Shetani ameaibika tena! Alituma mtu aibe 'assets' zangu zenye thamani ya dola 5000, amenaswa!

Alafu shetani ni nini? @Setfree
Shetani ni kiumbe wa kiroho anayejulikana kama adui wa Mungu na mwanadamu katika imani nyingi za kidini.

Kwa Wakristo: Shetani ni malaika aliyeasi dhidi ya Mungu kwa kiburi na uasi, akafukuzwa mbinguni. Tangu hapo anajulikana kama Ibilisi, na kazi yake ni kuwajaribu watu, kuwadanganya, na kuwaharibu wanadamu ili wamuasi Mungu (soma Isaya 14:12-15, Ezekieli 28:12-17, Ufunuo 12:9).

Majina yake mengine ni: Lusifa (kama ilivyotafsiriwa na wengine), Mjaribu, Adui, Mwangamizi, Mfalme wa giza.

Hizi ni tabia za Shetani (kulingana na Biblia):
  • Mdanganyaji (Yohana 8:44) – Anatambulika kuwa baba wa uongo.
  • Mjaribu (Mathayo 4:1-11) – Alimjaribu hata Yesu jangwani.
  • Mshitaki wa waaminio (Ufunuo 12:10).
  • Anajifanya kuwa malaika wa nuru (2 Wakorintho 11:14).
  • Anazunguka kama simba angurumaye akitafuta mtu wa kummeza (1 Petro 5:8).
Kwa ujumla, kulingana na mafundisho ya Biblia, Shetani anapinga kazi ya Mungu na hutafuta kuwaangamiza watu kwa kuwapotosha, kuwatia hofu, na kuwazuia kuijua kweli ya Mungu. Hatimaye, shetani ataangamizwa motoni milele pamoja na wanaomfuata (Ufunuo 20:10).
 
Acha tu mkuu, CCM ndie shetani anaezungumziwa hapa na mleta mada
Acha uongo Arizona 1
Waongo mbinguni hawaingii
Ufu 21:8
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
 
Hongera sana mkuu 🙏🙏🙏
 
Punguzeni kuingia kwenye maisha ya watu uokovu wako ni kwa faida yako mwenyewe.
 
Wewe ni mzembe,acha kumsingizia Shetani. Siku nyingine uache uzembe,sawa Setfree?
 
Sikusoma kiswahili, samahani kama kiswahili changu kinakufanya umkumbuke x wako!
Pole. Ila apps za Kiswahili zipo nyingi. Fanya bidii ujifunze Kiswahili fasaha.
Hizo stori za ma-X, nazisikia tu kwenu. Uzinzi na talaka ni marufuku kwangu.
 
Mkuu Setfree unawezaje kujibu comments za watu huku ukirejea vifungu vya ujumbe husika Kwa haraka haraka hivi? Je biblia nzima umeiweka kichwani kiasi cha kujua kila andiko na mahala linapopatikana?
 
Wewe na Mimi wote baba yetu ibilisi....umeridhika
Ah wapi. Shetani ninavyombagaza hivi awe baba yangu?
2 Kor 6:14-15
"...pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?..."
 
Mkuu Setfree unawezaje kujibu comments za watu huku ukirejea vifungu vya ujumbe husika Kwa haraka haraka hivi? Je biblia nzima umeiweka kichwani kiasi cha kujua kila andiko na mahala linapopatikana?
Biblia kwangu ni chakula. Nimeisoma sura kwa sura kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo, zaidi ya mara tatu. Hivyo ukisema jambo lolote nakumbuka haraka mstari/kifungu cha kukupatia.
Kol 3:16-17
"Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu..."
 
Duh. Huu kama sio ulafi ni nini?
Gal 5:21
"... husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu."
 
Duh. Huu kama sio ulafi ni nini?
Gal 5:21
"... husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu."
Chai ongeza sukari
 
Hongera Sana mkuu, umechagua fungu lililo jema!
 
Wewe ni mzembe,acha kumsingizia Shetani. Siku nyingine uache uzembe,sawa Setfree?
Tafakari andiko hili kabla ya ku-comment:
Yak 1:19-27
"...ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema.."

Forgetting something does not automatically make a person careless(mzembe). To forget is a human limitation that can happen even to the most responsible individuals. Carelessness(uzembe), on the other hand, implies a lack of concern, negligence, or disregard for responsibility. In my case, leaving the bag behind wasn’t due to neglect. So let’s be fair in our judgments: forgetting is not a moral failure, it’s simply part of being human. If forgetting a bag makes someone careless, then the whole world is full of careless people—because I doubt anyone has gone through life without ever forgetting something.
 
Amina mtumishi nataka niombewe na Mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…