Sheria zinasemaje kuhusu Polisi kuvamia ubalozi na kukamata mtu bila ruhusa ya balozi husika?

Sheria zinasemaje kuhusu Polisi kuvamia ubalozi na kukamata mtu bila ruhusa ya balozi husika?

Unaelewa sheria za kimataifa zinasemaje kuhusu kinga ya kibalozi?

Unaelewa kwa nini Julian Assange alikuwa kakaa kwenye ubalozi wa Ecuador Uingereza kwa miaka mingi tu, wakati Polisi wa Uingwreza wanataka kumkamata?

Unaelewa kwa nini Polisi wa Uingereza walishindwa kumkamata Julian Assange ingawa alikuwa kwenye ubalozi wa Ecuador nchini Uingereza uliopo London?
Kichwa panzi hicho.
 
Hapo hakuna shida yoyote kwani sheria za ndani ya nchi zinazohusiana na ukamataji zinahusika

Huyu asylum seeker angekuwa ameingia ndani ya ofisi ya ubalozi wa nchi yoyote basi VIENNA CONVENTION ON DIPLOMATIC RELATIONS ingetumika na ingeonekana yupo nje kwenye ikulu ya nchi nyingine na angekuwa na immunity ya kukatwa

Lakini eneo alilokamatiwa ni nje ya balozi zaidi ya moja na eneo hilo hakuna balozi hata mmoja itadai ni eneo lake hivyo eneo hilo lupo ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na hivyo municipal law haziwezi kuingiliwa kwa kuwa alikuwa bado hajafika kwenye ubalozi wa nchi yoyote
 
Weka picha
Poa
FB_IMG_1604065127033.jpeg
 
Unaelewa sheria za kimataifa zinasemaje kuhusu kinga ya kibalozi?

Unafahamu mkataba wa Vienna, ambao Tanzania inetia sahihi, unasemqje kuhusu majengo ya ubalozi kutoingiliwa na nchi yaliyomo?

Unaelewa kwa nini Julian Assange alikuwa kakaa kwenye ubalozi wa Ecuador Uingereza kwa miaka mingi tu, wakati Polisi wa Uingwreza wanataka kumkamata?

Unaelewa kwa nini Polisi wa Uingereza walishindwa kumkamata Julian Assange ingawa alikuwa kwenye ubalozi wa Ecuador nchini Uingereza uliopo London?

Diplomatic premises

It is an absolute rule that the premises of the mission are inviolable and agents of the receiving state cannot enter them without the consent of the mission. The receiving state is under a special duty to protect the mission premises from intrusion or damage or "impairment of its dignity".

[/URL]
Mkuu yaani huyo ni sawa na kumpigia mbuzi sebene, ataendelea kulia meee... Yaani wanachofahamu ni kile walichokaririshwa lumumba basi.
 
Kiutaratibu naona jeshi la Polisi ni kama wamefanya uvamizi nje ya ubalozi wa Ujerumani na kukamata mtu akiwa kwenye ombi la kuonana na balozi husika. Mbaya zaidi balozi wa Ujerumani nchini hakuwa na taarifa hizo.

Sijui sheria zinasemaje ila nahisi jambo hili litazua hisia sana kutoka kwa pande mbalimbali.

Hata kule Twitter nimeona reaction ya juu sana juu ya jambo hili.

Any way tusubiri tushuhudie yafuatayo.
Ulitakiwa kwanza uulize ni ipi mipaka ya dola kwenye dola yake yenyewe kwa dhati yake, kisha ukipewa majibu ndiyo uulize swali hilo.
 
Sheria gani, kwani huo ubalozi upo kwenye chupi ya hamisa, hii Ni nchi Tena huru. Tunawakamata hata mkiwa mnafanya ngono
Mkuu sheria za kimataifa Barozi ya nchi flani ni sawa na nchi husika, ndiyo maana Bwana Asange wa wikileaks alipokimbilia kwenye barozi ya Ecuardo uliopo Uingereza japo serikali ya Uingereza na Marekani walikuwa wanamtaka, Ecuardo ikagoma kumwachia aliendelea kuishi humo bila kutoka kwa kipindi cha miaka kadhaa mpaka pale walipokubariana kumkabidhi.
Kama walitaka kumkamata wangeweza kumkamata akitoka au asingetoka basi angeendelea ukaa humo ila siku akitoka hata iwe airport angekamatwa.
 
Halitorudi hata kushukuru kwa elimu aliyopatiwa kuhusu nguvu ya ubalozi maana akili yake inawaza chupi za hamisa/
 
Hapo hakuna shida yoyote kwani sheria za ndani ya nchi zinazohusiana na ukamataji zinahusika

Huyu asylum seeker angekuwa ameingia ndani ya ofisi ya ubalozi wa nchi yoyote basi VIENNA CONVENTION ON DIPLOMATIC RELATIONS ingetumika na ingeonekana yupo nje kwenye ikulu ya nchi nyingine na angekuwa na immunity ya kukatwa

Lakini eneo alilokamatiwa ni nje ya balozi zaidi ya moja na eneo hilo hakuna balozi hata mmoja itadai ni eneo lake hivyo eneo hilo lupo ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na hivyo municipal law haziwezi kuingiliwa kwa kuwa alikuwa bado hajafika kwenye ubalozi wa nchi yoyote
Hata hivyo walikuwa wanainusuru balozi hio kwa kuwa mtuhumiwa alikuwa anaenda pale bila appointment yeyote. Pengine alikuwa anaenda kulipua hivyo serkali ya ujerumani itoe shukrani kwa intellegensia ya Tz.
 
Sijui kwa sheria yetu lakini ubalozi hua unakua treated kama nchi yaani mfano ubalozi wa Kenya ukiwa Mwananyamala plot A hiyo plot inahesabiwa ni Kenya so mamlaka za Tz zinahitaji ruhusa kuoperate.

Niliwahi kusoma kesi moja ya ofisa mmoj wa ubalozi alimchoma moto mkewe ndani ya ubalozi na askari wa ile nchi wakabaki kuangalia as kuingilia ingekua ni kuanzisha ugomvi (Ni Malaysia au Thailand sikumbuki vizuri)

Pia kuna jamaa humu jf alielezea machafuko ya Rwanda yeye akiwa anafanya kazi ubalozini na akaelezea wenyeji walivyokua wanakimbilia ubalozini na waasi walikua wanachagua watu wao na kuwaacha wafanyakazi wa ubalozi.

So yeah pengine hata hakua ameingia ndani bado
 
Hata hivyo walikuwa wanainusuru balozi hio kwa kuwa mtuhumiwa alikuwa anaenda pale bila appointment yeyote. Pengine alikuwa anaenda kulipua hivyo serkali ya ujerumani itoe shukrani kwa intellegensia ya Tz.
Ni kweli angeenda kuleta maana huko ndani au kuandamana huko angesababisha chaos kwenye balozi hizo na kwa mujibu wa sheria hiyo ya viena receiving state ina wajibu wa kuhakikisha jengo la ubalozi ama balozi familia yake na wafanyakazi wake hawabughudhiwi na wala havamiwi na watu hatari (radicals)
 
Back
Top Bottom