Mhandisi Mzalendo
JF-Expert Member
- Aug 23, 2010
- 6,682
- 11,461
Issue sio udalali hapa. Malori ya mchanga yanaingia kwenye eneo lenye barabara ya kuingia kwake na pia kwenda shule ya sekondari na kufanya uharibifu wa barabara. Yeye Kawambwa na huyo mwingine aliyedhalilishwa DSO Mstaafu wa Kawe na Bagamoyo Madondola waliamua kuweka vigogo vya mnazi ili malori yasipite na kuharibu barabara ndipo walipokutwa na huyo Hassan Wembe Diwani mstaafu wa Kiromo na beki ya zamani ya timu ya Malindi Zanzibar. Wembe ni mmiliki wa mashimo ya mchanga huko Kiromo kwahiyo kuzibwa Kwa barabara kunazuia malori kuingia na hivyo kukosa fedha. Mhusika huyo wlWembe na washirika wenzie walikamatwa jana na wako lokapu hadi sasa. Nadhani jambo limekuwa kubwa kwani mmoja ya waliodhalilishwa ni DSO Mstaafu na DSO Bagamoyo kasimamia zoezi zima kuhakikisha wanakamatwa !