Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Nadhani Mkuu,tuendelee pale tulikoanza kimawasilianoSodomy inaweza kuwa kigezo cha kubatilisha ndoa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nadhani Mkuu,tuendelee pale tulikoanza kimawasilianoSodomy inaweza kuwa kigezo cha kubatilisha ndoa?
Habari,kutoka na matatizo yaliyotokea nimedivorc na mume wangu nimezaa nae mtoto1,,nilikuwa nauliza kama nina haki yeyote ya kisheria ya mali tulizochuma nae wakati niko ktk ndoa
Swali, Je, mwanamke ambae hakufunga ndoa na mwanaume na wameishi zaidi ya miaka kumi kama mke na mume na kujaaliwa kupata watoto. Endapo mume kamchoka mke na kuamua kumfukuza je huyo mke ana haki zipi na kwa taratibu zipi
(a) Haki katika mali za ndoa walizo chuma au kuziendeleza pamoja?
(b) Haki za kuona, kuhudumia au kulea watoto?
(c) Haki ya kuolewa kama akipata mpiga show mwingine?
Mkuu KIBONGOMKUTI,nikushauri siku nyingine uulize katika lugha ya staha ili upate majibu ya staha. Mwanamke wa namna hiyo uliyoiulizia atapata haki kadiri Mahakama itakavyoamuru. Lazima shauri lifunguliwe Mahakamani na lisikilizwe pande zote isipokuwa tu kama upande wowote utaamua kutosikilizwa.
Mkuu Zogwale, mtiririko wa kesi hizo umejaa ukakasi na giza kisheria. Ieleweke kuwa,kufungua kesi/shauri ni haki ya kila mtu mwenye malalamiko dhidi ya mwingine au Serikali.Baada ya kufunguliwa kwa shauri,mfunguzji anakuwa na wajibu wa kuhakikisha shauri lake linafikia mwisho-ikiwa ni pamoja na kuhudhuria Mahakamani.
Kufunguafungua kesi bila ya mpango na utaratibu ni usumbufu kwa unayemlalamikia na Mahakama kwa ujumla.Lazima kuwe na sababu na hoja za kila kesi. Ningekuwa mimi,ningemuandama kwa mapingamizi huyo mume hadi akome.
Kimsingi, mume na mke wote wana haki ya kufungua kesi ya kudai talaka.Jambo la muhimu ni kuwa na sababu za kudai talaka zinazotambuliwa na kuainishwa kisheria.Sababu kuu za kudai talaka ni uasherati,mateso na kutelekeza. Pia,lazima taratibu za shauri husika zifuatwe ipasavyo-muda,kupitia Bodi ya Usuluhishi na kadhalika.
Wana-JF,karibuni hapa kwa maswali mbalimbali yahusuyo Sheria ya Ndoa,1971.Wale wote waliopo kwenye ndoa na wanaotarajia kuwa kwenye ndoa wanakaribishwa hapa kuuliza na kujibiwa. Nitashirikiana na Mawakili Wasomi wenzangu waliopo humu kuwajibu maswali yenu.
Mods, mnaweza kuufanya uzi huu kuwa 'sticky'? Asanteni na karibuni!
mkuu msomi naomba uniambie age of marriage inakuwaje kisheria ni miaka mingap male or female anaweza oa au olewa.sor kwa kuchanganya lugha
Asante Mkuu alteza kwa swali lako. Umri wa wa kiume ni miaka 18 na wa kike ni miaka 15.Lakini,Mahakama yaweza kuwaruhusu wanaotaka kuoana kuoana hata bila kuwa na umri huo endapo: kwanza,wote wamefikisha umri wa miaka 14,na pili kama Mahakama imekubaliana na mazingira yaliyopo na kuiona ndoa husika inayotakiwa kufungwa.
asante learned sasa izo age mara nyingi bado tunaluwa tupo shule ya msing au secondary naona kunautata hapa kidogo nisaidie mkuu sijui kama bado nipo ndan ya mada au nimetoka.
thanks in advance.
Wana-JF,karibuni hapa kwa maswali mbalimbali yahusuyo Sheria ya Ndoa,1971.Wale wote waliopo kwenye ndoa na wanaotarajia kuwa kwenye ndoa wanakaribishwa hapa kuuliza na kujibiwa. Nitashirikiana na Mawakili Wasomi wenzangu waliopo humu kuwajibu maswali yenu.
Mods, mnaweza kuufanya uzi huu kuwa 'sticky'? Asanteni na karibuni!
Sheria ya ndoa inamsaidiaje pale ambapo mmoja wa wanandoa anaamua kuondoka nakumuacha mwenzake na pia mambo mengine yote yanakuwa yako vizuri kiasi kwamba hawezi sema ameachwa pasi na mahitaji yake ya kimaisha na yule alie muacha hana shida na mali walizopata na kwamba yule alieachwa anaweza kuishi kwa mali hizo pasipo shida. Je sasa huyu ambaye anaona kwamba mwzenzake anamuacha kwa maksudi, je sheria hii inamsaidiaje ili asiachwe? kwa mtazamo wangu sheria hii ya ndoa imekaa style ya kulinda mslahi (Material things) na sio kulinda hiyo Union isivunjike pale mmoja anapokuwa kaamua kumkimbia menzake na ukizingatia hakuna adhabu hazieleweki na ni kama hakuna adhabu ambayo inaweza kumzuia mmoja wao kuogopa kuvuruga ndoa hiyo kabla mahakama haijatoa talaka.
kwa mtazamo huo huo mimi nionavyo nguvu ya kulinda ndoa isivunjike atleast iko kwa wazazi lakini sheria ya ndoa na serikali haina 'meno' ya kulinda ndoa isisambaratike zaidi ya kutetea maslahi pekee, japokuwa serikali itagoma kutoa talaka lakini je pale mmoja anapokuwa hajali cha talaka na kuamua kwenda aendako sheria inasaidia vipi
hebu fafanua mwanasheria
Mkuu,mimi nijibu swali gani ikiwa umeuliza na kujibu mwenyewe?
Wana-JF,karibuni hapa kwa maswali mbalimbali yahusuyo Sheria ya Ndoa,1971.Wale wote waliopo kwenye ndoa na wanaotarajia kuwa kwenye ndoa wanakaribishwa hapa kuuliza na kujibiwa. Nitashirikiana na Mawakili Wasomi wenzangu waliopo humu kuwajibu maswali yenu.
Mods, mnaweza kuufanya uzi huu kuwa 'sticky'? Asanteni na karibuni!
Vipi mkuu procedures za kuvunja ndoa ambapo mmoja wa wanandoa ameshaenda zake na kufunga ndoa na mtu mwingine wakati ndoa ya awali bado haijavunjwa rasmi. utaratibu lazima kuanzia huko kwenye baraza la wazee au unaweza kwenda moja kwa moja mahakamani?
Pia naomba kujua maximum penalty kwa mtu kufunga ndoa nyingine wakati ndoa ya awali haijavunjwa kisheria