Kuna kingine zaidi ya mihemko na kiki za kijingaKwani hapa Bongo Elimu ya lazima ni mpka ufike level gani!?
Hapa wamezingua mtu amehitimu form four akili yake tiari imeshakomaa kuendelea kusoma na kuto endelea kusoma ni mamuzi yake yeye mwenyew kuamua siyo kuamuliwa .
Sjui hapa ni kigezo gani kimetumika kuvuruga harusi ya huyo binti
Zimetimia kabisaMabinti kuolewa wala hakukatishi ndoto ni kukariri maisha tu.
Rais wa nchi hii alihitimu kidato cha nne 1977 na mwaka 1978 akaolewa!
Ndoto zipi hajatimiza?
Itoshe kusema ni uinevuKuna kingine zaidi ya mihemko na kiki za kijinga
[emoji16][emoji16][emoji16]ili jamaa limewaza mbali sana, huwezi waza ivi kama muda huo huna njaaDaah ukute hapo hata muda wa mpunga ulikuwa ndio unakaribia alafu umewaambia nyumbn msioike Leo naenda kula harusini.
Mm nikisikiaga sherehe yyte jambo la kwanza linalokuja kichwan ni kula tu mengine sio issue, nikichangia harusi ukaja nipa vireja na maji utarudisha mchango wangu.[emoji16][emoji16][emoji16]ili jamaa limewaza mbali sana, huwezi waza ivi kama muda huo huna njaa
Ni watu werevu pekee ndiyo wataelewa hiki ulichoandika hapa.Hawa washenzi, kwani Binti hawezi kuolewa akaendelea na shule? Hii ni kuzuia maamuzi binafsi ya watu
Walimu mnawapa kazi sana na mishahara mbuzi, sasa huyu binti aliyepelekwa shule na SMG unategemea atasoma kweli
Kama Binti ameridhika wamuache tu, vijana watengeneza familia hata kwa kilimo na ufugaji watatoka tu, vijana wa vijijini wengi wamepiga hatua unakuta ana kajumba,shamba na mifugo mingi tu, huku mjini tukishapanga self na kumiliki I phone tunaona maisha tumeyaweza, alafu kwa ajira zipi watu walazimishwe kusoma kwa kushikiwa SMG?Ni watu werevu pekee ndiyo wataelewa hiki ulichoandika hapa.
Wajinga kweli, wamefanya kosa gani. Binti ni over 18.Ikiwa ni tofauti ya siku mbili tangu kuadhimishwa siku ya mtoto wa Afrika ilikwend ana kauli mbiu ya Mpe nafasi msichana boresha sheria ya ndoa na kuchagizwa na mabango yenye jumbe mbalimbali kama USINIPE MUME NIPE ELIMU.
Huko mkoani Shinyanga hali ni tofauti kabisa kwani imejitokeza tukio la kuozeshwa binti aliyefaulu na kuchaguliwa kwenda kidato cha tano. Wazazi wameona ni bora mtoto huyo akaolewe na kukatiza ndoto zake za kuendelea na maso.
=====
Jioni ya jana timu ya wataalam mbalimbali ikiambatana na Mhe Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christine Mndeme na vyombo vya DOLA wamefika katika kijiji cha Mwawaza na kufanikiwa Kuzuia NDOA ambayo Bi Harusi ni Mwanafunzi aliyechaguliwa kuingia kidato cha tano ila wazazi wake wakaamua KUMUOZESHA Sasa Hawa Wazazi watajua kuwa Shinyanga ya Mndeme ni ya ELIMU na SIYO kuoa WANAFUNZI.
Kuna comedian Jana nilimsikiliza, Naona anawazidi akili wote waliokwenda kuharibu shughuli ya Watu, Nanukuu, alisema Kwa mwanamke Kuna choices tatu, Kusoma, kutafuta Maisha na kuolewa, na Sio lazima upitie yote!! Unaweza kuruka yote na kuamua kuolewa kujenga familia, au unaweza ukaamua kutafuta Maisha, au Zaidi Zaidi ukaamua kusoma then ukaolewa!! Sasa hao Polisi wanakereka na nini!? Kuharibu Maisha ya Watu!?Maccm bana kazi kutumia nguvu,suala la elimu ni hiari ya mtu.
Or else km binti yupo under 18.
Acha kudanganya watu sheria ya ndoa imeruhusu mtoto wa miaka kumi na nne kuolewa kwa ridhaa ya wazazi Kama wazazi wamekubaliana wewe unaingilia Nini?. Halafu kitu kingine elimu ya msingi ni form four kwa Sasa. Sasa kashavuka huko Bado mnamfuatilia.Mwanafunzi haijalishi kuwa ameenda shule au hajaenda shule,taarifa inasema kwamba anatarajiwa kuingia kidato cha nne, kwa maana hiyo bado anahesabika kama mwanafunzi,kama angekuwa hayupo katika mahesabu ya kwenda shule, basi ungekuja kutetea hoja yako hii dhaifu.
Kama utasema huyo bado hajaenda shule,basi na hawa wengine wakiwa likizo tutasema hivi hivi kwamba bado hawapo shuleni, na kama kwenda shuleni ni hiyari, kwanini asingejitoa kwenye uanafunzi, lakini haiwezekani mtu bado upo kwenye mahesabu ya wanafunzi halafu aje mtu kusema kwamba eti shule ni hiyari,hivi unajua kweli kidato cha tano na sita bado ni wanafunzi ama na wewe tukupe mtihani wa uelewa
Anakwenda kujiunga na shule gani?. Kama yet binafsi amahairisha kusoma anataka kufanya mambo mengine utamlazimisha?. Mnaingilia ndoa lakini madangaji mnayashobokea.Uliza mwaswali yenye akili,taarifa inasema anakwenda kujiunga na kidato cha tano,wewe unakuja na maswali anakwenda shule gani.
Imetumika lugha tahisi sana, huyo ni Mwanafunzi,we unakuja kuuliza shule gani.
hii inaashiria hata uwezo wako wa kufahamu kidato cha tano ni kitu gani bado ni uwezo mdogo sana.
Cheap popularity. Hakuna kitu hapo.View attachment 2661940
Timu ya Wataalamu wa msaada wa kisheria kutoka Mama Samia Legal Aid Campaign ikishirikiana na RC wa Shinyanga, Christina Mndeme na Jeshi la Polisi Shinyanga wamefanikiwa kuzuia ndoa ya Binti aliyefaulu kuingia kidato cha tano lakini Wazazi wake waliamua kumuozesha katika kijiji cha Mwawaza nje kidogo ya Manispaa ya Shinyanga.
Timu hiyo ilifika eneo la tukio na kushuhudia zoezi la uzuiaji na kukamata walengwa ambapo RC wa Shinyanga amesema ndoa hiyo ililenga kuzima ndoto za Binti huyo.
Mndeme amesema Mkoa wa Shinyanga hauko tayari kuona Watoto wa kike wanashindwa kufikia ndoto zao kwa ajili ya Wazazi wachache wenye tamaa ya mali, ambapo ameagiza Wazazi hao ambao wametoweka kufika Kituo Kikuu cha Polisi Mjini Shinyanga “Serikali ya Mkoa wa Shinyanga itasimamia Binti huyu apate haki ya msingi ya kupata elimu ili aweze kufikia ndoto zake”
Mbona video ipo.Acheni uoga watajeni wahusika wekeni na video tuone Maxence Melo hajakataza kufanya hivyo Wala uongozi wa JamiiForums haujakataza sasa mnaogopa Nini hata picha ?