Shilole athibitisha kupigwa na Uchebe, asema kuanzia leo yeye siyo mke wa Uchebe

Shilole athibitisha kupigwa na Uchebe, asema kuanzia leo yeye siyo mke wa Uchebe

Nimeona shilole ameandika Gazeti refu sana kuhusu uchebe lakini amini Shilole ndo anazingua na hii yote sababu ana Pesa so anaishi like Uchebe hawezi mwambia kitu. Ukiwa na hela zako bhasi usiolewe wewe tafuta viben ten vya kukupa raha siku moja moja bhasii ila sio Utake MUME.

Ukishaolewa hizo hela zako weka pembeni vaa uhusika wa Mke..Fanya majukumu ya Mke pia Kuwa Mtii kwa mume wako na Upunguze Kidomodomoo lasivyoo utakuwa unapigwaa mpaka ukome sababu mwanaume kuwa juu ya mke ni Nature ukitaka wewe ndo uwe juu bhasi Utaumiaa tuuu na mimi nasemaa mpigwee tuu mpaka mnyooke.View attachment 1500945View attachment 1500946
Vi Ben Ten havipeleki soup hospitali ukiwa na malaria.
 
Officialshilole Naandika haya, nikiwa na akili timamu na utulivu, La kwanza kabisa nataka KUOMBA RADHI JAMII YANGU. Naomba radhi kwa sababu niliwaaminisha ndoa yangu haina tatizo, huku ukweli ukiwa hauko hivyo, nimekuwa mtu wa kuambulia vipigo na MENGINE yasiyozungumzika, Naomba radhi kwa sababu niliposikia wanawake wenzangu wakipigwa niliwaambia PAZENI SAUTI, niliposikia mwanamke kule Kigamboni ameuwawa na kuchomwa moto niliomboleza na jamii na kusema Bora angesema".. huku mimi nikijikausha na kujitoa kwenye kundi lao wakati ukweli wangu MIMI NI MWENZAO, Naomba radhi.

Mimi ni kioo cha jamii, tena sura kubwa ya wanawake. Leo numeona nivunje ukimya kwa kuweka wazi kwamba MUME WANGU ASHRAFU SADIKI, maarufu kama UCHEBE AMEKUWA ANANIPIGA SAAANA, na tena hata baada ya kunipiga hajali kupiga simu wala kujua naendeleaje, nauguzwa na watu baki hospitali, na bado manyanyaso mengine yanayoikosesha hii ninayoiita Ndoa uhai na furaha

na zaidi nina WATOTO, watoto wanaoniangalia kama Baba na Mama, leo nikubali kufa na kuacha wanangu barabarani, SITAWEZA

'Uchebe' ni mwanaume niliyempenda, nilimvumilia kwa madhaifu yote, nikampa kila kitu, (Utu wangu, Mali Zangu na hata palipotakiwa kumuendeleza asimame mwenyewe nilifanya kwakuwa nilijua tuko pamoja), lakini HILO HALIKUWAHI KUZUIA VIPIGO, DHARAU NA USALITI.

Siku 2 zilizopita baada ya kutoka SABASABA KUTAFUTIA WATOTO WANGU NA KUMTAFUTIA YEYE NILIPIGWA SANA. SABABU ZA KUPIGWA NI MIGOGORO MIDOGO YA KAWAIDA AMBAYO IPO KWENYE KILA NDOA, sio kwamba amenifumania au mambo yanayoshindwa kuzungumzika, hapana, Tena Namuheshimu sana, lakini solution aliyoiona ni kunipiga kinyama bila huruma, tena kwa kunishtua na ngumi nikiwa usingizini, Kama mnavyoona picha hapo ni matukio ya siku tofauti tofauti.

Najua nitalaumiwa kwa kuweka hili mtandaoni, ILA SINA NAMNA, MAISHA YANGU NI MAISHA YA WATU KWA KIASI KIKUBWA, JAMII INANITAZAMA KAMA MFANO.. Nimefika mwisho, na kuanzia sasa naomba nisitambulike kama Mke wa Uchebe, ila Mama alieamua kuweka maslahi ya watoto wake mbele na kuamua kuwa mwenyewe kwa usalama na furaha yake

Wakati nahangaikia mambo yangu ya ndoa, post hii itumike kuwakumbusha wanawake TUVUNJE UKIMYA, TUPINGE UKATILI, TUTAKUJA KUULIWA SABABU

Pia soma > Shilole amchapa makofi mpenzi wake Uchebe mbele za watu

Duuuh pole sana
Huu ni upuuzi unampiga mke kama unapiga mwizi
 
Mtia nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM Zena Mohamed aka Shilole ametangaza kumuacha mme wake wa ndoa Mr Uchebe.

Shilole amedai ameamua kumuacha Uchebe kutokana na vipigo alivyokuwa akipokea mara kwa mara kutoka kwa mumewe.
Pamoja na hayo Shilole amesema harakati zake za kulinyakua jimbo la Igunga huko Tabora ziko pale pale.

Source: Ayo TV

Maendeleo hayana vyama!
Huko Bungeni amri ya sita itakoma. Kuna Steve Nyerere, Harmonise, Babu Tale list ni ndefu.
 
Nna uhakika huu sio mwandiko wa Shilole
 
  • Thanks
Reactions: Pep
hahahah Naona huyo demu amepata size yake,yeye si alikuaga anakapa kichapo heavy ka nuhu mziwanda mpk kanakimbilia barabarani,Ustaadhi Uchedi style yake ya kushtua kwa ngumi usingizini sijui alifundishiwa dojo gani.
Noma sana!
 
Wanawake hawapo hvyo mkuu kazi ya mwanamke sio kufanya fadhili akikupenda inatosha. Mwanamke leo hii huna ela siku moja tuu akakununulia chakula cha elfu 2 kwa ela yake mwenyew siku mkigombana baada ya miezi 2 atakutangazia kwa watu alikuwa anakulisha miezi 2 yote kwahyo huna fadhila na utaonekana mbya. Kwa mfano huu utaelewa hawa viumbe ni wa aina gani
Kwahiyo dawa yake ni nini mkuu, kuwapiga???

Tuangalie na wanawake wa kuoa, shida nyingine ni za kujitakia tu.
Unamuoa shilole unategemea ule peke ako?
 
daah jamaa kapiga. achukuliwe hatua kali. siku moja moja shemeji wenu huwa "anaomba" nimpige, basi namgusa gusa tu
 
Back
Top Bottom