Shindano la big brother lina maudhui gani?

Shindano la big brother lina maudhui gani?

Mkuu, kuweka remote chumbani haitoshi, watoto wanahamisha direct kwenye decor.
Ni kweli, ila huwa nabeba kisimbuzi na remote yake.

Nyumbani kwangu nina Visimbuzi viwili, pamoja na Azam, kwahiyo huwa naondoa cha Dstv nawaachia Azam TV
 
Wanasema ukiona Kipindi hukielewi, huenda haukuwa Mlengwa.

Kutokana na Umri, kwasasa nimekuwa sifatilii Big Brother tena, ingawa wakati nilipokuwa kwenye lika la adolescent nilikuwa muhanga wa kukitazama miaka ile ya Akina Mwisho Mwampamba, baadaye akina Richard n.k

==============
Kuna baadhi ya Filamu/Vipindi vya TV kutokana na maadili yetu havistahili kutazamwa.

Hiyo Program ya Big Brother na nyingine zenye mlengo huo, zimeanzishwa kwaajili ya ku-brainwash Vijana wetu ili waone mambo ya ngono na kukaa na vichupi chupi mbele ya Wazee wao ni jambo la kawaida.

Kama una vijana wako nyumbani, ni heri Remote ikafichwa chumbani kwa Baba.

Ni heri kuitwa Mzee Mnoko kuliko kuharibu kizazi chako kwa mikono yako.
Asante.
 
Kuna mshikaji mmoja natamani nimtag aje atoe neno hapa maana kukiwa na BB siku hiyo mkizubaa hakuna kitakachoendelea kisa anaangalia show.

Maudhui yake nadhani, mbali na kuburudisha hasa katika kizazi hiki kinachoabudu celebrities hata kama hawana kipaji cho chote, ni kuonyesha ushindani; na hasa undumilakuwili na unafiki wa binadamu maana mule hakuna kuaminiana. Hata mtu mnayenyanduana naye anaweza kukugeuka wakati wo wote na kukuleftisha.

Ni show isiyoeleweka hasa katika uwasilishaji wake wa maudhui japo inapendwa sana na vijana wa kizazi kipya wanaotafuta mashujaa wapya na role models katika maisha yao.
Nilikuwa naipenda kipindi kile inajumuisha nchi zote za Africa maana kulikuwa kuna kaushindani ka kitaifa, halafu ile season ya kwanza ya kina Mwisho mwampamba na kidogo ya kina Richard ilikuwa na uhalisia, zilizofuata watu walikuwa wanaigiza sana

Inshort big brother ilikuwa ni reality show ya ukweli na wengi wetu tulikuwa tunapenda kuangalia personalities nzuri na drama lakini pia kujifunza mila, tamaduni na tabia za waafrika.. It was
πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

Hayo ya wengi wanaosema kuna sex, wangeiona ile season one iliyofungiwa ndo wangeelewa 😁😁😁 kwanza siku hizi wanaonesha shower hour kweli maana toka season ya Idris sultan, sijawahi kuiangalia tena
 
Back
Top Bottom