Shetani nakukemea: Acha kupotosha watu kwa habari za uongo

Huna uwezo wa kumkemea shetani, ni vile unajifaragua hapo shetani ni malaika wakati wewe ni binadamu mko levo mbili tofauti
Wewe endelea tu kuamini uongo wa shetani, hasara ni yako mwenyewe. Utaliwa pesa bure!

Ukiokoka, Yesu anakupa uwezo au mamlaka ya kukanyaga nyoka(shetani) na nge(mapepo)
Luka 10:19

Nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na kushinda nguvu zote za yule adui[wachawi]; wala hakuna kitu cho chote kitakachoweza kuwadhuru.

Yakobo 4:7-10
Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

Mathayo 10:8
Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
 
Ukiachana na kuleta vifungu vya bible.Jamaa alikuuliza swali zuri tu.

Shetani sio nyoka kwanza kuweka mambo sawa.Shetani ni malaika aliyefanya uasi kwa Mungu.Shetani nimeona walokole wakimchukulia kwa wepesi sana(unaweza ukawa miongoni mwao au usiwe) lakini ni kwambie ukweli nao jua mimi binafsi ni kwamba hizi spiritual figures ni hatari kupita hizo kelele walokole hufanya.

Mbaya zaidi unakuta humo kwenye makanisa wanakopiga kelele zimejazana za kutosha sema uwezo wa kuona ndio hivyo sio kila mtu anaweza au atawezeshwa(nimeshuhudia haya wala sio story)

Mwisho kabisa shetani sio mwepesi hivyo,kama anaweza kupewa uwiano sawa na Mungu(hii tafsiri sio ya kidini na kutumia logic za kawaida tu) basi ujue sio mwepesi.Kwenye dini mnasema mbiguni ni makazi ya Mungu and the opposite of heaven is likely to be hell where Satan is a king.Sasa hamuoni adui ni mkubwa kiasi kwamba mnahitaji utulivu mnavyo-wage battle nae?
 
KING MIDAS huna wazazi? Kama huna wazazi, hukuenda shule ukafundishwa adabu? Kama hukuenda shule, kanisani kwako hawakufundishi umuhimu wa kuwaheshimu Wakuu?

NAKUONYA kwa Neno la Bwana, acha mara moja, tabia hiyo ya kukosa heshima kwa Wakuu. La sivyo utajipatia hukumu(Warumi 13:7).
Mpeni kila mtu haki yake; mtu wa ushuru, ushuru; wa kodi, kodi; na astahiliye heshima, heshima

1 Petro 2:17

Waheshimuni watu wote...Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.
 
Shetani sio nyoka kwanza kuweka mambo sawa.
Shetani anawadanganya msisome Biblia, matokeo yake mnakosa ufahamu.
Ufunuo 12:9
"Yule nyoka mkuu, yule joka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, adanganyaye ulimwengu wote, akatupwa chini; yeye na malaika zake wakatupwa pamoja naye."

2 Wakorintho 11:3-4
"... kama vile Hawa alivyodanganywa kwa ujanja wa yule nyoka, mawazo yenu yasije yakapotoshwa, mkauacha unyofu na usafi wa upendo wenu kwa Yesu."
 
Wewe shetani. Kwanini unawaonea watu? Watu wanateseka, hawana kazi, hawana pesa, maisha yamekuwa magumu. Wakitazama TV, wanakutana na habari za vita, mauaji, majanga na dhiki kila mahali. Badala ya kuwaachia hata pumzi kidogo, unawaongezea maumivu. Unawatupia mapepo yanayowatesa kwa magonjwa yasiyojulikana - magonjwa yanayowafanya walie usiku na mchana, magonjwa yanayowachosha na kuwafanya waanze kumtukana Mungu. Halafu unachekelea unapowaona wanalia kama watoto. 👉We-wee!

Mbaya zaidi unawadanganya! Unawaambia magonjwa hayo yatapona yenyewe kwa antibodies, wakati unajua kabisa kwamba antibodies haziwezi kupambana na mapepo! Unawaambia watulie, wasubiri miili yao ijiponye yenyewe. Badala ya kupona, hali zao zinazidi kuwa mbaya. Maumivu yanaongezeka, afya inadorora, na matumaini yanazimika.

Wanakimbilia hospitali, madaktari wanaanza kazi ya kupima. Wanatumia: Thermometer, Stethoscope, Sphygmomanometer, Pulse Oximeter, Hematology Analyzer, Blood Glucose Meter, ELISA Machine, PCR Machine, Urinalysis Analyzer, X-ray Machine, CT Scan, MRI, Ultrasound Machine, ECG, Echocardiogram, Spirometer, Peak Flow Meter, Otoscope, Laryngoscope, Nasal Endoscope, Ophthalmoscope, Slit Lamp, Tonometer... madaktari wanashangaa, duuh—vipimo havionyeshi ugonjwa wowote, lakini maumivu yapo, tena mazito! Wagonjwa wanaambiwa labda ni stress, labda ni mawazo, nendeni mkapumzike! Wagonjwa wanarudi nyumbani kwa huzuni, maana wanajua ndani yao kuna mzigo usio wa kawaida.

Wanakopa pesa, wanapanda "pipa" wanaenda "majuu." "Wathungu" wanatumia mitambo mikali zaidi kupima, lakini mambo ni yaleyale. Daktari anaandika: "No abnormality detected (NAD)!" Wanarudi "home" wamenyong'onyea, maana pesa imeliwa bila uponyaji!

Shetani unawapotosha tena, unawaelekeza kwa waganga wa kienyeji. Wanaenda, wanapewa masharti ya kuwafadhaisha zaidi. Eti wapeleke kuku na pesa. Wanapeleka, kisha wanapewa dawa za uongo na kuambiwa hizo dawa wakazimeze usiku makaburini. Maumivu yanazidi wanarudi tena kwa waganga, wanaambiwa eti wapeleke mbuzi na mavi ya tembo, watapata dawa kali zaidi! Waganga wanakula mbuzi bila jasho, wakati wagonjwa badala ya kupona, wanajikuta wakifungwa zaidi na minyororo yako shetani!

Magari ya matangazo yanapita mitaani yakitangaza: "Jamani Yesu anaponya buree. Waleteni wagonjwa mkutanoni, watapona kwa Jina la Yesu - bila chumvi wala mafuta feki ya upako..." Wagonjwa wanajipanga kuhudhuria mkutano. Unawadanganya tena. Unawaambia eti miujiza haipo, eti haiwezekani mtu kupona kwa maombi tu. Unawashawishi waone maombi ni ujinga, waone uponyaji wa Jina la Yesu kama hadithi tu!

Kwa Jina la Yesu Kristo, nakukemea! Acha kupotosha watu wa Mungu! Magonjwa yanayosababishwa na mapepo, hayawezi kuondoka kwa tiba za kibinadamu, hayawezi kupona kwa antibiotics, hayawezi kuponywa na miti shamba wala dawa za kisasa! Ni kwa Jina la Yesu pekee!

Shetani leo nimekufichua. Wewe ni mwongo! Ndiyo maana ulifukuzwa mbinguni; na leo nakufukuza! Toka hapa!

Kwa mamlaka niliyopewa na Yesu, nakuamuru shetani:
👉 Toka kwa Jina la Yesu. Toka na mapepo yako.
👉 Toka katika miili ya watu uliowaonea!
👉 Toka na roho zako chafu! Toka na magonjwa yako yote. Shindwa na ulegee.
Watu wote wanaoteswa na mapepo wawe huru sasa hivi, kwa Jina la Yesu Kristo. Amen!

======================
Almighty God, in accordance with Your divine proclamation in John 8:32, I give thanks, for this day, the truth has been unveiled to Your people, and by it, they have been set free. In the glorious Name of Jesus, Amen.
Asante Sana Mama Mchungaji. Mungu akufunike kwa mbawa zake kama kuku anavyowafunika vifaranga wake.
 
Wewe endelea tu kuamini uongo wa shetani, hasara ni yako mwenyewe. Utaliwa pesa bure!

Ukiokoka, Yesu anakupa uwezo au mamlaka ya kukanyaga nyoka(shetani) na nge(mapepo)
Luka 10:19

Nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na kushinda nguvu zote za yule adui[wachawi]; wala hakuna kitu cho chote kitakachoweza kuwadhuru.

Yakobo 4:7-10
Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

Mathayo 10:8
Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
Ukweli usiopenda kusikia ni kuwa Yesu ni binadamu ila Shetani ni Malaika. Zaidi ya kunyanyua mdomo na kuongea huna uwezo wowote wa kumuonya shetani, kuponya wagonjwa wala kutoa pepo.
 
Wewe binadamu una uwezo gani wa kumkemea shetani ambae ni roho? Akikugeuzia kibai ni dakika sifuri anaondoka na roho yako. Labda umuulize Mungu wako unaemuabudu ni kwa nini anaruhusu shetani kufanya yote hayo.
 
Mnaonaje tuungane kwa pamoja tumuombe Mungu amfutilie mbali shetani aache kutusumbua na asituzoee zoee😂😂
Huyo katengewa adhabu na siku yake yaja. We pambania nafsi yako isije adhibiwa pamoja nae
 
Shetani anawadanganya msisome Biblia, matokeo yake mnakosa ufahamu.
Ufunuo 12:9
"Yule nyoka mkuu, yule joka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, adanganyaye ulimwengu wote, akatupwa chini; yeye na malaika zake wakatupwa pamoja naye."

2 Wakorintho 11:3-4
"... kama vile Hawa alivyodanganywa kwa ujanja wa yule nyoka, mawazo yenu yasije yakapotoshwa, mkauacha unyofu na usafi wa upendo wenu kwa Yesu."
Umejuaje hatusomi biblia?
 
Ndio maana huwa sipendi kutumia bible verses kufanya clarification ya jambo lolote lile maana ni rahisi kupatia au kukosea pia.

Yule malaika aliyetumwa kuchukua mwili wa Moses alipambana na shetani kwa muda kadhaa kabla ya kuchukua ule mwili.Je,ile ilikuwa nyoka?au yule alikuwa siyo shetani mwenyewe?

Job(Ayubu) anatajwa kujaribiwa na shetani baada ya Mungu kumruhusu shetani kufanya hivyo.Je,Ayubu alijaribiwa na nyoka?

Jesus Christ(Yesu) katika kipindi chake huko nyikani shetani alipata mtokea na kutaka kumtia majaribuni.Je,yule alikuwa nyoka?

Katika book of revelation,tunaelezwa kwamba shetani na malaika wake watakuwa chained for a mentioned period of time.Je,nyoka ndiye atakuwa chained? Na kama shetani ni nyoka,je malaika wake wanaumbo kama hilo?

Mwisho kabisa ni lini nyoka alitajwa kuwa malaika wa Mungu?maana shetani/devil/lucifer anatajwa kama malaika aliyekuwa akimtumikia Mungu na badae kuasi(The book of Enoch does tell everything.However,it is not included in Catholic bibles)
 
Wewe binadamu una uwezo gani wa kumkemea shetani ambae ni roho? Akikugeuzia kibai ni dakika sifuri
Yesu amenipa uwezo au mamlaka ya kumkemea shetani, mapepo na wachawi. Nataja tu Jina la Yesu, yanakimbia.
Lk 9:1
Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote

Mamlaka.jpg

Kama mtu hajui nini maana ya kupewa mamlaka, angalau picha hii inaweza kumsaidia kujua nini maana ya kupewa mamlaka. Askari wa usalama barabarani akinyoosha mkono tu barabarani magari hata kama ni malori makubwa yanasimama. Hata kama askari huyo ni mwembamba au mfupi, magari yanasimama. Ndivyo mtu alivyookoka anavyokuwa. Akitamka tu Jina la Yesu, shetani na mapepo na majini na makata na vibwengo vyote vinasalim amri. Jina la Yesu lina nguvu na linapita majina yote( Flp 2:9-11)
 
⚠️⚠️⚠️️WARNING/HATARI !!
Kama wewe hujaokoka
usithubutu kukemea pepo. Watakurarua kama walivyowafanyia watu hawa waliofikiri ni kujitamkia tu Jina la Yesu
Matendo 19:13-16
Baadhi ya Wayahudi wenye kutangatanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwapo wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile wakiwa uchi na kujeruhiwa.
 
Wewe shetani. Kwanini unawaonea watu? Watu wanateseka, hawana kazi, hawana pesa, maisha yamekuwa magumu. Wakitazama TV, wanakutana na habari za vita, mauaji, majanga na dhiki kila mahali. Badala ya kuwaachia hata pumzi kidogo, unawaongezea maumivu. Unawatupia mapepo yanayowatesa kwa magonjwa yasiyojulikana - magonjwa yanayowafanya walie usiku na mchana, magonjwa yanayowachosha na kuwafanya waanze kumtukana Mungu. Halafu unachekelea unapowaona wanalia kama watoto. 👉We-wee!

Mbaya zaidi unawadanganya! Unawaambia magonjwa hayo yatapona yenyewe kwa antibodies, wakati unajua kabisa kwamba antibodies haziwezi kupambana na mapepo! Unawaambia watulie, wasubiri miili yao ijiponye yenyewe. Badala ya kupona, hali zao zinazidi kuwa mbaya. Maumivu yanaongezeka, afya inadorora, na matumaini yanazimika.

Wanakimbilia hospitali, madaktari wanaanza kazi ya kupima. Wanatumia: Thermometer, Stethoscope, Sphygmomanometer, Pulse Oximeter, Hematology Analyzer, Blood Glucose Meter, ELISA Machine, PCR Machine, Urinalysis Analyzer, X-ray Machine, CT Scan, MRI, Ultrasound Machine, ECG, Echocardiogram, Spirometer, Peak Flow Meter, Otoscope, Laryngoscope, Nasal Endoscope, Ophthalmoscope, Slit Lamp, Tonometer... madaktari wanashangaa, duuh—vipimo havionyeshi ugonjwa wowote, lakini maumivu yapo, tena mazito! Wagonjwa wanaambiwa labda ni stress, labda ni mawazo, nendeni mkapumzike! Wagonjwa wanarudi nyumbani kwa huzuni, maana wanajua ndani yao kuna mzigo usio wa kawaida.

Wanakopa pesa, wanapanda "pipa" wanaenda "majuu." "Wathungu" wanatumia mitambo mikali zaidi kupima, lakini mambo ni yaleyale. Daktari anaandika: "No abnormality detected (NAD)!" Wanarudi "home" wamenyong'onyea, maana pesa imeliwa bila uponyaji!

Shetani unawapotosha tena, unawaelekeza kwa waganga wa kienyeji. Wanaenda, wanapewa masharti ya kuwafadhaisha zaidi. Eti wapeleke kuku na pesa. Wanapeleka, kisha wanapewa dawa za uongo na kuambiwa hizo dawa wakazimeze usiku makaburini. Maumivu yanazidi wanarudi tena kwa waganga, wanaambiwa eti wapeleke mbuzi na mavi ya tembo, watapata dawa kali zaidi! Waganga wanakula mbuzi bila jasho, wakati wagonjwa badala ya kupona, wanajikuta wakifungwa zaidi na minyororo yako shetani!

Magari ya matangazo yanapita mitaani yakitangaza: "Jamani Yesu anaponya buree. Waleteni wagonjwa mkutanoni, watapona kwa Jina la Yesu - bila chumvi wala mafuta feki ya upako..." Wagonjwa wanajipanga kuhudhuria mkutano. Unawadanganya tena. Unawaambia eti miujiza haipo, eti haiwezekani mtu kupona kwa maombi tu. Unawashawishi waone maombi ni ujinga, waone uponyaji wa Jina la Yesu kama hadithi tu!

Kwa Jina la Yesu Kristo, nakukemea! Acha kupotosha watu wa Mungu! Magonjwa yanayosababishwa na mapepo, hayawezi kuondoka kwa tiba za kibinadamu, hayawezi kupona kwa antibiotics, hayawezi kuponywa na miti shamba wala dawa za kisasa! Ni kwa Jina la Yesu pekee!

Shetani leo nimekufichua. Wewe ni mwongo! Ndiyo maana ulifukuzwa mbinguni; na leo nakufukuza! Toka hapa!

Kwa mamlaka niliyopewa na Yesu, nakuamuru shetani:
👉 Toka kwa Jina la Yesu. Toka na mapepo yako.
👉 Toka katika miili ya watu uliowaonea!
👉 Toka na roho zako chafu! Toka na magonjwa yako yote. Shindwa na ulegee.
Watu wote wanaoteswa na mapepo wawe huru sasa hivi, kwa Jina la Yesu Kristo. Amen!

======================
Almighty God, in accordance with Your divine proclamation in John 8:32, I give thanks, for this day, the truth has been unveiled to Your people, and by it, they have been set free. In the glorious Name of Jesus, Amen.
Waafrica tuna shida...Mungu awezi kua upande wa watu wajinga na wapumbavu
 
Back
Top Bottom