Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Ukiishi na mke kwa zaid ya miaka miwili bila kufunga ndoa ,kisheria hiyo inahesabka km ndoa.
Hata km mke anaamua kuondoka bado sheria ya ndoa haimpi fursa ya kubeba kila kitu, labda km alipata kabla ya ndoa au anavimiliki yeye. Kumchukua mke wa mtu ni kosa,unaweza kumshitaki na ukaombwa kulipwa fidia.
 
Ukiishi na mke kwa zaid ya miaka miwili bila kufunga ndoa ,kisheria hiyo inahesabka km ndoa.
Hata km mke anaamua kuondoka bado sheria ya ndoa haimpi fursa ya kubeba kila kitu,labda km alipata kabla ya ndoa au anavimiliki yeye.
Kumchukua mke wa mtu ni kosa,unaweza kumshitaki na ukaombwa kulipwa fidia.

ok ni kifungu gani cha sheria kinacho sema hivyo maana nayasikia sikia tu na wanaosema hivyo hawatoi vifungu vya sheria
 
ok ni kifungu gani cha sheria kinacho sema hivyo maana nayasikia sikia tu na wanaosema hivyo hawatoi vifungu vya sheria

160,sheria ya ndoa ya mwaka 1971
 
ikikumbukwe kwamba kifungu hiki kimeekwa kumlinda mwanamke...! Kwake ye inatumika kama ngao kwake katka mgawanyo wa mali na wewe..na sio kumpa nguvu ya kuamua atakavyo! Kuhusu Mgawanyo wa mali.
 
ikikumbukwe kwamba kifungu hiki kimeekwa kumlinda mwanamke...! Kwake ye inatumika kama ngao kwake katka mgawanyo wa mali na wewe..na sio kumpa nguvu ya kuamua atakavyo! Kuhusu Mgawanyo wa mali.

na kama kinamlinda yeye kama ngao kifungu hicho hakiwezi kumubana yeye kutoka kwa mwanamme na kwenda kuishi na mwanamme mwingine.kwa madai kuw sijafunga naye ndoa wala sijamtolea mahali kwao?
 
Mimi nilikuwa na mwanamke naishi naye nimeishi naye kwa zaidi ya miaka minne sikuwahi kufunga naye ndoa wala sikumtolea mahali,nimezaa naye watoto wawili sasa tumehitilafiana naye akabeba kila kitu ndani mwangu akaondoka navyo pamja na watoto na kuhamia kwa mwanamme mwingine.vitu wanavyotumia nivya kwangu je?nina haki ya kwenda kumyangaya vile vitu?naomba msaada wa kisheria kifungu kwa kifungu

Hapa kuna matatizo mawili makubwa ambayo pengine uamuzi wake unaweza kuhusisha sheria tofauti. Kwanza hilo la kuchukua mali zako na kuzihamishia kwa mwanaume mwingine limekaa kijinai (naona kama kuna harufu ya wizi/unyang'anyi). Toa taarifa polisi kuwa mali/vitu vyako vimechukuliwa kinyume cha sheria.

Hilo la yeye, kuondoka kutoka kwako pamoja na watoto wenu na kwenda kuishi na mwanaume ndio pengine sheria ya ndoa itaingia ili kujibu baadhi ya maswali (je kulikuwa na ndoa? Je ndoa hiyo kama ilikuwepio imevunjika/hairekebishiki? Je utaratibu na mustakabali wa watoto unakuwaje?). Na kama ndoa ilikuwepo, kunaweza kuwepo na kesi nyingine (kama utaamua kuifungua) ya madai dhidi ya huyu 'mkeo' na huyo 'mwanaume' mwingine.
 
Ukiishi na mke kwa zaid ya miaka miwili bila kufunga ndoa ,kisheria hiyo inahesabka km ndoa.
Hata km mke anaamua kuondoka bado sheria ya ndoa haimpi fursa ya kubeba kila kitu,labda km alipata kabla ya ndoa au anavimiliki yeye.
Kumchukua mke wa mtu ni kosa,unaweza kumshitaki na ukaombwa kulipwa fidia.

Ukiishi na mwanamke bila kufunga nae ndoa hata kama ni miaka mitano bado sheria inawachukulia kama nyie ni mahawara ila endapo kutakuwa na mgogoro ambao utapelekea wawili hao kuachana ndio sheria inapoingia kuona haki ya kila mtu ni ipi.

Sasa hapa ndugu alan anatakiwa awaone wanasheria kwa msaada zaidi wengine sie ni wazee wa kuangalia TV kuhusu elimu ya sheria hatupo nondo sana ila hili la kuhamisha vitu na kwenda kwa mwanaume mwingine nalo ni neno unless kama angekuwa anaishi mwenyewe maana kama kwako amekimbia siku wakikorofishana huko nako itakuaje maana hizo mali ni za hao watoto aliotoka nao kwako na si za yule bwana na watoto watakaozaliwa na yule mwanaume
 
Last edited by a moderator:
alan, La kwanza kabisa sheria inasema kuwa ukishakaa na mke kwa zaidi ya miaka miwili katika nyumba moja na mkalala kitanda kimoja na jamii iliyowazunguka ikaamini kuwa nyie ni mke na mume, hata kama hamjaoana inasema nyie ni wanandoa hadi hapo itakapothibitika vinginevyo.

Hivyo basi hivyo vitu kama mlichuma mkiwa pamoja inabidi mgawane kutokana na kila nguvu ya mtu ilivyotumika katika kuvichuma vitu hivyo. Ili upate ufafanuzi wa mgawanyo nenda kwenye vyombo vya sheria itatoa muongozo zaidi kwani kutakuwa na maswali mengi ambayo mtaulizwa nyie wote wawili ili kuthibitisha hayo ya kuishi pamoja kama mke na mume, nani alikua na kitu gani kabla na baada ya kuishi pamoja, na maswala ya watoto yanakuaje baada ya wawili nyie kutengana. Lakini mwisho ya yote kila mtu atapata stahiki yake. Pole sana
 
SMU,

Inakuwaje anakuwa na ujasiri wa kubeba na watoto kwenda ishi nao kwa mume mwingine, na huyo mume mwingine anakuwaje na ujasiri wa kulea watoto wa mtu mwingine? chunga mjomba vinasaba vinasemaje?
 
Ukiishi na mke kwa zaid ya miaka miwili bila kufunga ndoa ,kisheria hiyo inahesabka km ndoa.
Hata km mke anaamua kuondoka bado sheria ya ndoa haimpi fursa ya kubeba kila kitu,labda km alipata kabla ya ndoa au anavimiliki yeye.
Kumchukua mke wa mtu ni kosa,unaweza kumshitaki na ukaombwa kulipwa fidia.

There is a rebutable presumption of marriage! It does not come automatically that one is your wife/husband. Suppose one of you has a subsisting monogamy marriage? Waendee wanasheria, kuna technicalities za marriage law nyingi hapo
 
Inakuwaje anakuwa na
ujasiri wa kubeba na watoto kwenda ishi nao kwa mume mwingine, na huyo
mume mwingine anakuwaje na ujasiri wa kulea watoto wa mtu mwingine?
chunga mjomba vinasaba
vinasemaje?

Angekuwa yeye ndio kapeleka watoto wakalelewe na mama wa kambo vinasaba vingeuliziwa?
 
Angekuwa yeye ndio kapeleka watoto wakalelewe na mama wa kambo vinasaba vingeuliziwa?

sasa kwa mfano nimekwenda kupima vinasaba imegundulika wale watoto siyo wa kwangu na nimewalea zaidi ya miaka minne na hadi hivi sasa bado anakuja kuchukua pesa kwa ajiri ya watoto sasa je? watoto wakigundulika siyo wa kwangu je naweza kumshitaki na kwa kosa gani.wanasheria hebu fungukeni hapo
 
Je, ni taratibu zipi za kufuata ili mwanandoa aliyefunga ndoa ya Kikristo kanisani aweze kuivunja ndoa hiyo kimahakama au kisheria?

Wataalamu wa Sheria tafadhali naomba mnifahamishe.

Natanguliza shukrani.
 
Ujue ndoa za kikristo kimsingi hazivunjwi, ni mpaka kifo kiwatenganishe wanandoa. Nadhani inategemea pia umefunga ndoa ya kikristo ktk madhehebu gani. Kuna madhehebu ambayo kukiwa na matatizo fulani mazito ktk ndoa, yanaweza "kuivunja" ndoa hiyo na kukupa nafasi ya kufunga. Lakini kuna madhehebu ambayo nafasi hiyo ni finyu mno-mno.
 
mkuu kama kwel we ni muumini bora wa ndoa za kikisto kabla cjakushauri hebu jaribu kueleza tatizo la msingi linalokvafanya utake kuvunja ndo.a
 
Utangulizi.

Ndoa inaweza kuvunjwa na mahakama iwapo mambo haya yafuatayo yametokea kwenye ndoa husika na mmoja wa wanandoa kuchukua hatua ya kuomba mahakama ivunje ndoa hiyo.

1. kufumaniwa unazini-(walau iwe mara kwa mara)
2. ukatiri uliopitiza kwa mwenzi wako.
3. kumtenga mwenzi wako kwa kipindi kisichopungua miaka 8,aidha kwa kuhama chumba au kuhama nyumba,mji au nchi.

Sasa iwapo kati ya hayo niliyoyataja hapo juu yametokea mwanandoa anatakiwa kwanza aende kanisani kwa usuluhishi na ikishindika Mchungaji au Padri atatoa cheti cha kushindwa kusuluhisha, kwa faida ya watu wote iki cheti cha kushindwa kusuluhisha ni muhimu sana kwani huwezi kufungua kesi mahakama kuomba mahakama kuvunja ndoa bila kuonesha ulianzia kanisani na wakashindwa kuwasuruhisha.

Lakini mbali na zile sababu 3 nilizosema zinaweza peleka mahakama kuvunja ndoa, ili ndoa ivunjwe lazima mahakama ijiridhishe bila kutia shaka kuwa ndoa hiyo haiwezi kutengemaa kabisa.
 
Ujue ndoa za kikristo kimsingi hazivunjwi, ni mpaka kifo kiwatenganishe wanandoa. Nadhani inategemea pia umefunga ndoa ya kikristo ktk madhehebu gani. Kuna madhehebu ambayo kukiwa na matatizo fulani mazito ktk ndoa, yanaweza "kuivunja" ndoa hiyo na kukupa nafasi ya kufunga. Lakini kuna madhehebu ambayo nafasi hiyo ni finyu mno-mno.

catholics hawavunji ndoa aslani kwa lolote lile on earth! Hakuna talaka! acha talaka rejea
 
Jee, ni taratibu zipi za kufuata ili mwanandoa aliyefunga ndoa ya Kikristo kanisani aweze kuivunja ndoa hiyo kimahakama au kisheria?

Wataalamu wa Sheria tafadhali naomba mnifahamishe. Natanguliza shukrani.
Kwa nini unataka ivunjwe?
 
Back
Top Bottom