Mimi Kwa kweli wamenipa dhambi ya kuwacheka usiku huu🤣🤣🤣Baba angu kila nikienda home kumsalimia huwa haachi kuniambia, "mwanangu, kwenye maisha yako yote usimuweke mkeo kama sehemu ya maisha yako. Usiweke nae mipango yako mingi sanaa, fanya nae kwa kiasi tu". Anaendelea kisema, "siku hizi sheria zote ni za kumlinda mwanamke, kwa jambo lolote lile ukisimama mahakamani na mwanamke, atasikilizwa yeye kwanza, hadi uje usikilizwe wewe, umeshachakaa".
Ndugu zangu wote mnaosema hao wanaume ni ma zwazwa inawezekana hamjapitia changamoto za hawa wanawake. Hata kama hamjapitia ila kila mtu atakua amewahi kushuhudia mwanamke akimtunishia mwanaume, kama ile, "nipige, nipige sasa, nipige kama kweli wewe mwanaume" kwenye hali hii wanaume wengi huamua kuwaacha tu hawa wanawake bila kuwafanya chochote. Si kwamba hawana uwezo wa kuwapiga, la. Huwa wanaepusha shari.
Ukienda police kushitaki kuwa mkeo anakufanyia chochote kibaya hutasikilizwa, ila yy akienda hata kama akasema tu ulimtishia kumpiga, kimbembe unacho. Kuna msemo unasema "A men is guilty until is proved innocence and a woman is innocent until is proved guilty". Hao wanaume kwenye video ni wakuwaonea huruma tu na sio kuwacheka.
Niishie hapa
Ila let's be honest, hivi huyo mwanamke umeishi nae vipi hadi anapata nguvu ya kunyanyua stuli akupige, ukute mume ndo ameanza kila siku vipigo anampiga mkewe, mwisho mke anachoka ananyanyua stuli.
Halafu wanaume Wasichojua ubabe na ukali hautunzi ndoa, mke ni sikio, mpe maneno matamu uone Kama atapata nguvu ya kunyanyua stuli🤣🤣🤣 udhaifu wa wanawake upo masikioni ( inabidi nianze kufunda na wanaume sasa Lamomy ), mwanamke hana tabia, tabia anaikuta kwa mumewe, sasa nyie mnataka mpige wake zenu msirudishiwe🤣🤣
Afu huyo mstaafu🤣🤣🤣 Nani asiyejua vibweka vya wastaafu...pension wanahongea, hawashikiki, ikiisha wanataka warudi kwa wake zao🤣🤣🤣