Sheria zinasemaje kuhusu Polisi kuvamia ubalozi na kukamata mtu bila ruhusa ya balozi husika?

Sheria zinasemaje kuhusu Polisi kuvamia ubalozi na kukamata mtu bila ruhusa ya balozi husika?

Madhara ya elimu bure,hujui ubalozi ni ardhi ya nchi ya ubalozi huo? Nenda shule
Basi wangesema ubalozi wa ujerumani chini ujerumani na wasituambie ubalozi wa ujerumani chini Tanzania wanamiliki Vipi ARDHI yetu wakati tunao uwezo wa kufukuza ubarozi wao muda wowote na wakafungasha virago..?
 
Kuna watu wanajifunza hapa.

Kaka sio kila mtu ana mtazamo pevu na ukomavu kama wewe. Unaangalia jambo kwa maslahi mapana, haufungwi kwenye kupambana na unaemjibu, watu wengi wanafuatilia mjadala na wataona tofauti na kupata shule ambayo inaweza kuwasaidia sana mbeleni.

Kwa kuwaongezea tu, hata mfanyakazi wa kigeni/ ubalozi mwenye hashi ya diplomat akuwa kwenye majukumu yake analindwa na makubaliano ya mkataba wa Vienna.
 
Hawajamwachia bure. Walichukuwa mafurushi na video za kugushi alizokuwa anapeleka huko.
Na pasi ya kusafiria pia, abaki hapa tucheze nae kisawasawa
 
Wahalifu wote wakikimbilia kusimama mbele ya balozi hawatakamatwa? Hebu fafanua

Achilia mbali kusimama mbele ya ubalozi, hata wakiingia ndani wanaweza kufikishwa mbele ya sheria. Kinachoongelewa hapa ni utaratibu wa kuwakamata. Kuna mchakato wake.

Polisi hawawezi kwenda kupekua/ kuingia au kukamata mtu kwenye eneo la ubalozi wa nchi nyingine bila hizo taratibu walizojiwekea kimataifa kuzingatiwa.

Sio sahihi kufikiria ukifanya uhalifu suluhu na kukwepa sheria ni kukimbilia ubalozini, itachelewesha mchakato lakini haukwepi au kukingwa na hukumu.
 
Achilia mbali kusimama mbele ya ubalozi, hata wakiingia ndani wanaweza kufikushwa mvele ya sheria. Kinachoongelewa hapa ni utaratibu wa kywakamata. Kuna mchakato wake.

Polisi hawawezi kwenda kupekua/ kuingia au kukamata mtu kwenye eneo la ubalozi wa nchi nyingine bila hizo taratibu walizojiwekea kimataifa kuzingatiwa.

Sio sahihi kufikiria ukifanya uhalifu suluhu na kukwepa sheria ni kukimbilia ubalozini, itachelewesha mchakato lakini haukwepi au kukingwa na hukumu.
Umeeleweka mkuu
 
Unajiuliza swa;li na kujijibu! Huyo alikamatwa nje na siyo ndani. Baada ya kuchukuwa nyaraka zake za uongo wakamuachia.
Kwa ufahamu wako wa maswali na majibu upo sahihi. Labda tu kwa kukusaidia hizo nyaraka za uongo ulishazithbiitisha?
 
Kiutaratibu naona jeshi la Polisi ni kama wamefanya uvamizi nje ya ubalozi wa Ujerumani na kukamata mtu akiwa kwenye ombi la kuonana na balozi husika. Mbaya zaidi balozi wa Ujerumani nchini hakuwa na taarifa hizo.

Sijui sheria zinasemaje ila nahisi jambo hili litazua hisia sana kutoka kwa pande mbalimbali.

Hata kule Twitter nimeona reaction ya juu sana juu ya jambo hili.

Any way tusubiri tushuhudie yafuatayo.
Akiwaje nje ya ubalozi hapo bado ni TZ mkuu jitahidini kujifunza mambo kabla ya kutoa lawama tu. Malalamiko FC!
 
Bora kuficha ujinga wako kuliko kujinadi hadharani ulivyo mjinga.
Toa hoja mkuu. Ubalozi mpaka uwe ndani siyo pale nje kwenye lile jesho la Umoja wa EU. Jitahidi kujifunza ili uelewe. Poleni Malalamiko FC
 
Pilipili usioila yakuwashia nini? Kama ni kosa wapo wahusika ambao ni Ujeremani, sasa nyie wajuaji mnajitia mnajuwa zaidi kuliko ubalozi. Kwani Ujeremani hawajui kilichotokea na kimetokea vipi. Kama wanajuwa tutawasikia nyie acheni kuchonga midomo. Kura mmekosa na kula mmekosa.
Umesoma ukaelewa pointi yangu au umetoka kwenye siku zako unatafuta bwana.
Ningeweza kukuelewesha ila kwa sababu unajifanya mjuaji kaa na ujinga wako.
 
Kaka sio kila mtu ana mtazamo pevu na ukomavu kama wewe. Unaangalia jambo kwa maslahi mapana, haufungwi kwenye kupambana na unaemjibu, watu wengi wanafuatilia mjadala na wataona tofauti na kupata shule ambayo inaweza kuwasaidia sana mbeleni.

Kwa kuwaongezea tu, hata mfanyakazi wa kigeni/ ubalozi mwenye hashi ya diplomat akuwa kwenye majukumu yake analindwa na makubaliano ya mkataba wa Vienna.
Upo sahihi . JF ni darasa tosha kwa wale walio makini. Tatizo ni pale ufahamu wa mtu katika jambo husika unapopambanishwa na ushabiki wa kiitikadi. Hapo lazima kiswahili kigeuke kichina.
 
Acheni upotoshaji, sheria inakataza polisi kukamata mtu akishaingia ndani ya ubalozi na si vinginevyo.
Kama Tundu Lissu angekuwa ameingia ndani ya ubalozi na polisi wakamkamata wangechukuliwa hatua kwani ukishaingia ubalozini umeingia taifa jingine lakini sivyo kama mtoa mada unavyopotosha.
Nje ya Jengo la Umoja wa EU siyo ubalozini hapo unaweza kukamatwa tu bado ni TZ hiyo hadi uingie ofisini ama kwenye makazi ya balozi siyo getini. Tatizo la Malalamiko FC wanajidai wanajua kila kitu kumbe ni mbumbumbu wa karne ya 21.
 
Kiutaratibu naona jeshi la Polisi ni kama wamefanya uvamizi nje ya ubalozi wa Ujerumani na kukamata mtu akiwa kwenye ombi la kuonana na balozi husika. Mbaya zaidi balozi wa Ujerumani nchini hakuwa na taarifa hizo.

Sijui sheria zinasemaje ila nahisi jambo hili litazua hisia sana kutoka kwa pande mbalimbali.

Hata kule Twitter nimeona reaction ya juu sana juu ya jambo hili.

Any way tusubiri tushuhudie yafuatayo.
Ubalozi ndo unamficha mharifu anayetaka kulipua petrol station! Na akamatwe tu.
 
Kama hujui kitu uliza utapata aibu...ukisikia ubalozi wa nchi fulani jua ile sehemu inawakilisha taifa husika hivyo kisheria huwezi kufanya chochote mpaka uwataarifu kinyume na hivyo ni sawa umeingilia nchi ya watu.
Sheria gani, kwani huo ubalozi upo kwenye chupi ya hamisa, hii Ni nchi Tena huru. Tunawakamata hata mkiwa mnafanya ngono
 
Sheria gani, kwani huo ubalozi upo kwenye chupi ya hamisa, hii Ni nchi Tena huru. Tunawakamata hata mkiwa mnafanya ngono
Iko wapi ile CCM yetu ya zamani mahiri kwenye kujenga hoja sio hawa wa mambo ya kihuni. Inaaibisha turudishe watu wenye akili wapambane kwa nidhamu
 
Kiutaratibu naona jeshi la Polisi ni kama wamefanya uvamizi nje ya ubalozi wa Ujerumani na kukamata mtu akiwa kwenye ombi la kuonana na balozi husika. Mbaya zaidi balozi wa Ujerumani nchini hakuwa na taarifa hizo.
ukiwa nje ya ubalozi ni bado hujaingia kwenye himaya ya ubalozi
polisi walikua sahihi na ndio mana mabeberu wapo kimya kwa hilo
 
niliwahi kusikia ubalozi ni mali ya nchi ambayo ina ofisi hapo hivyo kwa sheria za kimataifa eneo la ubalozi wa nchi hiyo sio Tanzania hapo
 
Back
Top Bottom