Ohm24
Member
- Dec 28, 2020
- 83
- 87
Maeneo kadhaa huko Mbopo, Kinondo na sehemu fulani huko Mabwepande shirika la DDC linadaiwa kuvamia raia na kuyapora maeneo wakidai ni ya kwao. Nyumba zinavunjwa viwanja walivyonunua wananchi kwa taratibu kabisa na uwepo wa wajumbe wa maeneo husika lakini wanakuja kuwapora huu ni uvunjifu wa HAKI za binadamu na haikubaliki kunyanyasa raia wa nchi hii.
Ombi kwa serikali kuu ingilieni mtafaruku huu utasababisha uvunjifu wa amani pasipo sababu zozote. Muda wote walikuwa wapi hao DDC wakavizia wananchi wameuziwa na kujenga nyumba kisha waende kupora ardhi na kuvunja nyumba zao bila fidia?
Mada iko mezani wadau na wanasheria jitokezeni kukomesha uonevu huu. Mbunge wa Kawe yuko wapi?
Kumekua na malalamiko endelevu juu ya uendelezwaji holela wa makazi lakini mwisho wa siku lawama zote hurudi kwa serikali. Labda tujiulize-
Serikali ya mtaa inahusikaje na ardhi iliyo mjini?
Ni vitu gani vya kuzingatia kabla hujanunua au kuendeleza ardhi?
Sheria ya mipango miji ya 2007 izipa nguvu serikali za mitaa(town,district,municipal&cities)kama mamlaka za usimamiz wa ardhi kwa eneo husika(urban). je mamlaka hzo zimehusishwa kikamilifu wakati wa ununuzi na umilikishwaji na eneo lalamikiwa?
Ujenzi pasipo kibali cha ujenzi kutoka mamlaka husika. Maeneo hupangwa kwa matumizi tofauti(compatible land uses) sasa mtu anaenda weka nyumba ya makazi maeneo ya viwanda hatarishi unategemea utaachwa?
Tupate muda wa kujifunza zaidi kabla hatutoa lawama