Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Habari,kutoka na matatizo yaliyotokea nimedivorc na mume wangu nimezaa nae mtoto1,,nilikuwa nauliza kama nina haki yeyote ya kisheria ya mali tulizochuma nae wakati niko ktk ndoa
 
Mkuu 32Roberts,majibu yako ni kama ifuatavyo:

1. Kama ikitokea unachokidai kitajitokeza kama sababu ya kutaka kuvunja ndoa.anayedai hivyo atapaswa kuthibitisha hivyo. Lakini,ajenda ya siri si moja ya sababu za kuvunja ndoa. Soma majibu yaliyotangulia na utazijua sababu za kuvunja ndoa.

2. Jibu la swali hili limeshatolewa Mkuu.Lakini,kwa heshima yako,nalirudia kidogo. Ni kwamba,Sheria ya Ndoa inaruhusu mali binafsi na mali za pamoja katika ndoa. Ni wajibu wa mume kuhakikisha kuwa ana ushahidi juu ya mali binafsi.

3.Ndiyo

4. Ni uasherati unaotosha kuvunja ndoa

5.Mabaraza ya Usuluhishi yanaundwa kwa mujibu wa Sheria.Si kila Msikiti,Kanisa,Ustawi wa Jamii na kadhalika ni Mabaraza ya Usuluhishi
 
Last edited by a moderator:
Habari,kutoka na matatizo yaliyotokea nimedivorc na mume wangu nimezaa nae mtoto1,,nilikuwa nauliza kama nina haki yeyote ya kisheria ya mali tulizochuma nae wakati niko ktk ndoa

Mkuu hawasaid,kwanza,nikupe pole kwa kutokea kwa jambo hilo la talaka. Pili, natumai kuwa ndoa yenu imevunjwa Mahakamani.Kama si hivyo,basi ndoa yenu bado ipo. Tatu,sijui ni kwanini (kama ndoa ilivunjwa kimahakama) hukuambatanisha Maombi ya Mgawanyo wa Machumo katika maombi ya talaka. Lakini,una haki katika machumo.Utaipata haki hiyo pale ambapo utawasilisha ombi la kisheria Mahakamani kuaka jambo hilo.
 
Last edited by a moderator:
Swali, Je, mwanamke ambae hakufunga ndoa na mwanaume na wameishi zaidi ya miaka kumi kama mke na mume na kujaaliwa kupata watoto. Endapo mume kamchoka mke na kuamua kumfukuza je huyo mke ana haki zipi na kwa taratibu zipi
(a) Haki katika mali za ndoa walizo chuma au kuziendeleza pamoja?
(b) Haki za kuona, kuhudumia au kulea watoto?
(c) Haki ya kuolewa kama akipata mpiga show mwingine?

Mkuu KIBONGOMKUTI,nikushauri siku nyingine uulize katika lugha ya staha ili upate majibu ya staha. Mwanamke wa namna hiyo uliyoiulizia atapata haki kadiri Mahakama itakavyoamuru. Lazima shauri lifunguliwe Mahakamani na lisikilizwe pande zote isipokuwa tu kama upande wowote utaamua kutosikilizwa.
 
Asante Mheshimiwa Wakili Msomi vigezo na masharti kuzingatiwa, nina amini majibu uliyotoa ni mujarabu hayakuzingatia kukwaza kwa lugha niliyotumia kuuliza?
 
Naomba mnifahanishe iwapo mke ndio kataka kukatiza ndoa yake namaanisha kuomba talaka bila kuwa na ugomvi kati yake na mumewe. Je, hapo kunahitajika kigawana mali? Na je, mtoto ataenda kuishi na mama au baba?
 
Mkuu Zogwale, mtiririko wa kesi hizo umejaa ukakasi na giza kisheria. Ieleweke kuwa,kufungua kesi/shauri ni haki ya kila mtu mwenye malalamiko dhidi ya mwingine au Serikali.Baada ya kufunguliwa kwa shauri,mfunguzji anakuwa na wajibu wa kuhakikisha shauri lake linafikia mwisho-ikiwa ni pamoja na kuhudhuria Mahakamani.

Kufunguafungua kesi bila ya mpango na utaratibu ni usumbufu kwa unayemlalamikia na Mahakama kwa ujumla.Lazima kuwe na sababu na hoja za kila kesi. Ningekuwa mimi,ningemuandama kwa mapingamizi huyo mume hadi akome.

Kimsingi, mume na mke wote wana haki ya kufungua kesi ya kudai talaka.Jambo la muhimu ni kuwa na sababu za kudai talaka zinazotambuliwa na kuainishwa kisheria.Sababu kuu za kudai talaka ni uasherati,mateso na kutelekeza. Pia,lazima taratibu za shauri husika zifuatwe ipasavyo-muda,kupitia Bodi ya Usuluhishi na kadhalika.

Asante kwa ufafanuzi murua. Akimfungulia tena kesi nitakuomba umsaidie mkuu. Keep it up.
 
Wana-JF,karibuni hapa kwa maswali mbalimbali yahusuyo Sheria ya Ndoa,1971.Wale wote waliopo kwenye ndoa na wanaotarajia kuwa kwenye ndoa wanakaribishwa hapa kuuliza na kujibiwa. Nitashirikiana na Mawakili Wasomi wenzangu waliopo humu kuwajibu maswali yenu.

Mods, mnaweza kuufanya uzi huu kuwa 'sticky'? Asanteni na karibuni!

mkuu msomi naomba uniambie age of marriage inakuwaje kisheria ni miaka mingap male or female anaweza oa au olewa.sor kwa kuchanganya lugha
 
Asante Mkuu alteza kwa swali lako. Umri wa wa kiume ni miaka 18 na wa kike ni miaka 15.Lakini,Mahakama yaweza kuwaruhusu wanaotaka kuoana kuoana hata bila kuwa na umri huo endapo: kwanza,wote wamefikisha umri wa miaka 14,na pili kama Mahakama imekubaliana na mazingira yaliyopo na kuiona ndoa husika inayotakiwa kufungwa.
 
asante learned sasa izo age mara nyingi bado tunaluwa tupo shule ya msing au secondary naona kunautata hapa kidogo nisaidie mkuu sijui kama bado nipo ndan ya mada au nimetoka.
thanks in advance.
 
Mkuu alteza,ulihitaji umri nami nikakupatia. Ni kwa mujibu wa kifungu cha 13 cha Sheria ya Ndoa,1971. Vipi kuhusu wale ambao hawasomi Mkuu? Hiyo ni ruhusa tu na si shinikizo. Hapo Sheria imetoa umri wa chini kabisa wa kuweza kufunga ndoa.Basi.
 
Last edited by a moderator:
Asante bwana petro kwa ufafanuzi unaotoa ila naomba unieleweshe vizuri kuwa mwanaume na mwanamke wanaishi pamoja kwa miaka mitatu ndani ya kuishi pamoja kuna mali walichuma wote kama kununua kiwanja lkn baada ya mda fulan mwanamke akaondoka kwa maana hiyo mwanamke akamuacha mwanaume na wamezaa mtoto je ile mali itakuwa ya nani ya ndoa au?
 
Wana-JF,karibuni hapa kwa maswali mbalimbali yahusuyo Sheria ya Ndoa,1971.Wale wote waliopo kwenye ndoa na wanaotarajia kuwa kwenye ndoa wanakaribishwa hapa kuuliza na kujibiwa. Nitashirikiana na Mawakili Wasomi wenzangu waliopo humu kuwajibu maswali yenu.

Mods, mnaweza kuufanya uzi huu kuwa 'sticky'? Asanteni na karibuni!

Sheria ya ndoa inamsaidiaje pale ambapo mmoja wa wanandoa anaamua kuondoka nakumuacha mwenzake na pia mambo mengine yote yanakuwa yako vizuri kiasi kwamba hawezi sema ameachwa pasi na mahitaji yake ya kimaisha na yule alie muacha hana shida na mali walizopata na kwamba yule alieachwa anaweza kuishi kwa mali hizo pasipo shida. Je sasa huyu ambaye anaona kwamba mwzenzake anamuacha kwa maksudi, je sheria hii inamsaidiaje ili asiachwe? kwa mtazamo wangu sheria hii ya ndoa imekaa style ya kulinda mslahi (Material things) na sio kulinda hiyo Union isivunjike pale mmoja anapokuwa kaamua kumkimbia menzake na ukizingatia hakuna adhabu hazieleweki na ni kama hakuna adhabu ambayo inaweza kumzuia mmoja wao kuogopa kuvuruga ndoa hiyo kabla mahakama haijatoa talaka.

kwa mtazamo huo huo mimi nionavyo nguvu ya kulinda ndoa isivunjike atleast iko kwa wazazi lakini sheria ya ndoa na serikali haina 'meno' ya kulinda ndoa isisambaratike zaidi ya kutetea maslahi pekee, japokuwa serikali itagoma kutoa talaka lakini je pale mmoja anapokuwa hajali cha talaka na kuamua kwenda aendako sheria inasaidia vipi

hebu fafanua mwanasheria
 
Mkuu, mimi nijibu swali gani ikiwa umeuliza na kujibu mwenyewe?
 
Mkuu,mimi nijibu swali gani ikiwa umeuliza na kujibu mwenyewe?

Wewe kama mwanasheria ungenitoa kwenye perception yangu vinginevyo hiyo perception itabakia na mimi kwa kuweka huo mtizamo wangu ingekupa picha nzuri ya kunielewa vizuri na wewe kutoa ufafanuzi ambao ungetengua mitizamo kama hiyo vinginevyo itafanya any long perception to be correct
 
Wana-JF,karibuni hapa kwa maswali mbalimbali yahusuyo Sheria ya Ndoa,1971.Wale wote waliopo kwenye ndoa na wanaotarajia kuwa kwenye ndoa wanakaribishwa hapa kuuliza na kujibiwa. Nitashirikiana na Mawakili Wasomi wenzangu waliopo humu kuwajibu maswali yenu.

Mods, mnaweza kuufanya uzi huu kuwa 'sticky'? Asanteni na karibuni!

Vipi mkuu procedures za kuvunja ndoa ambapo mmoja wa wanandoa ameshaenda zake na kufunga ndoa na mtu mwingine wakati ndoa ya awali bado haijavunjwa rasmi. utaratibu lazima kuanzia huko kwenye baraza la wazee au unaweza kwenda moja kwa moja mahakamani?

Pia naomba kujua maximum penalty kwa mtu kufunga ndoa nyingine wakati ndoa ya awali haijavunjwa kisheria
 
Mkuu Balacuda,ndoa yoyote iliyokuwa halali lazima ivunjwe kwa mujibu wa taratibu za kisheria zilizopo. Moja ya taratibu hizo ni kupitia katika Baraza la Usuluhishi wa Ndoa. Hilo ni sharti muhimu.

Nyongeza: Kama ndoa ya mwanzo ilikuwa ni ya mke mmoja,hakukuwahi kuwa na ndoa nyingine ya pili au ya tatu na kadhalika. Lakini,aliyetelekezwa aweza kuomba kuvunja ndoa ya halali kwa kuweka mbele sababu za kutelekezwa na uasherati.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom