EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,325
Fanza hivi
1. Peleka malalamiko yako kwenye Baraza la Usuluishi linalotambulika kisheria (Ofisi ya ustawi wa Jamii, Kiongozi wa Kanisa mwenye mamlaka ya kufungisha ndoa)
2. Baraza/Kiongozi husika atawasikiliza wanandoa wote na kuona kama anaweza kuwashauri ili msamehane na kuendelea kuishi pamoja. Kutengana kisheria/makubaliano huwa ni mbadala katika hili.
3. Endapo usuluishi utashindikana Baraza/Kiongozi husika atakupatia Barua/Hati ya kushindwa kusuluishwa. Barua/Hati hiyo itaandikwa ikielekekzwa kupelekwa katika Mahakama husika.
4. Ukifika Mahakamani unatakiwa kulipia gharama za kufungua Kesi ya Ndoa ili kuomba TALAKA na Kuvunja Ndoa yenu rasmi kisheria ukipenda na mgawanyo wa mali za ndoa plus matunzo ya watoto kama wapo. Kumbuka kuambatanisha Madai yako na Cheti cha ndoa
5. Mahakama itasajili Kesi yako ya Madai ya Talaka na kukupa Hati ya kumwita Mkeo Mahakamani ili kujibu madai dhidi yake
Angalizo;
Sababu kubwa ya kuvunja ndoa na kutoa Talaka huwa ni KUWEZA KUITHIBITISHIA MAHAKAMA KUAMINI KUWA NDOA YAKO IMEVUNJIKA KIASI AMBACHO HAIWEZI KUREKEBISHIKA TENA.
Aidha Mahakama uangalia mambo muhimu/vigezo vifuatavyo ili kujiridhisha
(a) Ugoni
(b)Ukatili
(c)Kulawiti
(d)Kichaa
(e) Kuzembea wajibu kwa makusudi
(f) Uasi/Utoro
(g) Kutengana - kusiko pungua miaka 3
(h) Kifungo
(i) Dhana ya Kifo
(j) Tofauti za Dini/Kubadili Dini
Anyway huo ndo ushauri wangu faster lakini kwanini uvunje ndoa Bana, gangamala maisha sio mchezo etiii.
Kwa vile ndoa ni makubaliano ya watu wawili, vipi kama hao watu wakiamnua by mutual consent kuvunja makubaliano yao ya kuishi pamoja? Kwani ni lazima kuwe na ugoni, ukatili, kulawiti, nk? Si wanaweza kukubaliana tuu hata kama hayo uliyootheresha hapo juu hayapo? Mahakama inaweza kukataa?