Shirika la DDC Kuchukua Ardhi huko Mbopo, Kinondo na Mabwepande kutoka kwa Wananchi ni Uporaji

Maeneo kadhaa huko Mbopo, Kinondo na sehemu fulani huko Mabwepande shirika la DDC linadaiwa kuvamia raia na kuyapora maeneo wakidai ni ya kwao. Nyumba zinavunjwa viwanja walivyonunua wananchi kwa taratibu kabisa na uwepo wa wajumbe wa maeneo husika lakini wanakuja kuwapora huu ni uvunjifu wa HAKI za binadamu na haikubaliki kunyanyasa raia wa nchi hii.

Ombi kwa serikali kuu ingilieni mtafaruku huu utasababisha uvunjifu wa amani pasipo sababu zozote. Muda wote walikuwa wapi hao DDC wakavizia wananchi wameuziwa na kujenga nyumba kisha waende kupora ardhi na kuvunja nyumba zao bila fidia?

Mada iko mezani wadau na wanasheria jitokezeni kukomesha uonevu huu. Mbunge wa Kawe yuko wapi?

Kumekua na malalamiko endelevu juu ya uendelezwaji holela wa makazi lakini mwisho wa siku lawama zote hurudi kwa serikali. Labda tujiulize-
Serikali ya mtaa inahusikaje na ardhi iliyo mjini?
Ni vitu gani vya kuzingatia kabla hujanunua au kuendeleza ardhi?
Sheria ya mipango miji ya 2007 izipa nguvu serikali za mitaa(town,district,municipal&cities)kama mamlaka za usimamiz wa ardhi kwa eneo husika(urban). je mamlaka hzo zimehusishwa kikamilifu wakati wa ununuzi na umilikishwaji na eneo lalamikiwa?
Ujenzi pasipo kibali cha ujenzi kutoka mamlaka husika. Maeneo hupangwa kwa matumizi tofauti(compatible land uses) sasa mtu anaenda weka nyumba ya makazi maeneo ya viwanda hatarishi unategemea utaachwa?
Tupate muda wa kujifunza zaidi kabla hatutoa lawama
 
Pre occupation of land
Kuna wakili mmoja nimesoma mahali anadai iwapo mtu atavamia eneo lisilo lake na akaliendeleza kwa miaka 12 mfululizo bila mmiliki halali kujitokeza basi eneo hilo linatambulika lake kisheria.

Hii sheria ya ardhi ipo kweli au jamaa ni wale bush lawyers?
 
Hakuna WA kukomesha kisiasa, Mipango miji wafanye kazi Yao ni siasa iwekwe pembeni
 
Maeneo kadhaa huko Mbopo, Kinondo na sehemu fulani huko Mabwepande shirika la DDC linadaiwa kuvamia raia na kuyapora maeneo wakidai ni ya kwao. Nyumba zinavunjwa viwanja walivyonunua wananchi kwa taratibu kabisa na uwepo wa wajumbe wa maeneo husika lakini wanakuja kuwapora huu ni uvunjifu wa HAKI za binadamu na haikubaliki kunyanyasa raia wa nchi hii.

Ombi kwa serikali kuu ingilieni mtafaruku huu utasababisha uvunjifu wa amani pasipo sababu zozote. Muda wote walikuwa wapi hao DDC wakavizia wananchi wameuziwa na kujenga nyumba kisha waende kupora ardhi na kuvunja nyumba zao bila fidia?

Mada iko mezani wadau na wanasheria jitokezeni kukomesha uonevu huu. Mbunge wa Kawe yuko wapi?
Wananchi na serikali wanadhulumiana
 
Kuna wakili mmoja nimesoma mahali anadai iwapo mtu atavamia eneo lisilo lake na akaliendeleza kwa miaka 12 mfululizo bila mmiliki halali kujitokeza basi eneo hilo linatambulika lake kisheria.

Hii sheria ya ardhi ipo kweli au jamaa ni wale bush lawyers?
Hiyo Sheria ipo inahusu 'Adverse possession' lakini siyo automatic, inatakiwa muda huo ukipita,ufanye utaratibu wa kuomba umiliki kwenye mamlaka husika,siyo una-relax tu unasubiri vurugu ndo uje na hiyo option
 
Kwa stahili hiiii, Unadhan Wananchi wa Tanzania, utawaeleza nn kuhusu JPM Hadi wamuone mbaya??.

Mimi nadhani ni wapumbavu tu ndo wanaweza kupambana na Hayati JPM
Waliovunjiwa nyumba zao mbezi unawaweka kwenye kundi gani?binafsi pa1 na baadhi ya mazuri yake hamna serikali iliyowaumiza raia kama ya magu labda nyie wanufaika wake kwa 100% ndio mlikua amuoni hiyo kitu
 
Humu humpati wamanasheria katu. hakuna wartu wa hovyo kama wanasheria hasa mawakili. Wachoyo, roho mbaya na wanafiki. Uanasheria ni elimu ya kupingana na Haki..by Shaaban Robert1
Vipi kulikoni mwenzetu mbona umekuja na conclusion Hasi sana Kwa Mawakili wote.Hebu toa sababu hapa ya ku- justify roho Mbaya zao kiasi hicho
 
Hakuna Mtu aliekua na hati Miliki barabara ya Morogoro.

Mimi nilikua moja ya wahanga.

Usiongee usichofahamu mkuu

Acha uongo wewe watu kibao wana Hati nakutakija baadhi ya ninaowafahamu mzee hugo kisima wa safari resort anahati tokea zamani sana pia mzee tomas lyimo analogodown lake pale bucha anahati tokea miaka ya 80 .
Na pia waliobomolewa Kimara walienda mahakamani na wameshinda kesi wanatakiwa walipwe fidia
 
Siku Zote nasali njia Bora ya kuliweka Jiji katika mpangilio Hawa DDC walichelewa sana hadi Hawa wavamizi wakajimilikisha maeneo mengi Kama utulivu, Mwendokasi, Islamic na Zimbabwe, kote Huku wamejenga vibanda vya hovyo na kaharibu Mazingira!! Chonde chonde Serekali isimame mahala pake na kupima haya maeneo ili watu waweze kuwekewa barabara na huduma nyingine za kijamii, Najua maji yamewekwa katika mtazamo Watu watakapopimiwa huduma iwepo!!Mbona NSSF waliweza kuondoa wavamizi why not DDC!?
Shida na sisi wananchi watu Huwa waendi mipango miji mtu kauziwa tu eneo na dalali anaanza ujenz bila hata kutafuta uhalali wa lile eneo
 
Kumekua na malalamiko endelevu juu ya uendelezwaji holela wa makazi lakini mwisho wa siku lawama zote hurudi kwa serikali. Labda tujiulize-
Serikali ya mtaa inahusikaje na ardhi iliyo mjini?
Ni vitu gani vya kuzingatia kabla hujanunua au kuendeleza ardhi?
Sheria ya mipango miji ya 2007 izipa nguvu serikali za mitaa(town,district,municipal&cities)kama mamlaka za usimamiz wa ardhi kwa eneo husika(urban). je mamlaka hzo zimehusishwa kikamilifu wakati wa ununuzi na umilikishwaji na eneo lalamikiwa?
Ujenzi pasipo kibali cha ujenzi kutoka mamlaka husika. Maeneo hupangwa kwa matumizi tofauti(compatible land uses) sasa mtu anaenda weka nyumba ya makazi maeneo ya viwanda hatarishi unategemea utaachwa?
Tupate muda wa kujifunza zaidi kabla hatutoa lawama

Hayo maeneo ya huko mabwepande DDC walikuwa wanayamilika tokea zamani sana na hata sasa wanavyofanya kuyachukua ni kwamba kuna eneo wameliacha kwani limeshaendelezwa sana na limekuwa mji so wamerathimishiwa Kwa kuuziwa
Tatizo ni Serikali na taasisi zake wanachukua maeneo wanashindwa kuyeendeleza na kuzuia yasivamiwe.
Yaani inashangaza sana kusikia kuna wananchi wamevamia eneo la Jeshi na hadi amejenga ameishi amepata watoto na wajukuu Jeshi linakuja linasemq eneo lake.
Kuna mgogoro mwingine maeneo ya Baruti kwamba lile eneo kulikuwa na kiwanda cha Mlipuko cha wataliano kinaitwa twiga chemical s, sasa hawa jamaa walipofunga viwanda wakarudisha Hati ya kile kiwanda serikali ni.
Sasa wanachi wamevamia pale na wengine wameproces hadi Hati.
Sasa serikali imeibuka sasa hivi wanataka kujenga hospitali ya wilaya ya ubungo wanataka kichukua eneo la karibia ekari elfu2 Kwa ajili ya hospitali.
 
Vipi kulikoni mwenzetu mbona umekuja na conclusion Hasi sana Kwa Mawakili wote.Hebu toa sababu hapa ya ku- justify roho Mbaya zao kiasi hicho
Uliza kitu humu cha kisheria kama utapata jibu wakati wapo wengi tu JF! Omba case law yoyote kama utapata
 
Mleta mada anaelekea ni mmoja wa wavamizi huko. Ni hivi DDC wana hati ya miaka 99 tangu miaka ya 1970. Mmeenda huko kichwakichwa mkauziwa mkapigwa na madalali wezi . Sasa DDC wanataka eneo lao haki yao wengi humo wamekaa miaka 5 HADI 7 tu hawana haki ya adverse possesion . DDC wamewapa nafasi ya kukubaliana mlipe kidogo mnakataa. Kwanza mlitakiwa mnyongwe wezi wakubwa kama Magufuli.
Hata pale wazo kiwanda cha cement ni hivo hivo. LIPA AU ONDOKA BAAASI.
 
Sidhani kama hiyo ni sababu tosha ya kuwa- generalize kuwa Advocates wote ni wachoyo,wanafiki na Wana roho Mbaya,pengine una issue personal na advocate Fulani ndo unafanya wote kuwa wabaya.Hebu tupatie mifano michache ambayo uliomba msaada na ukanyimwa bila msaada wowote.Lakini pamoja na yote,kumbuka Sheria,kama ilivyo fani zingine kama za Tiba,Uhandisi n.k. Zina ethics zake na vigezo vya kutoa msaada wa ki-taaluma kuwa ni jambo gani na mtu gani ana qualify kupata msaada huo wa kisheria(Legal Aid). Si Mawakili wote wapo JF na si Kila wakili anasoma mada zote humu JF ,bora lingekuwepo Jukwaa la Sheria ambalo lingekuwa lina- attract many lawyers ungeweza kutoa tuhuma nzito kama hizo..Isitoshe,najua huko mtaani kuna vituo vingi vya msaada wa kisheria( legal Aid Centres) ,Je ulipokosa msaada JF umeenda na huko ukanyimwa?
 
Mleta mada anaelekea ni mmoja wa wavamizi huko. Ni hivi DDC wana hati ya miaka 99 tangu miaka ya 1970. Mmeenda huko kichwakichwa mkauziwa mkapigwa na madalali wezi . Sasa DDC wanataka eneo lao haki yao wengi humo wamekaa miaka 5 HADI 7 tu hawana haki ya adverse possesion . DDC wamewapa nafasi ya kukubaliana mlipe kidogo mnakataa. Kwanza mlitakiwa mnyongwe wezi wakubwa kama Magufuli.
Hata pale wazo kiwanda cha cement ni hivo hivo. LIPA AU ONDOKA BAAASI.
Kama sikosei hati ya DDC ni ya mwaka 1984 na sio mwaka 1970.
 
Maeneo kadhaa huko Mbopo, Kinondo na sehemu fulani huko Mabwepande shirika la DDC linadaiwa kuvamia raia na kuyapora maeneo wakidai ni ya kwao. Nyumba zinavunjwa viwanja walivyonunua wananchi kwa taratibu kabisa na uwepo wa wajumbe wa maeneo husika lakini wanakuja kuwapora huu ni uvunjifu wa HAKI za binadamu na haikubaliki kunyanyasa raia wa nchi hii.

Ombi kwa serikali kuu ingilieni mtafaruku huu utasababisha uvunjifu wa amani pasipo sababu zozote. Muda wote walikuwa wapi hao DDC wakavizia wananchi wameuziwa na kujenga nyumba kisha waende kupora ardhi na kuvunja nyumba zao bila fidia?

Mada iko mezani wadau na wanasheria jitokezeni kukomesha uonevu huu. Mbunge wa Kawe yuko wapi?
I salute the learned @ Adv. Tundu Antipas Mghwai Lissu for speaking out for the under-dogged voiceless citizens who were at gunpoint looted their land and houses demolished at Mabwepande, Mbopo, and Kinondo sub-urbs by a KDC task force.

Niliandika uzi huu wachangiaji wengi walinipuuza na hata nilipotoa wito wanasheria waingilie kuwasaidia wananchi nikabezwa lakini leo huyu mwanasheria nguli amewasemea walioumizwa tena kwa uchungu sana hizi ndizo ajenda hai ambazo wapinzani wanatakiwa sio kukumbatia CCM iliyojaa wananyang'anyi wenye kutumia dola kudhulumu wananchi ambao ndio walipa kodi lakini wanageuzwa kuwa wakimbizi.

Mh wakili msomi wananchi wa maeneo tajwa hapo ukiwasimamia katika hili hutajuta kamwe na hata huyuo mbunge aliyepo kwa sasa hata kuwa na chake tena ataanza kufungasha mapema kutoka jimbo hilo.

DDC wananyang'anya mtu kiwanja cha ukubwa wa 16 x 20 alichonunua sh mil 3,500,000/= na wengine mil 3,000,000 halafu wanamwambia huyo waliyemnyang'anya kwamba wataweka mawe ya mipaka (beacon) za namba kisha alipe hao DDC kupitia kile kinachoitwa KDC sh 2,600,000/= ukijumuisha thamani inakuwa mtu huyo analazimisha kununua kiwanja chake mwenyewe mara mbili!!!!

Huu ni wizi wa wazi kabisa

Narudia wewe wakili msomi@Tundu Antipas Lissu ndiye mtetezi wa haki katika uonevu huu uliofanywa ukifanikisha wananchi kurejeshewa mwaeneo yao nakuthibitishia hayo maridhiano yenu ya wanasiasa yatafanya nyota yako ing'are isivyo kawaida.

Morogoro : DC MSANDO AWAONDOA HOFU WANANCHI WA KIEGEA A NA B JUU YA UPIMAJI WA ENEO LA STAR CITY.

Credit to@

Wananchi wako nyuma yako tumia taaluma yako ya sheria na mahusiano na wananchi moja kwa moja kuwatetea warudishiwe ardhi zao na kulipwa fidia kwa kuvunjiwa nyumba zao kikatili na serikali.
 
Kwa stahili hiiii, Unadhan Wananchi wa Tanzania, utawaeleza nn kuhusu JPM Hadi wamuone mbaya??.

Mimi nadhani ni wapumbavu tu ndo wanaweza kupambana na Hayati JPM
Magufuli alifanya nini kwa wananchi wa Kimara, Ubungo, Kyela, Kagera zaidi ya kuwapora na kuwatishia maisha?

Kwa upande mwingine, nalaani kila anayepora ardhi - katika awamu hii au yoyote ile.

Toka baada ya Azimio La 'Uporaji' la Arusha mwaka 1967, nchi yetu imetumbukia kwenye mlolongo na tabia ovu ya uparaji - hasa serikali, taasisi zake, CCM na halmashauri nchini dhidi ya wananchi na Vijiji.
Wako pia watu binafsi wanaopora, nao nawalaani vile vile.
 
Back
Top Bottom