Shirika la Wanaume wanaopitia changamoto kwenye ndoa limesajiliwa kwa sheria gani? Video yao imenifanya niogope Ndoa

Shirika la Wanaume wanaopitia changamoto kwenye ndoa limesajiliwa kwa sheria gani? Video yao imenifanya niogope Ndoa

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
Habari wadau.

Kupitia Leo tena ya clouds FM imenifanya nilijue shirika la wanaume wanaopitia changamoto kwenye ndoa. Nikakutana na video ya maelezo ya wanachama wao.

Baada ya kuitazama hiyo video, nimecheka sana na kidogo Nimewaelewa wale wanaume wa humu jamiiforums wanaosema Kataa ndoa,

Tazama mwenyewe video niliyo upload


 
Nimecheka sana....Ila wanaume wa siku hizi mnadeka sana, mmepoteza Ile masculinity......Yani kupigwa na kijistuli na hivo vijikovu ndo habari ya kutangazia dunia nzima?!!!! 🤣🤣🤣 Mwanaume unapata wapi ubavu wa kutangazia ulimwengu umepigwa na mkeo? Au umenyimwa unyumba?

Mke akikupiga na wewe mvizie mpige na helaa, muongeze na viboko vya magic stick🤣🤣🤣🤣 hili nalo tuwafundishe🤣🤣🤣

Anyway siku hizi watu wanasaka fursa kila mahali, hao kwenye video ukiwaangalia Kwa jicho la ndani ni wasakatonge tu🤣🤣🤣
 
Na hao ndio wa kutushauri Sisi tuoe ...labda tuoe mamba, kenge na mijusi inayokimbia mvu na kuingia mtoni.
 
Baba angu kila nikienda home kumsalimia huwa haachi kuniambia, "mwanangu, kwenye maisha yako yote usimuweke mkeo kama sehemu ya maisha yako. Usiweke nae mipango yako mingi sanaa, fanya nae kwa kiasi tu". Anaendelea kisema, "siku hizi sheria zote ni za kumlinda mwanamke, kwa jambo lolote lile ukisimama mahakamani na mwanamke, atasikilizwa yeye kwanza, hadi uje usikilizwe wewe, umeshachakaa".

Ndugu zangu wote mnaosema hao wanaume ni ma zwazwa inawezekana hamjapitia changamoto za hawa wanawake. Hata kama hamjapitia ila kila mtu atakua amewahi kushuhudia mwanamke akimtunishia mwanaume, kama ile, "nipige, nipige sasa, nipige kama kweli wewe mwanaume" kwenye hali hii wanaume wengi huamua kuwaacha tu hawa wanawake bila kuwafanya chochote. Si kwamba hawana uwezo wa kuwapiga, la. Huwa wanaepusha shari.

Ukienda police kushitaki kuwa mkeo anakufanyia chochote kibaya hutasikilizwa, ila yy akienda hata kama akasema tu ulimtishia kumpiga, kimbembe unacho. Kuna msemo unasema "A men is guilty until is proved innocence and a woman is innocent until is proved guilty". Hao wanaume kwenye video ni wakuwaonea huruma tu na sio kuwacheka.
Niishie hapa
 
Nimecheka sana....Ila wanaume wa siku hizi mnadeka sana, mmepoteza Ile masculinity......Yani kupigwa na kijistuli na hivo vijikovu ndo habari ya kutangazia...
Aibu kubwa hii,kutwa kucha kulialia mara kupigwa yani wanatudhalilisha aisee. Na kwa akili hizo, watadundwa mpaka wang'olewe macho.
 
wanaume bado hatujasema,

na tutasema mbona
Kweli kabisa, hadi tuseme kwa sababu hawa wanawake tuliwapa makali sisi wenyewe baada ya mamlaka za nchi za magharibi ambazo kimsingi zilikua zikiongozwa na wanaume zilipoamua kuwa promot na kuwatetea wanawake kwa kila namna hadi kutunga sheria za kulinda mwanamke.

Hili hii imewafanya wanawake wengi wamini kuwa manaume ni adui zao. Hivyo hupambana sana kushindana na adui zao ambao ni wanaume, na wakifanikiwa tu, wanaume hukiona cha moto
 
Back
Top Bottom