Shibuda: Magufuli aliniahidi kunipa mil 5 nikalipe ada ya watoto lkn nilipompinga akanigeuka

Shibuda: Magufuli aliniahidi kunipa mil 5 nikalipe ada ya watoto lkn nilipompinga akanigeuka

Ukipenda yakubali ukipenda yakatae. Tatizo nini?
Kinachotuponza watanzania ni unafiki na kuwa waoga kupitiliza. Kwa ninayoyaona sasa, hata rais Samia hakuwa anakubaliana na mambo mengi sana ya Magufuli na alikuwa anaburuzwa tu. Kuwa sahihi zaidi, alikuwa ametengwa na hakuwa anashirikishwa kwenye mambo mengi ya maamuzi. Lakini ajabu na yeye alikuwa ameufyata na akabaki kuabudu na kutukuza. Anyways, siwezi kumlaumu sana kwani watanzania hawabebeki na ukijaribu kuwatetea, likikupata la kukupata wanajifanya kama hawaoni! Hii nchi bila wananchi kuamka na kuacha ''hewala bwana'' bado uongozi utaendelea kufanya makosa makubwa bila hofu. Rais Samia naye anajaribu kufuta yale mabaya ya Magufuli lakini naye anatengeneza mabaya yake mengi tu! Ni check and balance hakuna!
 
Akizungumza kwenye kongamano la kuenzi falsafa ya hayati Magufuli ya tanzania ya viwanda, ndugu Shibuda amesema siku moja alipata nafasi ya kumtembelea rais Magufuli ikulu.

Anasema siku hiyo Magufuli alimkaribisha ikulu na kumuuliza vipi watoto hawajambo? Akajibu hawajambo akamwambia nataka kuchangia ada yao shilingi mil5

Shibuda akajibu asante lakini sijaridhishwa na namna unavyoendesha demokrasia katika utawala wako ndipo rais akasema sasa hata hiyo hela sikupi.

Kwa nini Shibuda hakuyasema haya Magufuli akiwa hai?
Wote tunajuwa kuwa kumpinga bwana yule, tena hadharani, ilikuwa ni kujitafutia matatizo ya bure
 
Ktk wanafiki na ma-ndumi-lakuwili Tz huyu shibuda yupo, sio mtu wa kuaminika hadi ktk umri alionao!
Ni mtu wa kupuuza daima.
 
Shibuda ana masihara mengi sana huyo Mzee.
 
Kinachotuponza watanzania ni unafiki na kuwa waoga kupitiliza. Kwa ninayoyaona sasa, hata rais Samia hakuwa anakubaliana na mambo mengi sana ya Magufuli na alikuwa anaburuzwa tu. Kuwa sahihi zaidi, alikuwa ametengwa na hakuwa anashirikishwa kwenye mambo mengi ya maamuzi. Lakini ajabu na yeye alikuwa ameufyata na akabaki kuabudu na kutukuza. Anyways, siwezi kumlaumu sana kwani watanzania hawabebeki na ukijaribu kuwatetea, likikupata la kukupata wanajifanya kama hawaoni! Hii nchi bila wananchi kuamka na kuacha ''hewala bwana'' bado uongozi utaendelea kufanya makosa makubwa bila hofu. Rais Samia naye anajaribu kufuta yale mabaya ya Magufuli lakini naye anatengeneza mabaya yake mengi tu! Ni check and balance hakuna!
Hata wewe muoga. Nani asiyeogopa Tanzania? Tanzania tulianza kutishwa ilipoanzishwa "presidential detention act" Uliza wajuzi wakujulishe ni nani aliianzisha na nani akaifuta? Na wajanja wengine walipoona hiyo haipo wakajitungia sheria zilizopendekezwa na USA za kukandamiza watu, mfano sheria ya "ugaidi" iliyomfunga Mbowe. Au sheria za utakatishaji fedha na sheria ya uhujumu uchumi. Umeshawahi kujiuliza kwanini hizo hazina dhamana? Mimi nasema sheria hizo ni ukandamizaji, anakutuhumu kwa sheria hizo kaamua kukumaliza kwa mateso, kidogo kidogo, hatafuti haki wala hataki kujuwa haki iko wapi. Ni mateso tu ya kuhukumiwa bila ya hatia.

Ni wachache sana wasioogopa. Wasioogpa ni wale wanaokuja humu JF kwa majina yao na kutoa mawazo yao kinaga ubaga. Wengine tunaokuja na id za kujipachika ni waoga ytu.
 
Kama ni kweli kayasema yaliyoandikwa humu, hayo si masihara. Labda useme Shibuda anasema ukweli lakini mtindo wake wa kuongea unauona kama masihara.
kuna thread huko mtu anakuuliza
 
hata kama mtu anamapungufu hapa umeenda mbali sana, hata kama unachuki kubwa si vyema kutumia lugha kama hii.
Bullshit, acha kujifanya una mapenzi makubwa kiasi cha kuwa mnafiki. Kipi cha ajabu hapo nilichoandika kudhihirisha chuki?? Umeona mpaka emojis za kucheka kuashiria it was all written in light heartedness. So take a chill pill and relax
 
Dah JPM huko aliko kama anayasikia haya,,,, atafedheheka sana...

Unafiki wa wanasiasa umeonekana wazi wazi baada ya JPM kufariki.

Nchi ya hovyo sana.
 
Back
Top Bottom