Shetani ameaibika tena! Alituma mtu aibe 'assets' zangu zenye thamani ya dola 5000, amenaswa!

Shetani ameaibika tena! Alituma mtu aibe 'assets' zangu zenye thamani ya dola 5000, amenaswa!

Ninapoandika uzi wowote nazingatia sana Andiko hili:
Wakolosai 3:9-10
"Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; mkivaa utu mpya, unaofanywa upya katika ufahamu kulingana na mfano wake yeye aliyeuumba."

Hivyo usitarajie chai kwenye nyuzi zangu. Sitaki kuikosa mbingu kwa sababu ya uongo.
 
Amina mtumishi nataka niombewe na Mimi
Nilikuambia utaje hapa mahitaji yako nami nitakuombea.
Yesu anajua unayohitaji lakini anataka uyaseme.
Mk 10:51
"Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona."
 
Hakika heri wale ambao Yesu ni Bwana na mwokozi wa maisha yao(waliokoka kweli)
Ndugu zangu hii ni mojawapo ya faida za kuokoka na kuishi na Yesu. Yesu alisema atakuwa pamoja nasi hata ukamilifu wa dahari(Mt 28:20). Yesu anapokuwa nasi, anatupatia baraka nyingi, pamoja na ulinzi na ushindi dhidi ya adui shetani. Nawasikitikia wanaosema eti Mungu hayupo. Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini(Zab 34:8).
 
Nilikuambia utaje hapa mahitaji yako nami nitakuombea.
Yesu anajua unayohitaji lakini anataka uyaseme.
Mk 10:51
"Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona."
Nataka nikuoe
 
Hongera Sana mkuu, umechagua fungu lililo jema!
Na wewe chagua fungu hilo kama bado hujafanya hivyo. Neno la Mungu ni tamu kuliko asali.
Zaburi 119:103
"Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu, matamu kuliko asali katika kinywa changu!"

Shetani amepofusha akili za watu wengi na kuwafanya wasisome Biblia ili wakose "nondo" zilizomo kwenye Biblia.
2 Wakorintho 4:4
"...mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu."
 
Napenda, lkn mambo ya dunia yamenizonga, nakimbizana na maokoto!
 
Shetani ni malaika aliyeasi dhidi ya Mungu kwa kiburi na uasi,
Alitowa wapi mawazo maovu kiasi hiki ikiwa kule juu ni kusifu na kuabudu? Je kuna mahali aliona akatamani/kujifunza uasi?
 
Napenda, lkn mambo ya dunia yamenizonga, nakimbizana na maokoto!
Siku hizi kuna Biblia mpaka za audio. Ukiwa kwenye gari lako unaweza kusikiliza Neno wakati una-drive. Hivyo kukimbizana na maokoto sio sababu ya msingi tena ya kutoweza kujifunza Neno la Mungu.
 
Back
Top Bottom