Shetani nakukemea: Acha kupotosha watu kwa habari za uongo

Shetani nakukemea: Acha kupotosha watu kwa habari za uongo

Waafrica tuna shida...Mungu awezi kua upande wa watu wajinga na wapumbavu
Mpumbavu ni mtu anayesema kuwa Mungu hayupo. Hata wanaosema mapepo hayapo wanaingia katika kundi hilohilo. Soma
Zaburi 53:1
 
Duh, kweli njia ya upotevuni ni pana. Mtu anathubutu kabisa kujiita kaka yake shetani? Sawa nuru imekuja amechagua giza.
Yohana 3:19
Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.
 
Mnaonaje tuungane kwa pamoja tumuombe Mungu amfutilie mbali shetani aache kutusumbua na asituzoee zoee😂😂
Maombi ni silaha yetu kuu dhidi ya maovu, ila tusisahau Neno la Mungu linatuambia tumpinge shetani naye atatukimbia (Yakobo 4:7). Tukizivaa sila zote (Waefeso 6:11-18) za kiroho na kuishi maisha matakatifu, shetani hawezi kupata nafasi ya kutuzoeazoea.

Shetani ameishaandaliwa moto wa milele. Siku si nyingi atafutiliwa mbali.

"Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, enyi mlio laaniwa, mwende katika moto wa milele aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake." (Mathayo 25:41)
 
Mungu akufunike kwa mbawa zake kama kuku anavyowafunika vifaranga wake.
Amen. Haleluya!
Hakika BWANA ananifunika kwa mabawa yake, napata usalama kwake; mkono wake unanilinda na kunikinga sawasawa na ahadi yake katika:
Zaburi 91:4
"Atakufunika kwa mabawa yake, utapata usalama kwake; mkono wake utakulinda na kukukinga."
 
To dismiss the eschatological reality of Satan's condemnation as an 'illusion' is to negate the explicit declarations found in divine scripture. The notion that the lake of fire is merely a figment of human imagination contradicts the unequivocal assertion of Matthew 25:41, where Christ Himself proclaims that 'the eternal fire [is] prepared for the devil and his angels.' This is not an allegorical construct nor a psychological projection, but a definitive pronouncement of divine judgment.

To perceive this as an illusion is to misunderstand the ontological structure of divine justice, wherein rebellion against the Almighty necessitates an eternal consequence. The apocalyptic literature of Revelation 20:10 further substantiates this: 'The devil who deceived them was thrown into the lake of burning sulfur... and they will be tormented day and night forever and ever.' This language is neither metaphorical hyperbole nor poetic imagery—it is a theologically precise declaration of Satan's ultimate fate.

Thus, to relegate this profound eschatological reality to the realm of illusion is not only a hermeneutical misstep but an evasion of the very fabric of divine revelation.
 
Wewe shetani. Kwanini unawaonea watu? Watu wanateseka, hawana kazi, hawana pesa, maisha yamekuwa magumu. Wakitazama TV, wanakutana na habari za vita, mauaji, majanga na dhiki kila mahali. Badala ya kuwaachia hata pumzi kidogo, unawaongezea maumivu. Unawatupia mapepo yanayowatesa kwa magonjwa yasiyojulikana - magonjwa yanayowafanya walie usiku na mchana, magonjwa yanayowachosha na kuwafanya waanze kumtukana Mungu. Halafu unachekelea unapowaona wanalia kama watoto. 👉We-wee!

Mbaya zaidi unawadanganya! Unawaambia magonjwa hayo yatapona yenyewe kwa antibodies, wakati unajua kabisa kwamba antibodies haziwezi kupambana na mapepo! Unawaambia watulie, wasubiri miili yao ijiponye yenyewe. Badala ya kupona, hali zao zinazidi kuwa mbaya. Maumivu yanaongezeka, afya inadorora, na matumaini yanazimika.

Wanakimbilia hospitali, madaktari wanaanza kazi ya kupima. Wanatumia: Thermometer, Stethoscope, Sphygmomanometer, Pulse Oximeter, Hematology Analyzer, Blood Glucose Meter, ELISA Machine, PCR Machine, Urinalysis Analyzer, X-ray Machine, CT Scan, MRI, Ultrasound Machine, ECG, Echocardiogram, Spirometer, Peak Flow Meter, Otoscope, Laryngoscope, Nasal Endoscope, Ophthalmoscope, Slit Lamp, Tonometer... madaktari wanashangaa, duuh—vipimo havionyeshi ugonjwa wowote, lakini maumivu yapo, tena mazito! Wagonjwa wanaambiwa labda ni stress, labda ni mawazo, nendeni mkapumzike! Wagonjwa wanarudi nyumbani kwa huzuni, maana wanajua ndani yao kuna mzigo usio wa kawaida.

Wanakopa pesa, wanapanda "pipa" wanaenda "majuu." "Wathungu" wanatumia mitambo mikali zaidi kupima, lakini mambo ni yaleyale. Daktari anaandika: "No abnormality detected (NAD)!" Wanarudi "home" wamenyong'onyea, maana pesa imeliwa bila uponyaji!

Shetani unawapotosha tena, unawaelekeza kwa waganga wa kienyeji. Wanaenda, wanapewa masharti ya kuwafadhaisha zaidi. Eti wapeleke kuku na pesa. Wanapeleka, kisha wanapewa dawa za uongo na kuambiwa hizo dawa wakazimeze usiku makaburini. Maumivu yanazidi wanarudi tena kwa waganga, wanaambiwa eti wapeleke mbuzi na mavi ya tembo, watapata dawa kali zaidi! Waganga wanakula mbuzi bila jasho, wakati wagonjwa badala ya kupona, wanajikuta wakifungwa zaidi na minyororo yako shetani!

Magari ya matangazo yanapita mitaani yakitangaza: "Jamani Yesu anaponya buree. Waleteni wagonjwa mkutanoni, watapona kwa Jina la Yesu - bila chumvi wala mafuta feki ya upako..." Wagonjwa wanajipanga kuhudhuria mkutano. Unawadanganya tena. Unawaambia eti miujiza haipo, eti haiwezekani mtu kupona kwa maombi tu. Unawashawishi waone maombi ni ujinga, waone uponyaji wa Jina la Yesu kama hadithi tu!

Kwa Jina la Yesu Kristo, nakukemea! Acha kupotosha watu wa Mungu! Magonjwa yanayosababishwa na mapepo, hayawezi kuondoka kwa tiba za kibinadamu, hayawezi kupona kwa antibiotics, hayawezi kuponywa na miti shamba wala dawa za kisasa! Ni kwa Jina la Yesu pekee!

Shetani leo nimekufichua. Wewe ni mwongo! Ndiyo maana ulifukuzwa mbinguni; na leo nakufukuza! Toka hapa!

Kwa mamlaka niliyopewa na Yesu, nakuamuru shetani:
👉 Toka kwa Jina la Yesu. Toka na mapepo yako.
👉 Toka katika miili ya watu uliowaonea!
👉 Toka na roho zako chafu! Toka na magonjwa yako yote. Shindwa na ulegee.
Watu wote wanaoteswa na mapepo wawe huru sasa hivi, kwa Jina la Yesu Kristo. Amen!

======================
Almighty God, in accordance with Your divine proclamation in John 8:32, I give thanks, for this day, the truth has been unveiled to Your people, and by it, they have been set free. In the glorious Name of Jesus, Amen.
Muda mwingine shetani anaonewa, bora uwaseme wanasiasa
 
⚠️⚠️⚠️️WARNING/HATARI !!
Kama wewe hujaokoka
usithubutu kukemea pepo. Watakurarua kama walivyowafanyia watu hawa waliofikiri ni kujitamkia tu Jina la Yesu
Matendo 19:13-16
Baadhi ya Wayahudi wenye kutangatanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwapo wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile wakiwa uchi na kujeruhiwa.
Umeolewa? Kuna jambo nataka nikupe msaada
 
Shida ya Wakristo ni kumpachika sifa ambazo Yesu hana na hata mwenyewe hazijui Kwa muktadha huo wakristo wote ni waongo ni kwa mujibu wa mtoa mada wa Shetani ni muongo basi na Wakristo ni Mashetani.
Na ushahidi upo ndani ya Bible.
 
Mdo 10:38
"...Yesu wa Nazareti...akazunguka huko na huko akitenda mema, na kuwaponya wote waliokuwa wameonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.
Ibilisi ndiyo Shetani??
 
Back
Top Bottom