Shetani ameaibika tena! Alituma mtu aibe 'assets' zangu zenye thamani ya dola 5000, amenaswa!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Ndugu zangu, mara kwa mara nimekuwa nikiwasimulia humu mambo makuu anayonitendea Mungu maishani mwangu. Leo tena nawaletea ushuhuda wa kweli, kweli tupu, jinsi Mungu alivyoniwezesha kupata 'assets' zangu zilizokuwa zimeibwa na ajenti wa shetani(ibilisi).

Ilikuwa hivi: Hivi majuzi, mimi na rafiki zangu tulikuwa kwenye shughuli fulani muhimu, kuanzia asubuhi hadi mchana. Baada ya kukamilisha shughuli hiyo, tuliingia katika hoteli fulani ili tupate chakula. Siku hiyo nilikuwa na begi dogo lenye assets zenye thamani ya dola takriban 5,000. Baada ya kuingia hotelini pale, tulikaa kwenye viti kisha begi hilo nikaliweka chini ya meza. Tukatoa order ya kuletewa vyakula vitamu. Tukala, tukafurahia maisha. Baada ya kula, mimi nikaagana na wale marafiki. Nika-drive gari yangu, nikaondoka. Sikukumbuka kwamba nimeacha begi chini ya meza!

Shetani ni mwizi. Nilivyoondoka tu pale, alituma mtu, akalichukua lile begi akatoka nalo nje. Baada ya dakika kama moja hivi nikiwa naendesha gari, nikakumbuka nimesahau begi langu hotelini chini ya meza! Nikasimamisha gari, nikampigia simu mmoja wa wale marafiki zangu niliokuwa nao hotelini kumweleza kuwa nimesahau begi langu hotelini.

Akaniambia hivi: yeye na wenzake hawakufanya haraka kuondoka pale nje ya hoteli. Walipokuwa bado wapo pale, walimuona mtu ametoka ndani ya hoteli akiwa amebeba lile begi. Rafiki yangu huyo alipoliona lile begi alitambua ni la kwangu. Akamsogelea yule mtu(mwizi aliyetumwa na shetani kuiba) na kumwambia kwa ujasiri: "Hili begi sio lako. Kama unabisha tuambie ndani ya begi kuna nini." Yule mtu akashikwa na kigugumizi, akashindwa kutaja assets zilizokuwa ndani ya begi, akamwachia huyo rafiki yangu hilo begi.

Baada ya kusikia habari hizo njema, nikamshukuru Mungu, kisha nikageuza gari langu na kurudi hadi pale nje ya hoteli, nikamkuta huyo rafiki akanipatia begi langu.

Yule mwizi kama angeweza kuishia nalo hilo begi, angeuza hizo assets fasta sana maana hazipatikani kwa urahisi na watu wengi wanazihitaji.

Mimi Setfree, Setfree, Ee Mungu ninakusifu, Ee Mungu nakutukuza. Ulilinda begi langu...
 
Ndugu zangu hii ni mojawapo ya faida za kuokoka na kuishi na Yesu. Yesu alisema atakuwa pamoja nasi hata ukamilifu wa dahari(Mt 28:20). Yesu anapokuwa nasi, anatupatia baraka nyingi, pamoja na ulinzi na ushindi dhidi ya adui shetani. Nawasikitikia wanaosema eti Mungu hayupo. Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini(Zab 34:8). Haleluya!
 
Katika Zaburi 121:7–8 Mungu ameahidi hivi:
“Bwana atakulinda na uovu wote; Atakulinda nafsi yako. Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.”

Kwa kuzingatia ahadi hiyo, kabla sijalala lazima niombe ulinzi wa Mungu. Na pia kila nikiamka, siachi kumshukuru Mungu kwa ulinzi wake usiku kucha na kujikabidhi mikononi mwake tena anilinde safarini na kulinda vyote nilivyo navyo nyumbani, ofisini nk. Kwa njia hii nimekuwa nikiona ulinzi wa Mungu ukinifunika siku baada ya siku.
 
Ndugu zangu, mara kwa mara nimekuwa nikiwasimulia humu mambo makuu anayonitendea Mungu maishani mwangu. Leo tena nawaletea ushuhuda wa kweli, kweli tupu, jinsi Mungu alivyoniwezesha kupata 'assets' zangu zilizokuwa zimeibwa na ajenti wa shetani(ibilisi).

Ilikuwa hivi: Hivi majuzi, mimi na rafiki zangu tulikuwa kwenye shughuli fulani muhimu, kuanzia asubuhi hadi mchana. Baada ya kukamilisha shughuli hiyo, tuliingia katika hoteli fulani ili tupate chakula. Siku hiyo nilikuwa na begi dogo lenye assets zenye thamani ya dola takriban 5,000. Baada ya kuingia hotelini pale, tulikaa kwenye viti kisha begi hilo nikaliweka chini ya meza. Tukatoa order ya kuletewa vyakula vitamu. Tukala, tukafurahia maisha, Baada ya kula, mimi nikaagana na wale marafiki. Nika-drive gari yangu, nikaondoka. Sikukumbuka kwamba nimeacha begi chini ya meza!

Shetani ni mwizi. Nilivyoondoka tu pale, alituma mtu, akalichukua lile begi akatoka nalo nje. Baada ya dakika kama moja hivi nikiwa naendesha gari, nikakumbuka nimesahau begi langu hotelini chini ya meza! Nikasimamisha gari, nikampigia simu mmoja wa wale marafiki zangu niliokuwa nao hotelini kumweleza kuwa nimesahau begi langu hotelini.

Akaniambia hivi: yeye na wenzake hawakufanya haraka kuondoka pale nje ya hoteli. Walipokuwa bado wapo pale, walimuona mtu ametoka ndani ya hoteli akiwa amebeba lile begi. Rafiki yangu huyo alipoliona lile begi alitambua ni la kwangu. Akamsogelea yule mtu(mwizi aliyetumwa na shetani kuiba) na kumwambia kwa ujasiri: "Hili begi sio lako. Kama unabisha tuambie ndani ya begi kuna nini." Yule mtu akashikwa na kigugumizi, akashindwa kutaja assets zilizokuwa ndani ya begi, akamwachia huyo rafiki yangu hilo begi.

Baada ya kusikia habari hizo njema, nikamshukuru Mungu, kisha nikageuza gari langu na kurudi hadi pale nje ya hoteli, nikamkuta huyo rafiki akanipatia begi langu.

Yule mwizi kama angeweza kuishia nalo, angeuza hizo assets fasta sana maana hazipatikani kwa urahisi na watu wengi wanazihitaji.
Sasa shetani kaingiaje hapo? Yani uzembe wako unamsingizia shetani?
 
Ni kweli hata mimi juzi shetani kaumbuka vibaya sanaa.. Nilikua naendesha gari niko spidi 180 na mbele yangu kuna makutano na taa nyekundu imewaka kuashiria nisimame. Basi mimi sikusimama nikanyoosha na hizo hizo spidi. Mungu mkubwa nilipita salama salmini wala hakuna gari iliyonigonga. Shetani akaumbuka maana alitaka nipate ajali.
 
Sasa shetani kaingiaje hapo? Yani uzembe wako unamsingizia shetani?
Watu tukiwaambia msome Biblia mnasema ni kitabu kilichotungwa na watu.
Soma Luka 22:3. Imeandikwa hivi:
"Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskarioti..."
Baada ya shetani kumwingia Yuda, Yuda alipata ujasiri wa kumsaliti Yesu. Mtu wa kawaida hana ujasiri wa kuvunja nyumba na kuiba - ni mpaka aingiwe na shetani au mapepo yake. Shetani ni mwizi. Tabia hiyo ya wizi ndiyo anayowawekea wale anaowaingia! Wanaendeleza kazi zake mbovu.
 
hivi huwezi kuokoka na ukakaa kimya ikawa ni faida yako binafsi ni mpaka upige makeleleeee uwatangazie watu
Waliookoka kabla yangu kama wangekaa kimya na kuacha kupiga kelele, mimi nisingeokoka. Ningezama na kufa dhambini.

By the way, ni agizo la Yesu. Mtu ukiishaokoka unatakiwa uwaambie na wengine habari njema za wokovu. Hapa JF kuna nyuzi nyingi za watu wanaoteswa na dhambi. Wengine wanatamani kuacha ulevi wanashindwa. Wengine hawana furaha kwenye ndoa zao. Wengine wanaogopa wakisikia mabundi yanalia usiku. Mtu mwenye upendo, anayejali watu na aliye free from such bondage, hawezi kukaa kimya. Atatafuta kila njia ya kupiga kelele ili watu kama hao wajue jinsi ya kuondokana na adha walizo nazo; wawekwe huru mbali na mateso waliyo nayo. Hata Waswahili wanasema: "Kizuri kula na mwenzio" Tuache uchoyo na ubinafsi. Ila kama wewe ni ajenti wa shetani, pole. Lazima uchukie ukisikia nambagaza shetani.
 
Ndugu zangu, mara kwa mara nimekuwa nikiwasimulia humu mambo makuu anayonitendea Mungu maishani mwangu. Leo tena nawaletea ushuhuda wa kweli, kweli tupu, jinsi Mungu alivyoniwezesha kupata 'assets' zangu zilizokuwa zimeibwa na ajenti wa shetani(ibilisi).

Ilikuwa hivi: Hivi majuzi, mimi na rafiki zangu tulikuwa kwenye shughuli fulani muhimu, kuanzia asubuhi hadi mchana. Baada ya kukamilisha shughuli hiyo, tuliingia katika hoteli fulani ili tupate chakula. Siku hiyo nilikuwa na begi dogo lenye assets zenye thamani ya dola takriban 5,000. Baada ya kuingia hotelini pale, tulikaa kwenye viti kisha begi hilo nikaliweka chini ya meza. Tukatoa order ya kuletewa vyakula vitamu. Tukala, tukafurahia maisha. Baada ya kula, mimi nikaagana na wale marafiki. Nika-drive gari yangu, nikaondoka. Sikukumbuka kwamba nimeacha begi chini ya meza!

Shetani ni mwizi. Nilivyoondoka tu pale, alituma mtu, akalichukua lile begi akatoka nalo nje. Baada ya dakika kama moja hivi nikiwa naendesha gari, nikakumbuka nimesahau begi langu hotelini chini ya meza! Nikasimamisha gari, nikampigia simu mmoja wa wale marafiki zangu niliokuwa nao hotelini kumweleza kuwa nimesahau begi langu hotelini.

Akaniambia hivi: yeye na wenzake hawakufanya haraka kuondoka pale nje ya hoteli. Walipokuwa bado wapo pale, walimuona mtu ametoka ndani ya hoteli akiwa amebeba lile begi. Rafiki yangu huyo alipoliona lile begi alitambua ni la kwangu. Akamsogelea yule mtu(mwizi aliyetumwa na shetani kuiba) na kumwambia kwa ujasiri: "Hili begi sio lako. Kama unabisha tuambie ndani ya begi kuna nini." Yule mtu akashikwa na kigugumizi, akashindwa kutaja assets zilizokuwa ndani ya begi, akamwachia huyo rafiki yangu hilo begi.

Baada ya kusikia habari hizo njema, nikamshukuru Mungu, kisha nikageuza gari langu na kurudi hadi pale nje ya hoteli, nikamkuta huyo rafiki akanipatia begi langu.

Yule mwizi kama angeweza kuishia nalo hilo begi, angeuza hizo assets fasta sana maana hazipatikani kwa urahisi na watu wengi wanazihitaji.

Shetani anaweza kuwa Mwizi, ila na wewe ni Mzembe; Ni either una ujinga au Kuna namna unatupanga kwa Melengo fulani
 
Back
Top Bottom