Shibuda: Magufuli aliniahidi kunipa mil 5 nikalipe ada ya watoto lkn nilipompinga akanigeuka

Si unatuona tumerudi JF, ulituona wakati wa "bwana yule"? Tuliingia "mitini" wote.

Hata wafanya biashara wenye mitaji mikubwa waliihama nchi, lakini sasa wamerudi na AlhamduliLlah pesa zinazunguka tena mitaani. Huyajuwi hayo?
Wafanyabiashara Wenye biashara chafu ndiyo walikimbia,Sasa wanarudi tena na biashara zao chafu,but time will tell!!
 
Lakini wenye chama, wanasema alikua anakijenga chama chao kwa kuufutilia mbali upinzani. Maana bwana yule alihakikisha vyama vya upinzani havipandi majukwaani na vilikanyagwa hasa. Angalia uchaguzi wa 2020 ulivyoiacha nchi imepasuka (bunge la chama kimoja na kulazimika kuwatengeneza Covid-19), ambayo sasa mama anajitahidi kuiunganisha.

Ingawa kazi bado anayo, kwa sababu wateule wa mwendazake ambao baadhi bado anao, kuna maeneo wanamshauri vibaya au kutenda vibaya na kujikuta mama analazimika kurekebisha kwa gharama kubwa za kisiasa. Mfano kesi ya ugaidi ya Mbowe na walinzi wake watatu.
 
Nilivyosoma mimi ni kuwa Shibuda hajaomba, alipewa ofa.


Kasome tena uzi, usisome bichwa la habari tu ukaanza kuhukumu.
Ebu jiongeze akili kidogo,za kuambiwa changanya na zako,Magu alijuwaje Kama Shibuda ana shida ya ada za Watoto kama si Shibuda mwenyewe kueleza matatizo yake!? Shibuda kapindisha maelezo ili yeye aonekane mzuri na kumchafua Magu!!
 
Umeeleza ukweli kabisa. Tuweke pembeni mambo ya itikadi, tuungane na tujenge nchi yetu. Nchi imepita kipindi kigumu sana kwa miaka 5+
 
Basi mtindo wake wa kuwasilisha mada upo katika style ya masihara.
Shibuda anajua sana kiswahili. Anatumia misemo na lugha zenye misamiati migumu kufikisha ujumbe. Wengi wanaweza wasimuelewe. Ni Msukuma aliyekielewa kiswahili vizuri sana na hata matamshi yake, huwezi kuamini kwamba ni Msukuma.

Cc FaizaFoxy
 
Viongozi wa upinzani wakipata nafasi ya kuzungumza na Rais huwa wanakuwa na hoja nyepesi na maswala binafsi tu.

Hata Lisu aliomba mambo binafsi mengi tu.
Na yote hayo binafsi yanatokana na risasi 38 mlizommiminia kama mnataka kuua tembo.
 
Pumbavu we, unatamka mwenzako apotee?
 
Point mama. Umenena, wote humu ni kunguru tu. Ujasiri wetu unakomea pale majina yetu feki yanapoishia nyuma ya simu janja zetu.
 
Ayaseme hayo Magufuli akiwa madarakani, kwani hajipendi?.Mwandosya aliwahi kumkosoa , akamvua u Vice Chancellor MUST na Chuo cha Mwalimu Nyerere.
 
Kwani kuna tabu gani mkinyoosha kuwa alikua na roho mbaya mpaka mjifiche kwenye kivuli cha utani huku wenzenu wanaumizwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…