Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Kuna mwenzio alienda na suala kama lako kwa mchungaji akiomba avunje ndoa! mchungaji hakuwa na tatizo akawakubalia! akawaambia sawa njooni tuombe ili ndoa ivunjike, akaanza kusali kuomba kifo kimchukue mmoja kati ya wanandoa! kumaliza sala akajikuta amebaki mwenyewe jamaa wamesepa!
 
Jee, ni taratibu zipi za kufuata ili mwanandoa aliyefunga ndoa ya Kikristo kanisani aweze kuivunja ndoa hiyo kimahakama au kisheria?

Wataalamu wa Sheria tafadhali naomba mnifahamishe. Natanguliza shukrani.

Fanza hivi

1. Peleka malalamiko yako kwenye Baraza la Usuluishi linalotambulika kisheria (Ofisi ya ustawi wa Jamii, Kiongozi wa Kanisa mwenye mamlaka ya kufungisha ndoa)

2. Baraza/Kiongozi husika atawasikiliza wanandoa wote na kuona kama anaweza kuwashauri ili msamehane na kuendelea kuishi pamoja. Kutengana kisheria/makubaliano huwa ni mbadala katika hili.

3. Endapo usuluishi utashindikana Baraza/Kiongozi husika atakupatia Barua/Hati ya kushindwa kusuluishwa. Barua/Hati hiyo itaandikwa ikielekekzwa kupelekwa katika Mahakama husika.

4. Ukifika Mahakamani unatakiwa kulipia gharama za kufungua Kesi ya Ndoa ili kuomba TALAKA na Kuvunja Ndoa yenu rasmi kisheria ukipenda na mgawanyo wa mali za ndoa plus matunzo ya watoto kama wapo. Kumbuka kuambatanisha Madai yako na Cheti cha ndoa

5. Mahakama itasajili Kesi yako ya Madai ya Talaka na kukupa Hati ya kumwita Mkeo Mahakamani ili kujibu madai dhidi yake.

Angalizo: Sababu kubwa ya kuvunja ndoa na kutoa Talaka huwa ni KUWEZA KUITHIBITISHIA MAHAKAMA KUAMINI KUWA NDOA YAKO IMEVUNJIKA KIASI AMBACHO HAIWEZI KUREKEBISHIKA TENA.

Aidha Mahakama uangalia mambo muhimu/vigezo vifuatavyo ili kujiridhisha

(a) Ugoni
(b) Ukatili
(c) Kulawiti
(d) Kichaa
(e) Kuzembea wajibu kwa makusudi
(f) Uasi/Utoro
(g) Kutengana - kusiko pungua miaka 3
(h) Kifungo
(i) Dhana ya Kifo
(j) Tofauti za Dini/Kubadili Dini

Anyway huo ndo ushauri wangu faster lakini kwanini uvunje ndoa bana, gangamala maisha sio mchezo etiii.
 
mkuu kama kwel we ni muumini bora wa ndoa za kikisto kabla cjakushauri hebu jaribu kueleza tatizo la msingi linalokvafanya utake kuvunja ndo.a

Tatizo kubwa ni mke kabadili kabisa muelekeo kiimani kitu ambacho kinakingana na ile imani iliyokuwapo awali wakati wa kutoa kiapo cha ndoa kanisani. Licha ya kuonywa na kukatazwa mume, pia ndugu, jamaa na hata kasisi wamemshauri aondokane na hiyo imani yake mpya, bila mafanikio. Hii inaleta hali ya kutoaminiana na kuvunjika kwa amani nyumbani.
 
KIBONGOMKUTI,

Hapa naona umezungumza mambo ya maana. Je, unaweza fafanua zaidi kuhusu kigezo cha "tofauti za dini/kubadili dini"?

Mfano, inatosheleza kwamba mmoja wa wanandoa amebadili dhehebu ndani ya Ukristo? Asante!
 
Tatizo kubwa ni mke kabadili kabisa muelekeo kiimani kitu ambacho kinakingana na ile imani iliyokuwapo awali wakati wa kutoa kiapo cha ndoa kanisani. Licha ya kuonywa na kukatazwa mume, pia ndugu, jamaa na hata kasisi wamemshauri aondokane na hiyo imani yake mpya, bila mafanikio. Hii inaleta hali ya kutoaminiana na kuvunjika kwa amani nyumbani.

Hapa kuna utata.. labda tufafanulie hii imani imekuwake.binafsi naona hauna subira na unachukulia mambo haraka na utakuja juta.kumbuka uliapa kiapo for better for worse. kama unadhani mkeo kapotea wewe ndie mtu wa kwanza kumsaidia kurudi katika msitari. Tafuta hekima na akili ya kuishi na mkeo kwani wanawake ni viumbe dhaifu biblia inasema. Na itakuwaje kama ukioa mwingine nae abadilike utarudi tena mahakamani? Tafakari
 
Utangulizi.
................ ili ndoa ivunjwe lazima mahakama ijiridhishe bila kutia shaka kuwa ndoa hiyo haiwezi kutengemaa kabisa.

Du!!
Si bora kutokuifunga kabisa
Kuna ndugu yangu mmoja sasa ni mtu mzima kabisa miaka 78
enzi za ujana wake alikuwa na mke aliemkimbia na kumwachia kichanga, alihangaika kumafuta na kumrudisha nyumbani ikashindikana basi akapata mrembo mwingine, na wakaanza process za kuvunja ndoa ili wafunge ndoa, yani mhhh
walipata watoto ambao kwa sasa wote wanafamilia zao, ndoa bado haijavunjika, mke mdogo sasa ameshakufa miaka 67 ndoa haijavunjika!!
Yani hadi yule kichanga laieachwa ana mtoto ila ndoa haikuvunjika,
Maajabu sasa yule bibi ndio anataka kurudi anadai yeye ni mke halali!!
 
Wengi huwa wanaondoka tu na kuanza maisha mengine bila kuafuta ndoa ingine.
Hii ni nzuri zaidi kwani kuna uwezekano kuwa baadae akili zikitulia mtarudiana. Shida ni kama mtu bado una hasira na still unataka kufanya maamuzi.
 
Tatizo kubwa ni mke kabadili kabisa muelekeo kiimani kitu ambacho kinakingana na ile imani iliyokuwapo awali wakati wa kutoa kiapo cha ndoa kanisani. Licha ya kuonywa na kukatazwa mume, pia ndugu, jamaa na hata kasisi wamemshauri aondokane na hiyo imani yake mpya, bila mafanikio. Hii inaleta hali ya kutoaminiana na kuvunjika kwa amani nyumbani.
Mkuu, hapa hakuna ground nzito ya kuweza kujinasua kutoka ktk ndoa yako. Kubadili dini/dhehebu siyo sababu ya kuweza wewe kuvunja ndoa hiyo. Mbona zipo ndoa nyingi tu za mchanganyiko wa dini au madhehebu? Huwezi kumuacha mwenzako wa ndoa eti kwa sababu tu kaacha imani yake ya awali ambayo, nadhani, ndiyo hiyo uliyo wewe. Unapaswa kumheshimu, kujifunza kumvumilia na kuongea naye kwa upendo ili ikiwezekana arudi ktk imani yake ya awali; ikishindikana ishi naye hivyohivyo. Ndo ndoa hiyo mkuu: ndoa ndoana.

Kama suala ni kukosekana kwa amani katika nyumba, kimbilio siyo kuvunja ndoa bali kupatanishwa, kusaidiwa kuvumiliana. Na hiyo kazi wanaweza kuifanya wachungaji wenu au kamati ya usuluhishi ya usharika/parokia, nk. Vinginevyo kama huwezi vumilia basi kimbilia mahakama za serikali upate talaka hata kama kanisani haikusaidii wewe kiroho. Ila ujue hata huko mahakama za uraiani kwa kawaida zitakurudisha kanisani ili lishughulikiwe kikanisa.
 
KIBONGOMKUTI

Mbona huo mlolongo mkubwa mno hivyo?!

Unaweza kukuta watu wanakuwa emotional abused kwenye ndoa wanashindwa kutoka kwa sababu hawawezi kuonyesha wazi mateso, na mmoja kati ya wana ndoa hajakubali kuwa ndoa hiyo haiwezi kuendelea tena.

Something needs to be done, kulegeza masharti hayo.

Hii haijakaa sawa
 
zini hadi upate ukimwi,halafu ufe ndio utakuwa umeachana naye
 
kubadili imani sio sababu ya kuwatenga,kifo pekee ndicho kitawatenganisha
 
Hapa kuna utata.. labda tufafanulie hii imani imekuwake.binafsi naona hauna subira na unachukulia mambo haraka na utakuja juta.kumbuka uliapa kiapo for better for worse. kama unadhani mkeo kapotea wewe ndie mtu wa kwanza kumsaidia kurudi katika msitari. Tafuta hekima na akili ya kuishi na mkeo kwani wanawake ni viumbe dhaifu biblia inasema. Na itakuwaje kama ukioa mwingine nae abadilike utarudi tena mahakamani? Tafakari

Asante kwa maoni yako. Nachotaka kufahamu ni sheria imekaaje kuhusu tatizo hili. Isitoshe jee kiapo cha ndoa kilichotolewa dhehebu moja bado kitaendelea kuwa halali kama mmoja wa wanandoa baadaye aamue kujitoa kwenye dhehebu lake na kuingia dhehebu lingine?
 
Mkuu, hapa hakuna ground nzito ya kuweza kujinasua kutoka ktk ndoa yako. Kubadili dini/dhehebu siyo sababu ya kuweza wewe kuvunja ndoa hiyo. Mbona zipo ndoa nyingi tu za mchanganyiko wa dini au madhehebu? Huwezi kumuacha mwenzako wa ndoa eti kwa sababu tu kaacha imani yake ya awali ambayo, nadhani, ndiyo hiyo uliyo wewe. Unapaswa kumheshimu, kujifunza kumvumilia na kuongea naye kwa upendo ili ikiwezekana arudi ktk imani yake ya awali; ikishindikana ishi naye hivyohivyo. Ndo ndoa hiyo mkuu: ndoa ndoana.

Kama suala ni kukosekana kwa amani katika nyumba, kimbilio siyo kuvunja ndoa bali kupatanishwa, kusaidiwa kuvumiliana. Na hiyo kazi wanaweza kuifanya wachungaji wenu au kamati ya usuluhishi ya usharika/parokia, nk. Vinginevyo kama huwezi vumilia basi kimbilia mahakama za serikali upate talaka hata kama kanisani haikusaidii wewe kiroho. Ila ujue hata huko mahakama za uraiani kwa kawaida zitakurudisha kanisani ili lishughulikiwe kikanisa.

Kuna tofauti kubwa kati ya kuingia "ndoa za mchanganyiko wa dini au madhehebu" kwa hiyari wakati wa kufunga ndoa, na pale mmoja wa wanandoa anapoamua kuingia dini au dhehebu tofauti baada ya kiapo cha ndoa.
 
Kurahisisha matatizo ya ndoa za wenzenu mnaona jambo la kawaida sana, ngoja yawakute muone shughuli yake! kila ndoa ni unique na pia matatizo kati ya ndoa fulani na nyingine yanaweza kufanana lakini yakawa na uzito tofauti kutokana na mahusiano na kuzoeana baina ya wanandoa hao kulikopelekea wao kuoana. Tabia,uaminifu au imani ya mwanandoa inaweza kubadilika na kusababisha misingi ya ndoa kulegalega na hatimaye maana halisi ya ndoa husika inatoweka, mwanandoa mmoja anaweza kusamehe uzinzi wa mwenzi wake lakini si lazima iwe hivyo kwa ndoa nyingine!
Kubadili imani ya dini kwa kiasi kikubwa kunafanya ndoa iwe batili kwa kuwa maudhui ya ndoa yanatofautiana baina ya dini na dini; mathalani mwanamke anafunga ndoa ya kikristo akijua na kuamini kwamba kwenye ukristo mwanaume haruhusiwi kuwa na mke zaidi ya mmoja na hivyo akaridhia kuolewa kwa ndoa ya kikristo maana ndio anakubaliana nayo halafu inatokea mmewe anabadili dini na kuwa muislam ambapo ni ruksa kuoa mke zaidi ya mmoja, je hapo mustakabali wa ndoa yao unakuwa katika hali gani iwapo sasa mmewe wakati wowote anaweza kuongeza mke kwa mujibu wa dini yake wakati mke hakuingia kwenye ndoa kwa misingi ya imani hiyo!!?
 
Sheria haina dini, ndoa yeyote inaweza kuvunjwa hata hiyo ya kikristo...Biblia yenyewe inavunja ndoa kwa njia mbili...Ya kwanza ni ZINAA na ya pili ni KIFO. Mathayo 19

Kiswahili (Tanzania)

1
Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo, akatoka Galilaya akafika mipaka ya Uyahudi, ng'ambo ya Yordani.
2 Makutano mengi wakamfuata, akawaponya huko.
3 Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?
4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.
9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
10 Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.
11 Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.
12 Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.

British English

Matthew 19

New International Version (NIV)

Divorce

19 When Jesus had finished saying these things, he left Galilee and went into the region of Judea to the other side of the Jordan. [SUP]2 [/SUP]Large crowds followed him, and he healed them there.
[SUP]3 [/SUP]Some Pharisees came to him to test him. They asked, "Is it lawful for a man to divorce his wife for any and every reason?"
[SUP]4 [/SUP]"Haven't you read," he replied, "that at the beginning the Creator ‘made them male and female,'[SUP][a][/SUP][SUP]5 [/SUP]and said, ‘For this reason a man will leave his father and mother and be united to his wife, and the two will become one flesh'[SUP][b][/SUP]? [SUP]6 [/SUP]So they are no longer two, but one flesh. Therefore what God has joined together, let no one separate."
[SUP]7 [/SUP]"Why then," they asked, "did Moses command that a man give his wife a certificate of divorce and send her away?"
[SUP]8 [/SUP]Jesus replied, "Moses permitted you to divorce your wives because your hearts were hard. But it was not this way from the beginning. [SUP]9 [/SUP]I tell you that anyone who divorces his wife, except for sexual immorality, and marries another woman commits adultery."
[SUP]10 [/SUP]The disciples said to him, "If this is the situation between a husband and wife, it is better not to marry."
[SUP]11 [/SUP]Jesus replied, "Not everyone can accept this word, but only those to whom it has been given. [SUP]12 [/SUP]For there are eunuchs who were born that way, and there are eunuchs who have been made eunuchs by others-and there are those who choose to live like eunuchs for the sake of the kingdom of heaven. The one who can accept this should accept it."

iSizulu (iNingizimu Afrika)

1Kwathi uJesu eseqedile lawo mazwi, wamuka eGalile, weza emikhawulweni yaseJudiya phesheya kweJordani.
2 Izixuku ezinkulu zamlandela, waziphulukisa khona.
3 Kwase kusondela kuye abaFarisi, bamlinga bathi: "Kuvunyelwe yini ukuba indoda ilahle umkayo noma ngaliphi icala na?"
4 Waphendula, wathi kubo: "Anifundanga yini ukuthi owadala ekuqaleni wabenza owesilisa nowesifazane,
5 wathi: ‘Ngenxa yalokho umuntu uyakushiya uyise nonina, anamathele kumkakhe; labo ababili bayakuba nyamanye,' na?
6 Ngakho abasebabili, kodwa banyamanye. Ngakho-ke lokho akuhlanganisileyo uNkulunkulu, umuntu makangakwahlukanisi."
7 Bathi kuye: "Pho, uMose wayalelani ukuthi makanikwe incwadi yesahlukaniso, alahlwe, na?"
8 Wathi kubo: "Ngenxa yobulukhuni benhliziyo yenu uMose wanivumela ukwahlukana nabo omkenu, kepha kusukela kwasekuqaleni kwakungenjalo.
9
Namanje ngithi kini: Yilowo nalowo olahla umkakhe kungengokuphinga, aganwe ngomunye, uyaphinga; noganwa ngolahliweyo uyaphinga."
10 Abafundi bathi kuye: "Uma injalo indaba yomuntu nomkakhe, akukuhle ukuganwa."
11 Kepha wathi kubo: "Akusibo bonke abangalamukela leli zwi, kuphela abakunikiweyo.
12 Ngokuba kukhona abathenwa abazalwa benjalo kwasesiswini sikanina; kukhona nabathenwa abathenwe ngabantu; kukhona futhi abathenwa abazithenileyo ngenxa yombuso wezulu. Ongakwamukela lokho akwamukele."
 
Asante kwa maoni yako. Nachotaka kufahamu ni sheria imekaaje kuhusu tatizo hili. Isitoshe jee kiapo cha ndoa kilichotolewa dhehebu moja bado kitaendelea kuwa halali kama mmoja wa wanandoa baadaye aamue kujitoa kwenye dhehebu lake na kuingia dhehebu lingine?
Unauliza sheria ya dini au sheria ya nchi? Imani ni mambo binafsi. Sheria ya nchi haiwezi kuingilia uhuru wa mtu kubadili dini. Ila sheria ya nchi inachoangalia ni uwezekano wa mtu kubadili aina ya ndoa (angalia cheti cha ndoa). Unapofunga ndoa iwe ya kikiristo au ya imani nyingine kwenye cheti/shahada ya ndoa inayotolewa na serikali lazima aina ya ndoa iainishwe: yaani kama ni ya mke mmoja au ya wake wengi. Ndoa za kikristo daima za mke mmoja. Na kujitoa katika ndoa hii ya mke mmoja njia ya kawaida ni talaka. Ukishapata talaka unakuwa huru kuoa au kuolewa civilly. Kikanisa, talaka haikusaidii kwa sababu kanisani bado ndoa inatambulika mpaka kufa mmoja wenu. Hivyo kwa baadh ya madhehebu, kwa kuwa umepata talaka na kuoa, hutakubaliwa kupokea sakramenti wala kuzikwa kikristo.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya kuingia "ndoa za mchanganyiko wa dini au madhehebu" kwa hiyari wakati wa kufunga ndoa, na pale mmoja wa wanandoa anapoamua kuingia dini au dhehebu tofauti baada ya kiapo cha ndoa.
Mkuu, ndoa haimuzuii mtu kubadili dini kwani kuabudu ni moja ya haki msingi za mwanadamu. Wewe mwanandoa una haki kwa mkeo/mumeo katika mengi mf. tendo la ndoa, kuishi pamoja, kusaidiana. Lakini huna haki ya kumiliki maisha yake ya kiroho (ila haki na wajibu wa kumsaidia kuishi imani yake lakini si kummiliki kiimani). Unachotakiwa wewe kukidai kutoka kwake ni huduma zake, yaani haki zako wewe za kindoa. Huna haki za kiimani kwake.
 
Sio kweli wanavunja hasa sababu ikiwa ni mmoja wa wanandoa kutokuwa mwaminifu yaani kufanya uzinifu! Nina ushahidi wa ndoa ya kikatoliki iliyovunjwa kwa sababu hiyo!

Sijawahi sikia labda kutengana kwa muda na sio divorce. Nitalichunguza siwezi kukataa sana lakini nijuavyo ni hivyo. You might be right.
 
Back
Top Bottom