mwanamke yeyote ni jukumu lake kujua Mzunguko wake, iweje kosa liwe la mwanaume?
Tuacheni kutunga visheria vya kinafiki nafiki na vyenye upendeleo.
Mwanamke kama hajaolewa asifanye Ngono, na kama atafanya lolote litakalotokea hasa mimba litakuwa juu yake
Ikiwa mwanaume atamdanganya anataka mtoto Kutoka kwake, basi iundwe sheria ya kuandikishana ili pawepo ushahidi WA Jambo hilo. Ili kulinda Haki za mtoto atakayezaliwa.
Vinginevyo, sheria ya Kutoa mimba haiepukiki ni suala la Muda.
Kuna MTU atasema sio maadili ya muafrika, kwani sheria ya kumfunga aliyetelekeza Mtoto ndio maadili ya muafrika?
MTU anabeba mimba kimakusudi bila kumjulisha mwenzake, ninyi hamuoni kama hiyo sio Sawa Kwa sababu inakandamiza Haki za mwanaume na bila Shaka yoyote mtoto akizaliwa lazima aonje joto la jiwe.
Mnakalia mawazo ya mepesi kama Watu wasio na Akili, ATI kwani mtoto anakosa gani, Nani kasema mtoto anakosa, Mtoto kama Hana kosa huyo anayeonekana anaowajibu wa kumtunza mtoto si mumpe huyo mtoto amlee mwenyewe kama mmeshaona ni mtoto wake na nijukumu lake kumlea.
Sheria ya malezi ikiwa itaona shida kupitisha sheria za biashara za ukahaba na utoaji WA mimba basi sheria rahisi ni Mwanamke akizaa mtoto, kisha ikatokea wakaachana, ikiwa Mwanamke ataona Hana uwezo wa kumtunza mtoto amuachie mtoto Baba WA mtoto. Rahisi Sana. Lakini mnataka mambo yawe mengi ili nafasi zenu za kazi zionekane.
Hakuna Baba atakayetaka matumizi Kwa Mama wa mtoto, na wala hakuna Baba atakayemzuia Mama kuonana na mwanaye. Lakini ni mara ngapi Wanawake wanapiga mayowe kuhusu kuomba matumizi Kwa Baba WA watoto, na kuwanyima wababa kuona Watoto wao?
Hamuoni hiyo Gap? Je hamjui namna ya kuliziba Hilo Gap?
Matokeo yake mnaliongeza Gap ATA Kwa kumfunga MTU au kumlipisha Faini. 😀😀 Kuna mambo yanachekesha Sana.
Lengo la sheria ni kutatua matatizo ndani ya jamii na sio kuongeza,
Mwanaume tuu akipelekwa polisi au Huko ustawi wa jamii anavunja uhusiano hata uliobakia na mzazi mwenza sembuse kumfunga au kumlipisha hayo mafaini.
Ni Wakati WA Kutumia weledi na hekima katika kuyaendea haya mambo.
Njia nyepesi ni umezaa, jibu ni Ndio.
Unaweza kumtunza mwanao, Hapana,
Basi mpeleke mtoto Kwa Baba yake, simple. Ukitaka kwenda kumuona utamuona au mtoto ataletwa kwako.
Umezaa, Ndio, unaweza kumtunza mwanao, Ndio, basi lea mwanao.
Maelezo haya ni kwa Muktadha wa Watu ambao hawakufunga Ndoa.
Kwa wale wa kwenye Ndoa,
Kwanza Sisi wanasheria WA asili tunajua ndoa sio ya kila MTU. Hivyo waliotayari kuingia kwenye Ndoa wawekewe sheria zao ambazo haziingiliani na wale wasio na Ndoa.
Ndoa itahitaji Watu wenye Upendo, uaminifu na Akili.
Kukosa kimoja Kati ya hivyo vitatu hakuna Ndoa hapo.
Acha nipumzike
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam