Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Wewe shetani. Kwanini unawaonea watu? Watu wanateseka, hawana kazi, hawana pesa, maisha yamekuwa magumu. Wakitazama TV, wanakutana na habari za vita, mauaji, majanga na dhiki kila mahali. Badala ya kuwaachia hata pumzi kidogo, unawaongezea maumivu. Unawatupia mapepo yanayowatesa kwa magonjwa yasiyojulikana - magonjwa yanayowafanya walie usiku na mchana, magonjwa yanayowachosha na kuwafanya waanze kumtukana Mungu. Halafu unachekelea unapowaona wanalia kama watoto. 👉We-wee!
Mbaya zaidi unawadanganya! Unawaambia magonjwa hayo yatapona yenyewe kwa antibodies, wakati unajua kabisa kwamba antibodies haziwezi kupambana na mapepo! Unawaambia watulie, wasubiri miili yao ijiponye yenyewe. Badala ya kupona, hali zao zinazidi kuwa mbaya. Maumivu yanaongezeka, afya inadorora, na matumaini yanazimika.
Wanakimbilia hospitali, madaktari wanaanza kazi ya kupima. Wanatumia: Thermometer, Stethoscope, Sphygmomanometer, Pulse Oximeter, Hematology Analyzer, Blood Glucose Meter, ELISA Machine, PCR Machine, Urinalysis Analyzer, X-ray Machine, CT Scan, MRI, Ultrasound Machine, ECG, Echocardiogram, Spirometer, Peak Flow Meter, Otoscope, Laryngoscope, Nasal Endoscope, Ophthalmoscope, Slit Lamp, Tonometer... madaktari wanashangaa, duuh—vipimo havionyeshi ugonjwa wowote, lakini maumivu yapo, tena mazito! Wagonjwa wanaambiwa labda ni stress, labda ni mawazo, nendeni mkapumzike! Wagonjwa wanarudi nyumbani kwa huzuni, maana wanajua ndani yao kuna mzigo usio wa kawaida.
Wanakopa pesa, wanapanda "pipa" wanaenda "majuu." "Wathungu" wanatumia mitambo mikali zaidi kupima, lakini mambo ni yaleyale. Daktari anaandika: "No abnormality detected (NAD)!" Wanarudi "home" wamenyong'onyea, maana pesa imeliwa bila uponyaji!
Shetani unawapotosha tena, unawaelekeza kwa waganga wa kienyeji. Wanaenda, wanapewa masharti ya kuwafadhaisha zaidi. Eti wapeleke kuku na pesa. Wanapeleka, kisha wanapewa dawa za uongo na kuambiwa hizo dawa wakazimeze usiku makaburini. Maumivu yanazidi wanarudi tena kwa waganga, wanaambiwa eti wapeleke mbuzi na mavi ya tembo, watapata dawa kali zaidi! Waganga wanakula mbuzi bila jasho, wakati wagonjwa badala ya kupona, wanajikuta wakifungwa zaidi na minyororo yako shetani!
Magari ya matangazo yanapita mitaani yakitangaza: "Jamani Yesu anaponya buree. Waleteni wagonjwa mkutanoni, watapona kwa Jina la Yesu - bila chumvi wala mafuta feki ya upako..." Wagonjwa wanajipanga kuhudhuria mkutano. Unawadanganya tena. Unawaambia eti miujiza haipo, eti haiwezekani mtu kupona kwa maombi tu. Unawashawishi waone maombi ni ujinga, waone uponyaji wa Jina la Yesu kama hadithi tu!
Kwa Jina la Yesu Kristo, nakukemea! Acha kupotosha watu wa Mungu! Magonjwa yanayosababishwa na mapepo, hayawezi kuondoka kwa tiba za kibinadamu, hayawezi kupona kwa antibiotics, hayawezi kuponywa na miti shamba wala dawa za kisasa! Ni kwa Jina la Yesu pekee!
Shetani leo nimekufichua. Wewe ni mwongo! Ndiyo maana ulifukuzwa mbinguni; na leo nakufukuza! Toka hapa!
Kwa mamlaka niliyopewa na Yesu, nakuamuru shetani:
👉 Toka kwa Jina la Yesu. Toka na mapepo yako.
👉 Toka katika miili ya watu uliowaonea!
👉 Toka na roho zako chafu! Toka na magonjwa yako yote. Shindwa na ulegee.
Watu wote wanaoteswa na mapepo wawe huru sasa hivi, kwa Jina la Yesu Kristo. Amen!
======================
Almighty God, in accordance with Your divine proclamation in John 8:32, I give thanks, for this day, the truth has been unveiled to Your people, and by it, they have been set free. In the glorious Name of Jesus, Amen.